top of page

Aspiration nimonia kwa vichanga

 

​

Imenadikwa na madaktari wa uly clinic

​

Utangulizi

​

Wakati wa uchungu uliopitiliza na uzazi mgumu, kichanga tumboni huanza kupumua haraka haraka kwa sababu ya kutopata hewa safi ya kutosha kupitia kitovu kwa sababu ya mgandamizo. Kwenye hali hii mtoto anaweza kuvuta majimaji na kuingia kwenye mapafu yaliyochanganyika na kinyesi, nwele, damu,na seli  na uchafu mdogo na bakteria kutoka kwenye mlango wa uzazi. Hivi vitu husababisha kuziba kwa mirija midogo ya hewa kwenye mapafu na kusababisha kuvurugika kitendo cha mbadilishano wa hewa safi na hewa chafu kwenye mapafu. Kama bakteria wakivutwa kuingia kwenye mfumo wa hewa huweza kusababisha nimonia kwa jina jingine huitwa aspiration nimonia.

 

Mtoto anaweza kupata nimonia aina hii pia endapo ana fistula kati ya umio na trakea(mrija unaoingiza hewa kwenye mapafu) yaani tracheoesophageal fistula, endapo umio limeziba mwinshoni , tatizo la kubeuka, kumlisha mtoto vibaya, kutumia madawa ya kulewesha mwili.

 

Kuzuia uvutaji wa vilivyomo tumboni kwenda kwenye mfumo wa hewa, mtoto atawekewa mpira utaoingia tumboni kabla ya upasuaji wa kurekebisha tatizo hili la fistula.

 

Dalili

 

  • Homa kwa kichanga baada ya kuzaliwa

  • Kushindwa kupumua vema

  • Kupumua haraka haraka zaidi ya kichanga wa kawaida

 

Matibabu ya nimonia aspiration huhusisha kutibu dalili na kupewa dawa za kupambana na bakteria husika kwa njia ya mishipa. Uhauheni hupatikana kwenye siku ya 3 hadi 4.

 

Endapo mtoto atapata shida wakati wa kuzaliwa au akazaliwa akiwa amepakazwa kinyesi cheusi kwenye mwili basi atapewa dawa za mishipa ili kuzuia maambukizi kwenye damu na nimoni kwa kichanga.

Kumbuka nimoni aspiration ni hatari kwa mtoto na huweza kusababisha kifo hivyo wahi hospitali uhisipo dalili za hapo juu kwa matibabu.

 

 

Kama unahitaji msaada au una swali  wasiliana na daktari wako, unaweza kututafuta kupitia namba zetu chini ya tovuti hii

​

​

Toleo la 3

Imeboreshwa 8/2/2019

bottom of page