Kujikinga dhidi ya saratani ni muunganiko wa mambo na matendo yanayofanywa au kuzingatiwa ili kujikinga na hatari ya kupata saratani ambazo zinazuilika
Kwa kujikinga na saratani unapunguza idadi ya wagonjwa wapya katika Jamii na pia vifo vinavyotokana na saratani. Wanasayansi katika juhudi za kutafuta namna ya kuzuia saratani mpya kutokea wameweza kuelezea mambo mawili yanayomlinda mtu kupata saratani na mambo yanayo muweka mtu kupata saratani
Mambo yanayo muweka mtu katika hatari ya kupata saratani baadhi yake yanaweza kuzuilika na mengine hayazuiliki kwa mfano, uvutaji wa sigara na mtu kuwa na historia ya saratani kwenye familia yao humweka mtu hatarini kupata saratani mbalimbali, lakini uvutaji wa sigara tu ndio unaweza kuzuilika.
Kuna mambo mbalimbali ya kufanya ili kuzuia saratani kuanza au kuenea mwilini, mambo hayo ni pamoja na;
Kubadili mfumo wa maisha na mfumo wa kula
Kwa kula chakula bora na chenye afya kikihusisha matunda kwa wingi na nafaka zisizokobolewa, vyakula vinavyotokana na nafaka halisi mfano maharagwe, mahindi na mtama, chagua kula vyakula visivyonenepesha kwa au kuzuia mafuta ya wanyama na vyakula vyenye sukari kwa wingi.
Punguza kiwango cha pombe unachotumia kama huwezi kuacha, unaweza kufanya hivyo kwa kupunguza kiwango cha pombe unachokunywa au idadi ya siku ya kunywapombe. Pombe kitaalamu inaonekana kuwa kihatarishi kikubwa cha kupata saratani ya ini, mapafu, utumbo, titi na figo.
Punguza kula nyama za kusindikwa. Shirika la Afya Duniani WHO limethibitisha kuwa kula vyakula vya kusindikwa huambatana na saratani mbalimbali. Chagua vyakula aslia mfano vyakula vya nafaka, vyakula jamii ya kunde, mboga za majani na matunda kwa wingi, mafuta mazuri ya kupikia mfano mafuta ya mzeituni, mafuta ya alizet, mafuta ya ufuta, nyama nyeupe mfano samaki na kuku badala ya nyama nyekundu mfano ya mbuzi na n'gombe
Imarisha mwili wako
Kwa kufanya mazoezi kwa mda wa dakika 30 kwa siku, hakikisha mwili wako unafanyamazoezi au kazi zinazosababisha utoe jasho, hakikisha pia unakuwa na uzito unaoshauriwa kiafya. Kusoma zaidi kuhusu uzito unaoshauriwa kiafya bonyeza hapa
Kupata dawa au chanjo zinazoaminika kupunguza au kuzuia saratani au kuzuia saratani kuanza au kuendelea kuhudru mwili. Mfano chanjo dhidi ya kirusi cha hepatitis B kinachosababisha saratani ya ini, Kirusi cha HPV kinachosababisha saratani ya shingo ya kizazi n.k
Zuia na ondokana na tabia hatarishi mfano ngono zembe (kufanya mapenzi bila kutumia kondomu, au ngono ya uume kwa haja kubwa), punguza idadi ya wapenzi- kuwa na wapenzi wengi kunaweza kukusababishia kupata maambukizi ya HPV yanayosabaisha saratani ya shingo ya kizazi. Usishiriki kutumia sindano au vitu vyenye ncha kali pamoja na mtu mwingine kwani unaweza kupata maabukizi ya Kirusi cha Hepatitis C ambacho pia husababisha saratani ya
Zuia mwanga wa jua usikupige sana kwa kuzuia kutembea juani wakati wa jua kali, Kama ni lazima kutembea juani hakikisha unatumia nyezo yoyote kukukinga na mwanga huo kama vile mwamvuli au nguo ambazo zinaziba maeneo ya mwili yasipigwe na mwanga wa jua. Kumbuka kuchagua nguo ambazo hazi akisi mwanga wa jua kama vile nguo nyeupe au nyeusi zisizobana, na zisizotengenezwa kwa pamba. Zuia kutumia vidani vinavyobana kwani vinasababisha uungue maeneo ambayo mwanga wa jua unakupiga. Tumia miwani ya jua wakati unatembea juani ili kulinda macho yako na mwanga huo, hili ni lazima kwa watu walio na ualbino
Pata uchunguzi wa daktari na vipimo kwa mda uliojipangia. Unapoumwa ukiwa upo mzima ni vema ukawa na mazoea ya kucheki afya yako na kufanya vipimo mbalimbali ambavyo daktari atakushauri kuvifanya ili kucheki afya yako na kugundua mapema magonjwa ambayo yanaweza kuwa mwilini au ishara za saratani.
Madaktari wa uly clinic wapo kwa ajili ya kukupa Tiba na ushauri endapo utahitaji, wasiliana nasi kwa whatsapp namba zilizo chini ya tovuti hii au kupitia email zetu. Karibu sana
Comments