top of page

Tatizo la manjano kwa vichanga


Manjano kwa Kichanga aliyezaliwa


Imeandikwa na madaktari wa ULY-Clinic


Mara baada ya mtoto kuzaliwa, mkunga ama mtaalamu wa afya ataukagua mwili wote wa mtoto kwa umakini sana ili kutambua kama kuna tatizo lolote amezaliwa nalo , moja ya kitu ambacho kitaangaliwa ni manjano kwa kichanga. Manjano kutokea kwa mtoto ni kitu cha kawaida, ila kiwango cha manjano kikizidi kiwango cha kawaida basi lazima hatua za dharura zichukuliwe. Manjano hutokea mara nyingi kwa watoto wanao nyonya maziwa na huweza kudumu kwa kipindi kirefu. Madaktari bado hawajaunda utaratibu wa jinsi gani manjano itibiwe wakati wa kunyonyesha na kwa namna gani

Nini maana ya manjano kwa mtoto aliyezaliwa?

Manjano ni hali inayoweza kujitokeza kwa watoto wanaozaliwa, mtoto hubadilika rangi ya macho ama ngozi kuwa njano. Mara nyingi rangi ya manjano ya mtoto mweupe huonekana vema kuliko ya mtoto mwenye rangi nyeusi. Kutokea kwa Manjano huweza kusababishwa na mambo tofauti ambayo ni


· Ugonjwa unaoendelea ndani ya mwili

· Sababu za kifisiologia kwa mtoto

· Manjano ya kunyonya maziwa

· Manjano ya kutonyonya maziwa


Manjano ya ugonjwa

Aina hii ya manjano mara nyingi hutokea siku ya kwanza yakuzaliwa mtoto

Huweza kusabishwa na hali au madhaifu mblimbali aliyozaliwa nayo mtoto kama tatizo la gilbert syndrome na crigler najjar syndrome, ingia katika kurasa za tovuti hii kusoma kuhusu hali hizi.


Manjano ya kifiziologia

Manjano kutokana na mabadiliko ya kifisiologia ni aina ya manjano inayotokea kwa wingi, ainahii huathiri kwa asilimia 60 ya watoto wanaozaliwa na manjano, licha ya hivyo huoneka wiki ya kwanza ama ya pili toka siku ya kuzaliwa.

Aina hii hutokea kutokana na kuzidi kwa kiwango cha kemikali ya bilirubini kwenye damu. Bilirubini ni kemikali inayozalishwa kwa kuvunjwa vunjwa chembe nyekundu za damu. Mtoto huwa na chembe nyekundu za damu nyingi sana wakati anazaliwa, chembe hizi huishi mda mfupi na hivyo huvunjwa vunjwa na kuzalisha bilirubid na madini chuma mda wake unapofika. Mtoto anapozaliwa ini lake huwa na uwezo mdogo wa kubadilisha kemikali hi ya bilirubini ili kutolewa kwenye mkojo na kinyesi, endapo uzalishaji wa bilirubin ni mkubwa kuliko utoaji kwa njia tajwa, matokeo yake ni kukusayika kwa kemikali ya bilirubin kwa wingi katika damu. Kemikali ya birilubini kwa kuwa inauwezo wa kuoenyeza kwenye ngozi basi huleta rangi ya njano kwenye ngozi na macho.

Manjano kutokana na maziwa

Manjano aina hii hutokea siku ya 3 hadi ya 5 hadi baada ya kuzaliwa na pia huendelea huzidi sana kwenye wiki la pili na hupotea kati ya wiki ya tatu hadi ya 12 baada ya kuzaliwa. Manjano hii kwa jina jingine inaitwa manjano ya kifiziolojia inayoendelea. Mpaka sasa hakuna sababu inayofahamika nini husababisha manjano hii. Kuna sababu zinazohusianishwa kwamba zinaweza kuwa na mchango katika kuleta tatizo la manjano kama vile, kiwango cha kemikali ya nonesterified fatty acid kutoka kwenye maziwa ya mama husababisha utendaji kazi wa vimengenya ini kutofanya kazi vizuri ya kusafisha au kutoa bilirubin, pia kuna kiwango cha homoni ya progesterone inayotolewa na mama, mazao yanayotokana na uvunjwaji wa homoni hii pia husababisha utendaji kazi wa vimengenya ini kushindwa kusafisha bilirubin katika damu.


