Tiba ya dawa asilia dhidi ya matatizo mbalimbali ya kiafya
Imeandikwa na waandishi wa uly clinic na kupitiwa na timu ya madaktari wa uly clinic
Bawasili
Bawasiri kwa jina jingine la kitaalamu pile ni vimbe kwenye mishipa ya damu ya vein iliyopo ndani ya tundu la haja kubwa au chini ya ngozi inayotengeneza mlango wa kutolea kinyesi. Vimbe za mishipa hii inaweza kutokana na
-
Kukenya(kutumia nguvu nyingi/kubwa kusukuma kinyesi) wakati wa kujisaidia haja kubwa au
-
Ongezeko la shinikizo la ndani ya mishipa hii wakati wa ujauzito kama mojawapo ya kisababishi.
Bawasiri huweza kuwa sehemu ya ndani kasisa ya njia ya haja kubwa ambapo huitwa bawasiri la ndani au nje ya njia ya haja kubwa na huitwa bawasili la nje
Bawasili ni tatizo linalotokea kwenye umri wa miaka 50, nusu ya watu hawa huwa wanavimba au kuwa na michomo katika mishipa hii ndani au nnje ya mkundu na hutokea na dalili za kuwashwa, hali isiyo ya kawaida maeneo hayo na kutokwa damu
Kwa bahati nzuri matibabu ya aina nyingi ya tatizo hili yapo, wakati mwingine mtu anaweza kupata matibabu ya nyumbani yakiendana na mabadiliko ya mfumo wa maisha.
Dalili za bawasili
-
Kutokwa na damu pasipo maumivu- utaona kiwango kidogo cha damu nyekundu kwenye kinyesi au karatasi ya kutawazia au kwenye choo
-
Miwasho maeneo ya mkundu
-
Maumivu au kutojisikia vyema maeneo ya mkundu
-
Kuvimba sehemu ya mkundu
-
Mchomoko wa uvimbe maeneo ya mkundu unaoweza kuwa na maumivu
-
Kinyesi kutoka chenyewe
Bonyeza mawasiliano yetu yaliyo chini ya tovuti hii kupata Dawa asilia inayoweza kutibu bawasili bila kutumia tiba ya upasuaji, au endapo umefanyiwa operashion basi unaweza kutumia dawa hizi ili kukusababishia upone haraka na kurudi katika hali ya kawaida
Bidhaa hii pia inaweza kutumia kwa watu wanaotaka kujikinga na tatizo la bawasili. Wasiliana na daktari siku zote kuhusu hali yako ya kiafya kwa ushauri zaidi. Pia unawez akutumia madaktari wanaofanya kazi uly clinic kupata ushauri na Tiba sahihi
Miwasho sehemu za siri na Fangasi Ukeni
Miwasho sehemu za siri/Ukeni huweza kusababisha mwanamke kujihisi vibaya sana na haswa akiwa sehemu za watu kwa sababu hali hii humlazimu ajikune au aondoke kwenye shughuli alokuwa anafanya akapate kujikuna maeneo yanayowasha.
Miwasho ukeni huashiria kuna maambukizi au kitu fulani kigeni kimeingia sehemu hizo na hivo lengo la makala haya ni kuzungumzia vitu na maambukizi yanayosababisha miwasho ukeni
Nini husababisha miwasho Ukeni?
Maambukizi mbalimbali yanaweza kusababisha miwasho ukeni kama;
-
Maambukizi ya bakiteria
-
maambukizi ya bakiteria maeneo haya huweza kusababisha miwasho pamoja na kuhisi kama unaungua , kutoa harufu mbaya kama samaki aliyeoza na kutoa uchafu ukeni wa rangi tofauti
-
-
Magonjwa ya zinaa
-
Mambukizi ya fangasi ukeni- wanawake wa 3 kati ya wa 4hupata maambukizi haya maishani mwao. Maambukizi haya hutokea pale ambapo fangas hawa wamezaliana kupitiliza kwa Kuchangiwa na mambo mengi kamvile kinga ya mwili kushuka au kutumia dawa za antbiotik ambazo huua bakteria walinzi
Dalili
Miwasho sehemu za siri huwa dalili tawala kwenye mgonjwa mwenye tatizo la fangasi ukeni
Dalili zingine ni
-
Kuhisi kuungua sehemu za uke
-
Kubadilika kwa rangi sehemu za siri
-
Kuvimba kwa mashavu ya uke
-
Kutokwa na uchafu mweupe mzito kama maziwa mgando unaonata kwenye kuta za uke unaokuwa na harufu kiasi au bila harufu kabisa au kutokuwa na uchafu kabisa au kutokwa na uchafu mwepesi, majimaji na unaoshindwa kutofautishwa na majimaji mengine yanayoweza sababishwa na magonjwa ya zinaa
-
Kuchubuka kwa ngozi au mipasuko ya uke
-
Dalili pia zinaweza ambatana na maumivu wakati wa kukojoa haswa kwenye mashavu na uke, maumivu wakati wa kujamiiana.
