Mwandishi:
Dkt. Sospeter B, MD
Mhariri:
Dkt. Peter A, MD
Jumamosi, 27 Novemba 2021
Ukweli kuhusu maziwa ya ng'ombe
Maziwa ya ng’ombe ni moja ya vinywaji vinavyotumika sana katika nchi mbalimbali za magharibi na kwa sasa kumekuwa na ongezeko la matumizi barani Afrika. Maziwa hawa huwa na kiasi kikubwa cha virutubishi 22 vilivyo muhimu sana kwa ajili ya ukuaji wa ndama.
Ukweli unaofahamika kwamba maziwa ya ng’ombe yana virutubishi vingi kwa ajili ya binadamu hautoshi kuchukuliwa kuwa wa afya. Hakuna mashaka kwenye ukweli wa kwamba maziwa ya ng’ombe yametengenezwa maalumu kwa ajili ya ndama na si binadamu au kichanga wa binadamu. Hii ndio sababu kwanini maziwa haya huwa na kiasi cha protini sawa na mara tatu na madini calcium sawa na mara nne ya kiwango kilicho kwenye maziwa ya mama anayenyonyesha.
Licha ya kuwa na virutubishi vingi, maziwa ya ng’ombe hayathibitishi kufaa sana kwa binadamu na hayapaswi kupendekezwa kuwa kinywaji kinacholeta afya kwa watoto na watu wazima pia.
Hasara za maziwa ya ngombe
Zifuatazo ni madhara ya kutumia maziwa ya ng'ombe;
Mfumo wa umeng'enyaji chakula wa watoto na watu wazima walio wengi hushindwa kumeng'enya maziwa na pia kushindwa kustahimiliwa kutokana na kuwa na laktosi kwa wingi.
Husababisha upungufu wa damu kwa watoto chini ya umri wa mwaka mmoja
Huwa na kemikali zinazosababisha mzio
Huwa na kiwango kidogo cha madini chuma na pia hupunguza ufyonzaji wa madini chuma mwilini kiasi cha kuweza kusababisha upungufu wa damu kwa mjamzito na watu wengine
Huongeza hatari ya kupata magonjwa ya mishipa ya damu kama kiharusi, mshituko wa moyo, angina.
Huongeza hatari ya magonjwa ya mfuko wa kizazi
Huongeza hatari ya saratani ya ovari na tezi dume
Huongeza hatari ya kupata ugonjwa wa mifupa dhaifu (osteoporosis)
Huongeza hatari ya uzee
Huongeza hatari ya kufa mapema.
Je maziwa ya ngo’mbe huongeza hatari ya kuvunjika kwa mifupa?
NDIO!
Utafiti kubwa umefanyika na kuonyesha kuwa kuvunjika kwa mifupa ni kawaida sana kwa watu wanaotumia maziwa ya ng’ombe kwa wingi kinyume na kile kilichosemwa tangu zamani kuwa hufanya mifupa kuwa imara. Mbali na kuvunjika mifupa, maziwa ya ng’ombe huongeza hatari ya magonjwa mishipa ya damu.
Ukweli kutoka kwenye tafiti
Madhara yaliyoelezewa kwenye Makala hii yametokana na tafiti kubwa iliyofanyika kuangalia athari za maziwa ya ng’ombe kwa binadamu na ilihusisha jumla ya watu 100,000 kwenye nchi mbalimbali duniani. Watu hawa walifuatiliwa kwa ukaribu kwa kipindi cha miaka 20(Karl Michaëlsson, et al)
Wapi unaweza pata taarifa zaidi?
Pata taarifa zaidi kuhusu maziwa ya ng'ombe kwenye linki za mada zifuatazo.
Maziwa ya ngombe na binadamu
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
20 Julai 2023 06:40:52
Rejea za mada hii:
1. Karl Michaëlsson, et al. Milk intake and risk of mortality and fractures in women and men: cohort studies. BMJ 2014; 349 doi: https://doi.org/10.1136/bmj.g6015. Iemchukuliwa 27.11.2021
2. Thorning, et al. “Milk and dairy products: good or bad for human health? An assessment of the totality of scientific evidence.” Food & nutrition research vol. 60 32527. 22 Nov. 2016, doi:10.3402/fnr.v60.32527