top of page

Mwandishi:

WAMJW

Mhariri:

10 Oktoba 2021 13:04:39

Unaweza kuchanganya chanjo kama ya awali haipatikani?

Je kama mtu amechanjwa chanjo ambayo anatakiwa kupata dozi mbili akachoma dozi ya kwanza na wakati anaenda kuchanjwa dozi ya pili akakuta ipo J&J ambayo wanachoma dozi moja anaweza kuchoma?

Ndiyo!

Mtaalamu wa afya ataangalia aina ya chanjo mtu alipewa awali. Kama chanjo aliyopewa awali imetengenezwa kwa kutumia teknolojia sawa na J&J ataweza kuchoma. Pia kama kama siku 28 zimepita kutokea siku aliyochanjwa anaweza kupokea chanjo ya J&J


Utafiti nchini Uingereza (Com- CoV Study) umeonyesha ufanisi mtu akipokea chanjo ya kwanza ya AstraZeneca ikifuatiwa na chanjo ya pili ya Pfizer. Tafiti bado zinaendelea ili kubaini ufanisi na madhara ya uchanganyaji wa aina tofauti za chanjo. Kwa ushahidi uliopo hadi sasa, inashauriwa kutumia aina ile ile ya chanjo.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

10 Oktoba 2021 13:04:39

Rejea za mada hii

bottom of page