-
Dalili huwa kali Zaidi wiki chache kabla ya kuona hedhi
Bonyeza mawasiliano yetu yaliyo chini ya tovuti hii kupata Dawa asilia inayoweza kutibu na kukuondoa katika maambukizi sugu ya Miwasho sehemu za siri na Fungas Ukeni au endapo unapata maambukizi ya amra kwa mara unaweza kutumia dawa hizi kujikinga kupata maambukizi hayo haswa kwa watu wanao tumia vyoo vya kushiriki na walio kwenye mkusanyiko wa watu wengi.
Wasiliana na daktari siku zote kuhusu hali yako ya kiafya kwa ushauri zaidi. Pia unawez akutumia madaktari wanaofanya kazi uly clinic kupata ushauri na Tiba sahihi
UTI Sugu
UTI ni ugonjwa unaosumbua sana wanawake, ugonjwa huu unasababishwa na kupanda kwa vimelea vya bakiteria kutoka ukeni na kuingia kwenye mrija unaotoa mkojo nje ya mwili kutoka kwenye kibofu yaani urethra.
Wadudu hawa wanaweza wasiishie kwenye kibofu tu bali wanaweza kukwea na kufika katika mirija inayotoa mkojo kutoka kwenye figo ijulikanayo kama ureta na hatimaye kuingia kwenye figo. Mfumo wa mkojo kwa binadamu umegawanywa katika sehemu mbili, mfumo wa chini wa mkojo ambao ni kibofu na urethra na mfumo wa juu wa mkojo ambao unaundwa na ureta na figo
Maambukizi ya mfumo wa chini hutokea kwa wingi kuliko ule wa mfumo wa juu, ingawa maambukizi ya mfumo wa juu yanatokea ni kwa nadra sana na endapo maambukizi yatatokea basi maranyingi hua yameambatana na magonjwa/hali zingine kwa mgonjwa kama ugonjwa wa kisukari, watu wanaoitumia dawa za kushusha kinga mwilini, wanaotumia dawa za kutibu Saratani(mionzi na dawa za kumeza au kuwekwa kwenye mishipa), watu waliobadilishiwa figo na magonjwa mengine sugu.
Dalili ya za awali za mtu mwenye UTI ni maumivu wakati wa kukojoa yanayoambatana na
-
Kuwa na haja ya kukojoa mara unapo banwa na mkojo na kwenda haja ndogo mara kwa mara
-
Kuhisi mkojo umejaa kwenye kibofu
-
Kujihisi na hali isiyo ya kawaia kwenye tumbo chini ya kitovu
-
Maumivu nyuma ya mgongo kwenye miishio ya ubavu na maumivu ubavuni kama ukishikwa( ingawa huonekana sana kwenye maabukizi ya mfumo wa juu wa mkojo)
-
Damu kwenye mkojo ingawa ni marachache sana na kwa lugha nyingine inaitwa (hemorrhagic cystitis)
-
Homa, kutetemeka, mwili kuchoka vinaweza kuwepo kwa mtu mwenye maambukizi kwenye kibofu ingawa vinahusiana na maambukizi ya juu ya mfumo wa mkojo (pyelonephritis)
Bonyeza mawasiliano yetu yaliyo chini ya tovuti hii kupata Dawa asilia inayoweza kutibu na kukuondoa katika maambukizi sugu ya UTI au endapo unapata maambukizi ya amra kwa mara unaweza kutumia dawa hizi kujikinga kupata maambukizi hayo haswa kwa watu wanao tumia vyoo vya kushiriki na walio kwenye mkusanyiko wa watu wengi.
