top of page

Mwandishi:

Dkt. Benjamin L, MD

Mhariri:

Dkt. Charles W, MD

11 Oktoba 2021, 05:31:21

Unaweza pata kinga ya COVID-19 kwa kuongezewa damu ya mtu aliyechanja?

Je, unaweza pata kinga ya COVID-19 kwa kuongezewa damu ya mtu aliyechanja?

Hapana!


Chanjo za COVID-19 ikiwa pamoja na chanjo za mRNA au za vekta, humeng’enywa na mwili muda mfupi mara baada ya kuingia kwenye chembe hai, na hakuna ushahidi kwamba kupokea damu kutoka kwa mtu aliyechoma chanjo kunaleta madhara kwa anayeongezewa damu.


Licha ya hivyo imeonekana pia kuwa, kupokea damu kutoka kwa mtu aliyechanjwa hukusababishi ugonjwa wa COVID-19 walakumlinda mpokeaji dhidi ya maambukizi ya kirusi cha COVID-19.


Mashirika ya kiafya yanazungumziaje kuhusu uchangiaji damu?


WHO, FDA na NBTC na mashirika mengine ya afya yametoa mapendekezo mbalimbali kuhusu uchangiaji damu kutoka kwa mtu aliyechoma chanjo kama inavyoonekana katika aya zinazofuata.


  1. Wapokeaji wa chanjo yenye kirusi hai kilichotolewa makali wanapaswa kusubiria kwa muda wa wiki 4 kabla ya kuchangia damu, hii ikiwa sawa na utaratibu wa kawaida wa sasa.

  2. Watu wanaojisikia vibaya baada ya kupokea chanjo ya COVID-19 hawapaswi kuchangia damu kwa muda wa siku 7 au zaidi mpaka pale dalili zitakapopotea ndipo waruhusiwe kuchangia damu

  3. Kwa taasisi ambazo haziwezi kufahamu kama mchangiaji wa damu amepokea chanjo yenye kirusi hai cha COVID-19, wanapaswa kumpa mgonjwa wiki 4 kabla ya kupokea damu kutoka kwa mchangiaji.

  4. Wachangiaji damu kutoka kwa waliojitoa kufanyiwa tafiti kwa kuchanjwa chanjo hai cha COVID-19 kilichotolewa makali, wanapswa kutochangia damu kwa miezi 12 mfulilizo tangu kupokea damu, isipokuwa kama chanjo itahalalishwa ramsi.

  5. Wachangiaji damu kutoka kwa waliojitoa kufanyiwa tafiti kwa kuchanjwa chanjo isiyo hai ya kirusi cha COVID-19, wanapswa kutochangia damu kwa siku 28 mfulilizo toka wamepokea chanjo, isipokuwa kama chanjo itahalalishwa ramsi.


Chanjo


Mfano wa chanjo hai ya kirusi cha COVID-19 kilichofifishw amakali ni Covishield


Soma zaidi kuhusu aina zingine za chanjo za COVID-19 kwa kubofya hapa

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

11 Oktoba 2021, 06:47:38

Rejea za mada hii

  1. Canadian blood services. COVID-19 vaccines and blood donation. https://www.blood.ca/en/covid19/vaccines-and-blood-donation. Imechukuliwa 10.10.2021

  2. Gupta, et al. “Blood donor deferral periods after COVID-19 vaccination.” Transfusion and apheresis science : official journal of the World Apheresis Association : official journal of the European Society for Haemapheresis vol. 60,5 (2021): 103179. doi:10.1016/j.transci.2021.103179

  3. Bhasker, B. “Covid 19 vaccination: Latest guidelines on blood donor deferral in India.” Transfusion clinique et biologique : journal de la Societe francaise de transfusion sanguine vol. 28,3 (2021): 299. doi:10.1016/j.tracli.2021.05.005

  4. United States Food and Drug Administration updated information for blood establishments regarding the COVID-19 pandemic and blood donation.  https://www.fda.gov/vaccines-blood-biologics/safety-availability-biologics/updated-information-blood-establishments-regarding-covid-19-pandemic-and-blood-donation?utm_medium=email&utm_source=govdelivery. Imechukuliwa 10.10.2021

  5. Singapore Health Sciences Authority . 2021. COVID-19 vaccine and blood donation guidelines. available from https://www.hsa.gov.sg/blood-donation/covid-19-vaccine. Imechukuliwa 10.10.2021

bottom of page