Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
ULY CLINIC
29 Novemba 2024, 13:44:21

Unaweza kupata mimba baada ya kutoa mimba?
Ndio, inawezekana kupata ujauzito baada ya kutoa kwani kutoa mimba hakuathiri uwezo wako wa kupata ujauzito mwingine.
Unaweza kupata ujauzito mwingine wiki chache baada ya kutoa mimba. Baada ya kutoa mimba mzunguko mpya wa hedhi huanza na uovuleshaji unaweza kutokea siku ya 14 kwa mzunguko wa siku 28 au mapema zaidi kwa mzunguko mfupi. Hata hivyo kutolewa kwa yai hutegemea umri wa ujauzito wakati wa kutolewa, hivyo hatari ya kupata ujauzito huongezeka endapo mimba ilikuwa na wiki chache ukilinganisha na mimba kubwa.
Mambo ya kuzingatia
Unshauriwa kutumia njia ya uzazi wa mpango ikiwa haujapanga kupata ujauzito mwingine ili kuzuia mimba isiyotarajiwa.
Ikiwa unapanga kupata ujauzito onana na daktari wako kwa uchunguzi na vipimo kabla ya kubeba ujauzito mwingine
Wapi utapata maelezo zaidi?
Kupata maelezo zaidi kuhusu kupata ujauzito baada ya kutoa mimba bofya hapa
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
17 Machi 2025, 16:18:35
Rejea za mada hii
Pregnancy After Miscarriage: From Risks to Rainbow Babies.Healthline https://www.healthline.com/health/pregnancy/pregnancy-after-miscarriage. Imechukuliwa 29.11.2024
Pregnancy: Ovulation, conception and getting pregnant. my.clevelandclinic.org/health/articles/11585-pregnancy-ovulation-conception--getting-pregnant. Imechukuliwa 29.11.2024
Pregnancy after miscarriage: What you need to know - Mayo Clinic. https://www.mayoclinic.org/healthy-lifestyle/getting-pregnant/in-depth/pregnancy-after-miscarriage/art-20044134. Imechukuliwa 29.11.24