top of page

Saratani ya wilms’

Imeandikwa na madaktari wa uly clinic

Saratani ya wilms’ ni saratani ya figo inayotokea kwa unadra sana na awali huwadhuru watoto, kwa jina jingine inafahamika kama nephroblastoma. Saratani hii huwa ni miongoni kati ya saratani za figo zinazotokea sana kwa watoto. Saratani ya wlms’ huwadhuru watoto walio katika umri wa miaka 3 hadi 4 na hutokea kwa nadra kwenye umri zaidi ya miaka 5.

Saratani ya wilms’ hutokea kwenye figo moja ingawa inaweza kutokea kwenye figo zote mbili.

Kuboreshwa kwa vipimo utambuzi na matibabu ya saratani hii imefanya kuongeza matokeo mazuri ya matibabu kwa watoto wenye saratani hii. Matokeo ya matibabu kwa watoto mara nyingi huwa mazuri.

 

Dalili

 

Saratani ya wilms’ mara nyingi huwa haiambatani na dalili au viashiria. Watoto wenye saratani hii huweza kuonekana wana afya njema, au wanaweza kupata dalili na viashiria kama;

 

  • Uvimbe tumboni

  • Uvimbe wa tumboni  unaoweza kuhisika ukishikwa

  • Maumivu ya tumbo

  • Homa

  • Damu kwenye mkojo

 

Wakati gani wa kumwona daktari

 

Weka miadi na daktari endapo unahisi mwanao ana dalili na viashiria vinavyokupa hofu. Dalili na viashiria vinavyoambatana na saratani ya wilms’ huwa hazipo moja kwa moja kuashiria saratani hii na huweza kusababishwa na mambo mengine pia.

 

Visababishi

 

Haijulikani nini husababisha saratani ya wilms’

Madaktari wanajua kwamba saratani hii huanza pale kunapotokea makosa katika chembe za DNA. Makosa haya huweza kusababisha chembe hai za figo kujizalisha na kuishi mda mrefu kuliko chembe za kawaida. Mkusanyiko wa chembe hizi huanza kuleta uvimbe kwenye figo.

 

Kwa asilimia chache baadhi ya makosa kwenye DNA huweza kurithiwa katika ya kizazi na kizazi na husafilishwa kwa watoto. Kwa watu wengi hakuna uhusiano kati ya watoto na wazazi unaoweza kupelekea kupata saratani.

 

 

 

Vihatarishi

 

 

Mambo ambayo yanaongeza hatari ya kupata saratani ya wilms’ ni huwa pamoja na;

 

  • Kuwa mtu mweusi- watoto wa watu weusi huwa na hatari zaidi ya kupata saratani ya wilms’ mara dufu zaidi ukilinganisha na watu wa asili nyingine.

  • Watoto wa asili ya kiasia huwa na hatari kidogo kuliko watoto wa asili nyingine.

  • Kuwa na historia kwenye familia ya saratani ya wilms’- kama kuna mtoto wa ndugu  wa damu moja kwenye familia amewahi kupata saratani ya wilms’, mwanao anakuwa hatarini kupata saratani hii pia.

  • Saratani ya wilms’ pia hutokea kwa watoto wanaozaliwa na udhaifu Fulani ikiwa pamoja na;

  • Kutokuwa na mboni- mboni ni sehemu ya jicho yenye rangi, watoto hawa huwa na mboni iliyofanyika nusu au kutokuwepo kabisa.

  • Kukua nusu upande wa mwili- mtoto anakuwa mkubwa nusu ya upande wa mwili wake

  • Kutoshuka kwa korodani- korodani moja au zote zinaweza kuwa zimeshindwa kushuka kwenda kwenye pumbu.

  • Hypospadias- kishimo cha mkojo kutofungukia katikkati kwenye ncha ya uume, hivyo hufungukia  sehemu nyingine lakini chini ya uume.

