Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Sospeter B, MD
Imeboreshwa:
7 Septemba 2025, 04:21:41

PrEP: Matumizi, Madhara na Tahadhari kwa Mtumiaji
Swali la msingi
“Nimejikuta nikijisaidia choo cheusi kinachonata, chenye harufu mbaya isiyo ya kawaida… halafu nahisi kizunguzungu mara kwa mara, hasa nikisimama. Sina maumivu yoyote makali, lakini hali hii inanitia wasiwasi. Inaweza kuwa nini? Je, ni chakula tu au kuna jambo kubwa zaidi linaloendelea mwilini mwangu?”
Majibu
Kujisaidia choo cheusi na kinachonata ni dalili ambayo mara nyingi huashiria uwepo wa damu iliyovuja kwenye sehemu ya juu ya mfumo wa chakula kama vile tumbo au utumbo mdogo wa juu. Iwapo dalili hii inaambatana na kizunguzungu, inaweza kuwa ishara ya upungufu wa damu (anemia) au kushuka kwa shinikizo la damu, jambo ambalo ni hatari na linahitaji tathmini ya haraka ya kitabibu.
Maana ya choo cheusi kinachonata (Melena)
Melena ni hali ya kujisaidia choo cheusi sana, laini au kinachonata, na chenye harufu kali isiyo ya kawaida. Rangi hiyo nyeusi hutokana na kumeng’enywa kwa damu tumboni au sehemu ya juu ya utumbo mdogo (duodenam), ambapo damu inapogusana na asidi ya tumbo, hubadilika na kuwa nyeusi.
Dalili zinazoambatana
Choo cheusi kinachonata (melena)
Kizunguzungu
Uchovu usioelezeka
Mapigo ya moyo kwenda haraka
Kushindwa kusimama kwa muda bila kuhisi mzunguko
Rangi ya ngozi kuwa hafifu au kuchanganyikiwa ikiwa upotevu wa damu ni mkubwa
Visababishi vya hoo cheusi kinachonata
Kuna visababishi mbalimbali vya hali hii, baadhi ya visababishi vya mara kwa mara vya choo cheusi kinachonata ni pamoja na;
1. Vidonda vya tumbo
Vidonda kwenye tumbo au duodenum huweza kuvuja damu na kusababisha choo kuwa cheusi. Hii mara nyingi huhusishwa na maumivu ya tumbo yanayopungua baada ya kula au kutumia dawa za kuzuia uzalishaji wa tindikali tumboni. Sababu za vidonda ni pamoja na:
Maambukizi ya Helicobacter pylori
Matumizi ya muda mrefu ya dawa kama aspirin, ibuprofen, au diclofenac
2. Kutokwa damu kwenye mfumo wa juu wa chakula
Sababu kuu ni:
Kupasuka kwa mishipa ya damu kwenye umio, hasa kwa wagonjwa wa sirosis ya ini
Gastraitis kali (uvimbe wa ukuta wa tumbo)
Matumizi ya pombe kupita kiasi
3. Saratani ya tumbo au umio
Saratani inaweza kusababisha kutokwa damu polepole au ghafla, na hivyo kusababisha choo cheusi kinachonata na dalili za upungufu wa damu (kizunguzungu, kuchoka, nk.)
4. Matumizi ya dawa
Dawa kama zile za jamii ya NSAIDs (aspirin, diclofenac, naproxen) huongeza hatari ya vidonda vya tumbo na kutokwa na damu.
Dawa za kuzuia damu kuganda(kuyeyusha damu) kama warfarin au heparin pia huongeza hatari ya kutokwa na damu.
5. Kula vyakula au dawa zenye rangi nyeusi (Sababu zisizo za hatari)
Ingawa si kawaida kusababisha choo kinachonata, baadhi ya vyakula au virutubisho kama:
Dawa yenye madini chuma (Vidonge vya nyongeza ya madini chuma)
Dawa za makapi za vizio vya bismuth (mfano Pepto-Bismol)
Vyakula vyenye rangi nyeusi (mfano damu ya mnyama, beetroot)
Hata hivyo, choo kutokana na hivi huwa hakina harufu kali wala haliambatani na kizunguzungu.
Visababishi vya kizunguzungu kinachoambatana na choo cheusi
Kizunguzungu kinapotokea pamoja na melena, mara nyingi ni matokeo ya:
Upungufu wa damu (anemia) – damu inapopotea polepole kupitia njia ya chakula, mwili hupoteza seli nyekundu na oksijeni hupungua, na hivyo mtu huhisi kizunguzungu, kuchoka au hata kupoteza fahamu.
