Kuigiza unakunywa, kutumia chombo tofauti cha kumnyweshea, kuchanganya na chakula au kubadilli njia ya kutoa dawa ni baadhi ya mbinu za kumfanya anywe dawa.
Maumivu ya tumbo kwenye ujauzito ni kawaida kutokea kwa wajawazito wengi na huisha bila matibabu, baadhi ya nyakati hata hivyo huashuria uwepo wa tatizo fulani la kiafya.
Kucheua kwa watoto ni hali ya kawaida inayotokea muda mfupi baada ya kunyonya. Hata hivyo wakati mwingine huashiria tatizo kubwa hususani ikiambatana na dalili nyingine kama kutokuongezeka uzito n.k.
Kutokwa na ute mweupe kwenye uume au uke unaoambatana na maumivu wakati wa kukojoa au hedhi katikati ya vipindi ni miongoni mwa dalili zinazoonekana siku ya 7 hadi 28 tangu kushiriki ngono zembe.
Dalili za gono inayosababishwa na Neisseria gonorrhea huonekana siku ya 2 hadi 21 tangu kushiriki ngono. Wanawake huchelewa onyesha dalili za awali na kupata athari zinazotokana na maambukizi.