  • Pia saratani ya wilms’ huweza kutokea kwenye mkusanyiko wa dalili Fulani kama;

  • WAGR- W humaanisha saratani ya wilms’, A humaanisha kutokuwepo kwa mboni, na madhaifu katika mfumo wa mkojo na viungo vya siri na M Humaanisha mtindio wa ubongo

  • Debys-Drash- Mtoto anakuwa na saratani ya wilms’, magonjwa ya figo na mtoto wa kiume anazaliwa akiwa na korodani na anaweza kuwa na sifa za kimaumbile ya kike.

  • Beckwith wiedemann- mtoto anazaliwa na matumbo yakiwa nje ya mwili yaani tumbo linakuwa wazi kwenye kitovu, ulimi mkubwa, na kukua kwa organi za ndani ya mwili.

 

 

 

Vipimo na utambuzi

 

Ili kutambua saratani ya wilms’ daktari anaweza kushauri

Kufanya uchunguzi wa mwili- daktari ataangalia viashiria vya saratani hii.

 

Vipimo vya mkojo na damu-vipimo vya damu haviwezi kutambua saratani ya wilms’, lakini inaweza kumsaidia daktari kutambua afya ya mtoto kwa ujumla.

 

Vipimo vya mionzi- kipimo cha CT scan huweza  kutambua asili ya uvimbe ama saratani katika figo, namna ilipotokea na endapo imesambaa sehemu nyingine za mwili

 

Upasuaji- kama mwanao ana uvimbe kwenye figo daktari anaweza kushauri kuondoa uvimbe huoa ama kuondoa figo yote ili kutambua kama uvimbe huo ni saratani au la.

 

Chembe za uvimbe hupimwa kwenye maabara ili kutambua sifa za chembe hizo. Upasuaji hutumika pia kama matibabu ya uvimbe wa wilms’

 

Hatua za ugonjwa

  • Hatua ya 1 saratani ipo kwenye figo moja tu na kwa kawaida inaweza kutolewa kabisa kwa upasuaji

  • Hatu ya 2 saratani imesambaa kwenye tishu na viungo vingine jirani na figo iliyoathiriwa, kama vile mafuta au mishipa ya damu lakini inaweza kutolewa kabisa kwa upasuaji.

  • Hatua ya 3- saratani imesambaa mbali na maeneo ya jirani kama kwenye mitoki ndani ya tumbo na saratani haiwezi kuondolewa yote kwa uapsuaji.

  • Hatu ya 4 saratani imesambaa kwenye viungo vya mbali kama mapafu ini na mifupa au ubongo.

  • Hatua ya 5- saratani ipo kwenye figo zote

 

Matibabu

 

Matibabu ya saratani ya wilms au nephroblastoma mara nyingi huhusisha upasuaji na madawa ya saratani. Lakini matibabu yanaweza kutofautiana iitegemea hatua ya ugonjwa mwilini.

 

Upasuaji

 

Matibabu ya saratani hii mara nyingi huanza na upasuaji wa kuondoa figo yote au sehemu ya figo iliyoathiriwa na saratani. Upasuaji pia hutumika kuthibitisha utambuzi wa saratani hii kwa sababu chembe zilizotolewa huenda kupimwa maabara ili kuona kama kuna chembe zenye sifa za saratani.

  • Upasuaji wa saratani ya wilms huweza kuwa

  • Kuondoa sehemu ya figo iliyoathiriwa

  • Kuondoa figo iliyoathiriwa nachembe za jirani

  • Kuondoa figo zote au sehemu zilizoathiriwa tu- kama saratani imeathiri figo zote mbili, mtoto anapoondolewa figo zote atahitaji figo bandia au mashine itakayosaidia kufanya kazi za figo au kupandikizwa figo kutoka kwa mtu mwingine.

 

Dawa za saratani na mionzi pia huweza kutumika katika hatua Fulani za ugonjwa ili kuleta matokeo mazuri.

Madawa ya kuua chembe za saratani huwa na madhara yake kama kichefuchefu, kutapika, kupoteza hamu ya kula, kupoteza nywele, na kupata maambukizi ya mara kwa mara.

 

Madawa haya huweza kutumika kabla ya upasuaji ili kusinyaza chembe za saratani na baada ya upasuji ili kuua chembe zilizosambaa sehemu nyingine ya mwili.

Toleo la 2

Imeboreshwa 8/12/2018

bottom of page