top of page

MAMBO YA KUFANYA KABLA YA KUPATA UJAUZITO
 

Imeandikwa na ulyclinic

Je unafikili kupata ujauzito/mimba?

 

Kuna mambo mengi unayotakiwa kufanya kabla ya kupata ujauzito/mimba , mambo haya si kwa ajili ya afya yako tu bali ni pamoja na kulinda afya ya mwanao na kupata mtoto bora mwenye akili safi na uwe na familia yenye furaha inayokuzunguka

Tabia hizi/mambo haya unatakiwa uzingatie kabla hujapata ujauzito

 

1.Acha kuvuta sigara/tumbaku

 

Asilimia 20 ya uzito kidogo kwa watoto wanaozaliwa na uzito kidogo, asilimia 8 ya watoto kuzaliwa kabla ya umri/njiti na asilimia 5 ya vifo vya watoto wakati wa kuzaliwa husababishwa na uvutaji sigara/tumbaku. Licha ya kusababisha matatizo kwa mama na mtoto uvuaji huu umeonekana kusababisha ugumu wa kupata mimba kwa wanawake, pia kemikali zilizo kwenye sigara hupunguza kichochezi cha estrogeni. Mbali na hivyo ukiacha uvutaji sigara unapata uwezekano wa kupata mimba haraka na pia kupata mtoto mwenye afya bora

 

2.Kupata vidonge vya Madini ya foliki asidi (folic acid) ni ya muhimu

Wanawake wengi wanapopata mimba hujua umuhimu wa madini haya kwamba huzuia kupata watoto wenye matatizo ya kuzaliwa nayo(congenital defects) kama tundu kwenye mgongo na matatizo mengine ya mfumo wa fahamu yanayotishia uhai wa mtoto, lakini  hawajui kwamba kupata vidonge hivi kabla ya ujauzito, wiki 4,6 hadi 8 kabla ya kupata ujauzito ni muhimu kukuhakikishia kwamba mwili wako unakiwango cha kutosha mwanzoni kabisa kabla mimba haijatungishwa. Hivo ni muhimu kupata vidonge hivi kila siku kabla ya ujauzito

 

3.Acha matumizi ya pombe na vinywaji vya caffein

Ni muhimu kuacha matumizi haya hasa pale unapohisi unataka kupata ujauzito maana huwa na madhara kwa mtoto. Baada ya kumaliza hedhi (bleeding) mzunguko unaofuatia huwa wa muhimu sana maana mimba huweza kutungwa kwa kipindi hiki hivo endapo unajua unataka kupata mimba basi ni vyema ukaacha vinywaji hivi. Lakini endapo umepata mimba na hukujua na ulikuwa unatumia vinywaji hivi basi unaweza kuendelea na mimba hiyo ila unatakiwa uache matumizi hayo. Pombe husababisha kuzaa mtoto mwebye matatizo katika mfumo wa fahamu na kumsababishia mtoto kuwa na uelewa hafifu na pia kuzaliwa na uzito kidogo.

 

4.Fanya vipimo vya magonjwa mbalimbali

Magonjwa ya zinaa/sexual transmitted disease (STD) ni hatari kwani huweza kumdhuru mtoto na kusababisha matatizo ya kuzaliwa nayo kama upofu, magonjwa haya huweza kusababisha mimba kuharibika/ kutoka na pia ni muhimu kupata chanjo ya magojwa ya tete kuwanga n.kpia  endapo dakitari ataona unatatizo lolote basi utapata matibabu kabla hujapata ujauzito.

 

5.Pumguza uzito

 

Fanya hivi unauzito zaidi ya kiwango, watu wenye uzito zaidi ya kiwango wanahatari ya kupata matatizo mengi wakati wa ujauzito kama, magonjwa ya moyo, kisukari, saratani (kama ya ukuta wa ndani wa mfuko wa kizazi-endometritis,ziwa-breast utumbo mpana-colon). Pia wanawake wenye uzito kidogo wanapata matatizo mbalimbali kweye uzazi, tatizo hili la uzito sio kwamba uache kula, ni kula mlo kamili na mazoezi. Kama unauzito mkubwa au mdogo ongea na dakitari ili kujua njia zipi unaweza kutumia kupunguza uzito huo.

 

6.Jifunze historia ya familia yako

 

Kujifunza historia ya familia yako inaweza kukusaidia kutambua magonjwa ambayo yanarithiwa kwenye familia yako, hivyo dakitari wako ataweza kukushauri mambo ya kufanya ili kuweza kupata familia bora. Mfano ugonjwa wa sickle cell (SCD) hurithiwa na endapo ugonjwa huu upo kwenye familia basi dakitari anaweza kukushauri na kukupima wewe na mpenzi wako kuona kama mna vinasaba-genes za ugonjwa huu vinavyoweza kusafilishwa kwa mtoto. Kufanya hivi unazuia hatari ya kupata mtoto mwenye matatizo mbalimbali au kujipanga na mambo yanayoweza kutokea

 

7.Pata ushauri wa dakitari

 

Dakiari anaweza kukuuliza historia mbalimbali za maisha yako kuhusu magonjwa ulionayo na jinsi yanavyoweza kukudhuru ukiwa mjamzito , hivyo kabla hujapata ujauzito ni vema kumwambia dakitari kuhusu magonjwa hayo  pia unaweza kumkubusha dakitari wako kama asipokuuliza kuhusu ugonjwa ulio nao

 

Endapo unamatatizo/magonjwa sugu na unatumia dawa  kama magonjwa ya moyo, kisukari, kifafa, msongo wa mawazo, ugonjwa wa migraine(maumivu ya kichwa ya musimu) na mengine basi pata ushauri wa dakiari maana dawa hizi huathiri ukuaji na utengenezwaji wa mtoto

Mambo mengi dakitari anaweza kukupima na kukupa ushauri na hivo ni muhimu sana endapo utaonana na dakitari kabla hujapata ujauzito.

 

8.Pata tiba ya kiakili

 

Akili ni jinsi tunavyo fikiri, hisi, tenda na kuendana na hali ya maisha, na ikiwa unamatatizo kama vile unajisikia hofu zaidi ya kawaida na una huzuni, au misongo ya mawazo  ni vema ukaonana na dakitari ili ajue unatatizo gani na aweze kukupa ushauri na matibabu sahihi

imechapishwa 5/1/2015

imeboreshwa 14/11/2018

ambo ya ufanya kabla yaujauzito
bottom of page