Shinikizo la damu kushuka (Presha ya kushuka unabobadili mkao) – hasa baada ya kupoteza kiasi kikubwa cha damu, mtu husikia kichwa kuzunguka au kupoteza fahamu anaposimama.
Vipimo na uchunguzi
Kwa mgonjwa anayewasilisha dalili hizi, uchunguzi wa haraka ni muhimu. Vipimo vinaweza kujumuisha:
1. Vipimo vya damu
Hemoglobin na hematocrit – kupima kiwango cha damu (kugundua anemia)
FBC (Hesabu kamili ya damu) – kuona dalili za upungufu wa damu au maambukizi
Urea na creatinine – kupima kazi ya figo, huathiriwa na kutokwa damu
Kundi la damu na rhesus – kujiandaa kwa ajili ya kuongezewa damu
2. Kinyesi kwa damu iliyofichika
Hupima uwepo wa damu ambayo haionekani kwa macho ya kawaida kwenye kinyesi
3. Endoscopi
Kutazama ndani ya tumbo na sehemu ya juu ya utumbo kwa kutumia kamera, kubaini chanzo cha damu.
4. Ultrasound ya tumbo au CT scan
Hufanyika kama kuna shaka ya matatizo ya ini au saratani.
Tiba na utunzaji
Matibabu hutegemea chanzo kilichogunduliwa. Hata hivyo, kwa hali ya dharura:
Hatua za dharura
Mgonjwa hulazwa hospitali haraka
Hupewa maji (IV fluids) kurekebisha mzunguko wa damu
Kuwekwa damu iwapo upungufu wake ni mkubwa
Kupumzika na kuchunguzwa shinikizo la damu mara kwa mara
Matibabu maalum kulingana na sababu
Vidonda vya tumbo – dawa za kupunguza asidi ya tumbo (PPI kama omeprazole, esomeprazole)
Gastraitis au maambukizi ya H. pylori – antibiotics pamoja na PPI
Kupasuka kwa mishipa ya damu – tiba ya haraka kwa njia ya endoscopy, wakati mwingine upasuaji
Saratani – huhitaji rufaa kwa oncologist kwa ajili ya tiba ya mionzi, chemotherapy au upasuaji
Tahadhari na ufuatiliaji
Kuepuka matumizi holela ya dawa za maumivu jamii ya NSAIDs bila ushauri wa daktari
Wagonjwa wa vidonda vya tumbo wanapaswa kufuata dawa kikamilifu
Kunywa pombe kwa kiasi au kuacha kabisa
Kufanya uchunguzi wa mara kwa mara kwa watu waliowahi kupata kutokwa damu kwenye mfumo wa chakula
Hitimisho
Kujisaidia choo cheusi kinachonata na kizunguzungu si jambo la kawaida na mara nyingi huashiria kutokwa na damu kwenye mfumo wa juu wa chakula. Hii ni hali ya dharura inayohitaji matibabu ya haraka. Ikiwa unajikuta na dalili hizi, usisubiri – wasiliana na kituo cha afya kilicho karibu nawe kwa uchunguzi wa haraka.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeandikwa,
7 Septemba 2025, 04:20:13
Rejea za mada hii
Grant RM, Lama JR, Anderson PL, McMahan V, Liu AY, Vargas L, et al. Preexposure chemoprophylaxis for HIV prevention in men who have sex with men. N Engl J Med. 2010;363:2587–99.
Baeten JM, Donnell D, Ndase P, Mugo NR, Campbell JD, Wangisi J, et al. Antiretroviral prophylaxis for HIV prevention in heterosexual men and women. N Engl J Med. 2012;367:399–410.
World Health Organization. Consolidated guidelines on HIV prevention, diagnosis, treatment and care for key populations. Geneva: WHO; 2016.
McCormack S, Dunn DT, Desai M, Dolling DI, Gafos M, Gilson R, et al. Pre-exposure prophylaxis to prevent the acquisition of HIV-1 infection (PROUD): effectiveness results from the pilot phase of a pragmatic open-label randomised trial. Lancet. 2016;387:53–60.
Centers for Disease Control and Prevention. Pre-exposure prophylaxis (PrEP). 2022. Available from: https://www.cdc.gov/hiv/basics/prep.html