Wasiliana na daktari siku zote kuhusu hali yako ya kiafya kwa ushauri zaidi. Pia unawez akutumia madaktari wanaofanya kazi uly clinic kupata ushauri na Tiba sahihi
Uvimbe kwenye kizazi Uterine Fibroids
Fibroids ni Vimbe zisizokuwa na sifa ya saratani, hazibadiliki kuwa saratani zinapotokea kwa mwanamke na si kihatarishi cha kupata saratani katika mfuko wa uzazi.
Vimbe hizi huanza kipindi cha uzazi yaani kipindi mwanamke anauwezo wa kubeba mimba na hutokea sana kati ya umri wa miaka 35- 45. Fibroids au kwa jina jingine ni leiomyoma hukua sehemu mbalimbali za misuli ya mfuko wa uzazi kama, katikati ya misuli ya ukuta wa kizazi au ndani,. Ukuaji wa vimbe hizi huwa wa tofauti sana kati ya mtu na mtu au kati ya uvimbe na uvimbe kwa mtu mmoja.
Vimbe zingine hukua haraka sana na zingine huweza kukua polepole au wakati mwingine kutokua kabisa. Baadhi ya vimbe hizi huweza kuwa kubwa zaidi ya mpira wa miguu kiasi cha kufikia kwenye mbavu na kusababisha matatizo ndani ya tumbo na zingine huweza kuwa ni ndogo sana na kutonekani wala kutoa dalili yoyote na pia wakati mwingine vimbe hizi husinyaa na kupotea kabisa.
Bonyeza mawasiliano yetu yaliyo chini ya tovuti hii kupata Dawa asilia inayoweza kutibu na kuondoa uvimbe wa fibroid bila kufanyiwa upasuaji. Endapo unahitaji kufanyiwa vipimo pia kuhusu kizazi chako unaweza wasiliana nasi
Wasiliana na daktari siku zote kuhusu hali yako ya kiafya kwa ushauri zaidi. Pia unawez akutumia madaktari wanaofanya kazi uly clinic kupata ushauri na Tiba sahihi
Maumivuya nyonga na mgongo
Bonyeza mawasiliano yetu yaliyo chini ya tovuti hii kupata Dawa asilia inayoweza kutibu na kuondoa na maumivu ya mgongo na nyonga bila kufanyiwa upasuaji. Endapo unahitaji kufanyiwa vipimo pia kuhusu kizazi chako unaweza wasiliana nasi
Wasiliana na daktari siku zote kuhusu hali yako ya kiafya kwa ushauri zaidi. Pia unaweza kutumia madaktari wanaofanya kazi uly clinic kupata ushauri na Tiba sahihi
Maumivu na Ganzi kwenye mikono na miguu na maumivu
Ni hali ya kuhisi miguu kuwa ya moto na inauma, hali hii huweza kuwa ya maumivu madogo au makali na wakati mwingine unaweza ukakosa usingizi kabisa wakati wa usiku kwa sababu ya maumivu. Baadhi ya visababishi vya miguu kuwaka moto huweza kuambatana na moja kuhisi miguu inachoma kama sindano au mwiba na mbili kupata ganzi au vyote viwili.
Ingawa uchovu au maambukizi kwenye ngozi huweza kusababisha miguu kuwaka moto kwa mda mfupi na kubadilika mwonekano wake wa kawaida(rangi), kuumia kwa mishipa ya fahamu ya neva huwa ni sababu kuu ya kusababisha miguu kuwaka moto.