Hata hivyo maziwa ya mama huwa hayana tatizo, na endapo motto anapata manjano kwa sababu ya maziwa haina haja ya kumwachisha kunyonya


Manjano kutokana na kunyonya maziwa Kidogo

Aina hii ya manjano hutokea kwa watoto endapo hawanyonyi au hawanyonyeshwi maziwa ya kutosha. Mara nyingi hutokea ndani ya siku 3 za kwanza mtoto alipozaliwa. Kwa kawaida mtoto anatakiwa anyone maziwa ya kutosha na anaponyonya maziwa ya kutosha utumbo wake huweza kufanya kazi vizuri na kupitisha kinyesi kwa haraka kwa sababu hushiba. Asiponyonya maziwa ya kutosha husababisha bilirubin kukaa mda mrefu kwenye tumbo, na hivyo kufyonzwa. Haya yote yanatokea pale mtoto anapokuwa anakosa kujisaidia haja kubwa. Hivyo mtoto kwenda haja kubwa husaidia kusafisha kemikali hizi za bilirubin, na hili linawezekana kufanyika endapo mtoto atanyonya maziwa yakutosha


Nini Matibabu gani ya manjano yaliyopo?

Kama kiwango cha bilirubin katika damu kipo chini ya miligramu 20 kwa mtoto aliezaliwa kwenye siku zake za matarajio, ana afya njema, basi matibabu yafuatayo yanaweza kufanyika kwa ajiri ya manjano kutokana na maziwa au kutokana na kunyonya maziwa ya mama.


Ongeza kiwango cha kunyoshesha mpaka mara 8 hadi 12 kwa siku.

Njia muhimu ya kupunguza kiwango cha bilirubin ni kupunguza kiwango hicho kukaa katika tumbo mda mrefu, na njia nzuri ni kumnyonyesha mtoto ili kusaidia apate haja kubwa ambayo hubeba kiwango cha bilirubin

Kaa na mtu mzoefu akufundishe kwa jinsi gani ya kumweka mtoto katika titi ili anyone vema, apate kiwango kizuri cha maziwa. Kumweka mtoto katika mkao mzuri kutamsaidia kunyonya maziwa ya kutosha

Kama kiwango cha birilubini kinazidi miligramu 20 katika damu, basi ni vema kuacha kunyonyesha maziwa ya mama ama ya chupa kwa masaa 24 na kuanza matibabu ya mwanga wa bluu ambayo hufanyika hosptali. Kwa namna hii kiwango cha bilirubini hupungua na kisha mama anaweza kuendelea kumnyonyesha mtoto baada ya masaa 24 kupita.


Kama mtoto hana afya njema na ni mtoto njiti, matibabu yatafanywa na mtaalamu wa afya kutokana na hali ya mtoto alivyo


Mambo yakutofanya


Kumpa mtoto maji ya sukari kwa ajiri ya kufidia kiwango cha maziwa anachotakiwa kupata hairuhusiwi kwa sababu itasababisha kupanda kwa kiwango cha bilirubini. Sukari huingilia usafishaji na unyonyaji wa bilirubini hivyo kuleta manjano zaidi


Kuacha kumnyonyesha mtoto. Hili litasababisha kupanda kwa kiwango cha birilubini na pia mtoto kukosa virutubisho.


Manjano huweza kuzuilika?


Manjano hutokea kwa asilimia 50 hadi 70 ya watoto wanaozaliwa. Hakuna njia ya kuzuia manjano, ila kinachotakiwa ni kuzuia kiwango cha manjano kuongezeka na kuleta madhara. zingatia ushauri wa hapo juu na ushauri wa dakitari anayekuhudumia


Imechapishwa 3/3/2015

Imeboreshwa 12/11/2018

Chapisho la 2

53 views0 comments

Recent Posts

See All

ความคิดเห็น


bottom of page