Kuumia kwa neva huweza kusababishwa na mambo mbalimbali kama kisukari, ulevi wa pombe wa kupindukia, sumu aina fulani, upungufu wa madini na vitamin (vitamin B), au maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Vifuatavyo ni visababishi vya miguu kuwaka moto kwa undani zaidi;
Visababishi vya miguu kuwaka moto ni
-
Ulevi wa kupindukia(pombe)-( ugonjwa wa kutumia pombe)
-
Maambukizi ya fangas kwenye miguu
-
Ugonjwa wa Charcot marie tooth
-
Kutumia dawa za kutibu saratani
-
Udhaifu wa mishipa ya fahamu
-
Matumizi ya madawa
-
Ugonjwa wa mishipa ya fahamu kutokana na kisukari
-
Upungufu wa homoni (thyroid) ya tezi shingo
-
Upungufu wa vitamin mwilini(kama vile vitamin B)
Bonyeza mawasiliano yetu yaliyo chini ya tovuti hii kupata Dawa asilia inayoweza kutibu na kuondoa Maumivu na Ganzi kwenye mikono na miguu na maumivu . Endapo unahitaji kufanyiwa vipimo pia kuhusu kizazi chako unaweza wasiliana nasi
Ugonjwa wa TB
TB ni ugonjwa unaosababishwa na maambukizi ya bakteria waitwao mycobacteria tuberculosis, Bakteria hawa huambukizwa kwa njia ya hewa. Mtu anapopata maambukizi kwa njia ya hewa kutoka kwa mtu anayekohoa anaweza kutulia kwa mda bila kuonyesha dalili, endapo dalili zitaanza kuonekana basi mtu huyu ataonyesha dalili mbalimbali;
Dalili za mgonjwa wa TB hutegemea mambo mbalimbali ikiwemo umri na hali ya mtu kuwa na magonjwa mengine ama ugonjwa huu umesambaa au umeathiri maeneo gani mengine ya mwili mbali na Mapafu
Dalili kwa ujumla kwa mtu yeyote huweza kuwa kama zifuatazo
-
Kukohoa mfululizo kusikopungua wiki mbili
-
Kupata homa kwa mda wa mwezi mzima
-
Kupata jasho jingi (kiasi cha kulowanisha mashuka) wakati wa usiku
-
Kupungua uzito kusikoelezeka na sababu yeyote
-
Kukohoa damu
-
kupoteza hamu ya kula
-
Maumivu ya kifua ama kushindwa kupumua vizuri
-
Mwili kuchoka
Endapo umepata dalili hizi basi utahitaji kufanyiwa vipimo na kuanza tiba ya miezi 6 hadi 9 kwa kutumia mchanganyiko wa dawa maalumu kuua bakteria hawa. Asante kwa Bidhaa za asilia zinazotengenezwa ambazo zinaweza kutibu TB bila kuwa na madhara makubwa ya dawa. Endapo pia unatumia dawa ambazo si za asilia unaweza kutumia bidhaa hizi asilia kwa ushauri wa daktari tu
Kupata Dawa za kutibu TB au endapo unatumia dawa za kutibu TB na unahitaji kuongeza dawa za asilia basi wasiliana nasi kwa namba zilizo chini ya tovuti hii kuanza Tiba, Kusoma zaidi kuhusu TB bonyeza hapa
Kupunguza uzito na nyama uzembe au kitumbo
Zipo njia aina tofauti za kupunguza uzito wa mwili uliozidi, njia hizo zinaweza kuwa za dawa, mazoezi, kuzingatia chakula au kufanyiwa upasuaji. Kutokana na kuwa na njia za aina tofauti, njia hizi zinaweza kupangwa kwenye mipango au plan 4
Unapaswa ufahamu kwamba, plani za kupunguza uzito zipo za aina tofauti
-
Plan A ni kwa njia ya mazoezi tu
-
Plan B ni kwa njia ya chakula tu
-
Plan C kwa njia ya dawa, lakini plan C imegawanyika katika makundi mawili ambayo ni plan C1 na plan C2
-
Kwenye plan C1 ni kutumia dawa za asilia, na plan C2 ni kutumia dawa za hospitali ambazo umeandikiwa na daktari.
-
Plan D ni kwa njia ya upasuaji au mashine za kuyeyusha mafuta mwilini
Nani anapaswa kutumia plan C (dawa za kupunguza uzito)
Utapata dawa tu endapo umeshindwa kupungua uzito licha ya kuzingatia plani A na B ya chakula nan na mazoezi pamoja na kuwa na
-
Uzito wa mwili wenye BMI Zaidi ya 30
-
BMI kuwa Zaidi ya 27 na una magonjwa yanayotokana na matatizo ya uzito kupita kiasi
Kabla ya kuchagua aina ya dawa daktari atakuuliza maswali mbalimbali kuhusu afya yako, ili kujua kama maudhi madogomadogo au mwingiliano wa dawa unaweza tokea kwa dawa atakazokupa.
Dawa za kupunguza uzito hazipo kwa ajili ya kila mtu kutumia, mfano kwa wamama wajawazito au wale wanaotarajia kupata ujauzito au wanaonyonyeha.
Je dawa hizi zinafanaya kazi vema?
Dawa zote za kupunguza uzito ambazo zinakubalika kutumika kwa mda mrefu zinapunguza uzito. Kuna matokeo mazuri hutokea endapo mtu atatumia njia zote tatu za kuzingatia chakula na mazoezi. Kasi ya kupungua uzito huwa kubwa Zaidi.
Wastani wa kupoteza uzito endapo utatumia dawa tu kwa mwaka ni kilo 6 kwa mtu mwenye kilo 90 na kilo 4.2 kwa mtu mwenye kilo 60. Ukichanganya na njia zingine kasi na uzito wa mwili hupungua zaidi.
Kiasi cha kupungua uzito kwa dawa kinaweza kuonekana kuwa ni cha chini sana, lakini kupungua huko husaidia kuimarisha shinikizo la damu na kukuondoa katika kihatarishi cha magonjwa yanayotokana na uzito kupita kiasi.
Maudhi ya dawa za hospitali za kupunguza uzito ni yapi?
Karibia kila dawa inaweza kuwa na madhara makubwa na madhara madogo ambayo yanaitwa maudhi, maudhi hayo yanayoweza kutokea huwa pamoja na;
-
Kichefuchefu
-
Choo kigumu
-
Kuharisha
Maudhi haya yanaweza kutokea kwa mda Fulani na kuisha jinsi mda unavyoenda, kwa hivyo ni muhimu sana kuwasiliana na daktari wako ili akuambie maudhi ya dawa anayokupa ili usije acha au kufikilia unashida Fulani mara maudhi yatakapokuwa yanatokea siku za mwanzo za kuanza kutumia dawa hizo
Utatumia dawa kwa muda gani?
Inategemea dawa uliyopewa na endapo utapata maudhi yatakayofanya ubadilishiwe dawa. Inategemewa kwamba mtu mwenye kilo 60 atapoteza wastani wa uzito wa kilo 3 kwa kutumia dawa kwa wiki 12 au miezi mi 3.
Endapo haufikii malengo hayo daktari anaweza kuona uhaja wa kukubadilishia dawa ili ziendane na malengo yako. Mara baada ya kuacha dawa baadhi ya watu hurudi kwenye uzito wao wa awali. Unaweza kusoma maelezo zaidi kuhusu kwanini watu wanarudia uzito wa awali kwenye sehemu ya tovuti hii mahari pameandikwa chakula na mazoezi. Ili kutorudia uzito wa awali ni vema endapo utazingatia kanuni mbalimbali za kiafya kama utakavyoelekezwa na daktari wako, chakula na mazoezi.
Dawa gani zinafaa kutumiwa kwa ajili ya kupoteza uzito?
Zipo dawa aina kadhaa ambazo zimekubaliwa na shirika la viwango vya vyakula na dawa duniani- FDA, dawa hizi zinaweza kuwa zile za asili kama bidhaa za BF suma au dawa zinazopatikana hospitali
Bidhaa za asili zilizothibitishwa zina uwezo mkubwa wa kupunguza uzito hadi wa kilo 5 kwa wiki endapo zitatumiwa kama inavyotakiwa.
Kupata tiba wasiliana na daktari wako au tumia namba zilizo chini ya tovuti hii kuanza tibia na daktari wa uly clinic, popote pale ulipo utafikishiwa dawa na utaelekezwa hatua kwa hatua mpaka ufikie kiwango cha uzito unaohitaji.
Matatizo mengine yanayopatiwa dawa za kuborehs maisha na tiba ni
-
Tatizo la Kutoona vyema na mtoto wa jicho (matatizo ya macho)
-
Maambukizi kwenye kitovu cha kichanga au kuzuia maambukizi
-
Homa yabisi
-
Maumivu ya maungio ya mwili
-
Maumivu ya meno
-
Kuondoa kitambi na uzito kupita kiasi
-
Na mengine mengi. Kujua zaidi wasiliana nasi
Siku zote wasiliana na daktari ili kupata matibabu bora ya ya uhakika. Unaweza kuwasiliana na madaktari wa uly clinic ili kupata matibabu ya haraka bila kupanga foleni. Ingia kwenye application ya uly clinic uanze kuomba tiba kutoka kwa daktari
Au tumia namba za simu chini ya tovuti hii ili kupata dawa za asili au zisizo za asili za tatizo lako. Kumbuka uly clinic inaongozwa na wataalamu wa afya wenye uzoefu na tiba tu, hivyo huna haja ya kuogopa kuomba ushauri toka kwao.
Toleo la 2
Imeboreshwa 15/1/2019
Dawa za asili zinazopatikana ni za kutibu, bonyeza kusoma au kupata tiba ;
Vimbe za fibroid kwenye kizazi
Ganzi na maumivu ya mikono na miguu
Kupunguza uzito na nyama uzembe