top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Jumatatu, 26 Julai 2021

Uoge maji baridi au moto baada ya mazoezi?

Uoge maji baridi au moto baada ya mazoezi?

Wakati wa mazoezi, mwili huzalisha jasho na kemikali ya laktiki asidi kwa wingi. Ili urejea mazoezi yajayo pasipo maumivu makali, unapaswa kuupoza mwili wako kwa kuoga maji sahihi na wakati sahihi. Je ni maji ya baridi au moto?


Kwanini ufahamu kuhusu ana ya maji ya kuoga baada ya mazoezi


Baada ya kufanya mazoezi, watu wengi hukimbilia kuoga ili kupooza mwili na kuondoa jasho. Aina ya maji na wakati unapotumia maji hayo huathiri mwili na ufanisi wa mazoezi yatayofuata. Ili kupungua athari hizo ni vema watu wakafahamu tabia njema na aina maji ya kutumia baada ya mazoezi.


Makala hii imelenga kukuelimisha namna sahihi ya kusimamisha mazoezi, maji gani ya kutumia, wakati gani wa kuoga na kwanini uoge maji sahihi.


Namna gani sahihi ya kusimamisha mazoezi


Kama unavyopasha mwili wakati wa kuanza mazoezi ili kuuandaa na mazoezi ya sasa, wakati unataka kukatisha mazoezi unapaswa kuuandaa mwili wako pia. Mfano kama unafanya mazoezi ya kukimbia, unapaswa kupuguza hatua unazokimbia taratibu na kufuatiwa na kutembea haraka haraka kisha taratibu kabla ya kupumzika.


Kufanya hivi kutafanya mwili upoe taratibu na mapigo ya moyo wako kupungua taratibu, hii ni tabia njema ya kiafya na hupunguza madhara ya mazoezi.


Maji gani ya kuoga baada ya mazoezi?


Baada ya kufanya mazoezi unapaswa pia kuchagua maji sahihi ya kuoga. Inafahamika kwenye tafiti nyingi kuwa misuli huzalisha kiwango kikubwa cha laktiki asidi, kumikali inayozalishwa na misuli wakati inajitengenezea nguvu. Kemikali hii ni chanzo kikuu cha maumivu ya misuli endapo itakusanyika kwa wingi kuzunguka misuli. Ili kuzuia laktiki asidi kukusanyika kwenye misuli, unapaswa kuikanda na kuchagua maji sahihi ya kuoga.


Kuoga maji sahihi kutafanya urejee siku za mbeleni kwenye mazoezi bila kuwa na maumivu makali

Baada ya mazoezi makali na kutumia mbiu sahihi za kusimamsha mazoezi kama ilivyotolewa mfano wa mazoezi ya kukimbia hapo juu, tafiti nyingi zinaonyesha kuoga maji ya baridi au barafu baada ya mazoezi husaidia kuimairisha misuli, kuipoza haraka na kupunguza maumivu wakati wa mazoezi yanayofuata.


Tafiti zingine zinaonyesha kuwa, kuoga maji ya baridi baada ya mazoezi hupunguza mapigo na msongo wa kweney moyo kwa wanaoishi kwenye maeneo ya joto.


Namna ya kupoza mwili kwa maji baada ya mazoezi


 • Unapohitaji kupumzika wakati wa mazoezi makali, anza kwanza na mazoezi ya kutumia nguvu kidogo, mfano kama unafanya mazoezi ya kukimbia, anza kukimbia taratibu kisha kutembea mpaka kusimama. Tumia muda wa dakika 5 hadi 10 kwa mazoezi ya nguvu kidogo

 • Baada ya kusimama, anza mazoezi ya kunyoosha misuli, hii itasaidia kuondoa laktiki asidi kwenye misuli na kuzuia maumviu ya misuli kutokana na mazoezi

 • Anza kuoga maji ya uvuguvugu ili usiushitue mwili wako kwa kuupoza haraka. Joto la mwili linaloshuka kwa maji ya uvuguvugu, malizia kulishusha kwa maji ya baridi. Au kama umepumzika kwa muda zaidi wa nusu saa kutoka kwenye mazoezi na mwili umepoa, oga moja kwa moja maji ya baridi

 • Tumia sabuni kusafisha ngozi ili kuondoa jasho na uchafu unaoziba vinyweleo vya ngozi

 • Unapobakisha sekunde chache kabla ya kumaliza kuoga, tumia maji ya baridi zaidi au barafu kupooza mwili na misuli iliyohusika kwenye mazoezi ili kuipa nguvu misuli iliyochoka


Jikaushe kwa taulo kisha vaa nguo safi na kupumzika au kuendelea na shughuli zingine.


Faida za kuoga baada ya mazoezi na mambo ya kuepuka


 • Faida za kuoga baada ya mazoezi ;

 • Hupunguza msongo kwenye misuli na kuharakisha mwili kurejea kwenye hali yake ya kawaida

 • Huzuia magonjwa ya ngozi

 • Huzibua vitundi vya ngozi na hivyo kukukinga na chunusi pamoja na maambukizi kwenye ngozi

 • Huongeza kinga ya mwili Mambo ambayo hutakiwi kufanya baada ya mazoezi makali

 • Hutakiwi kuoga maji ya baridi punde tu baada ya mazoezi makali. Kufanya hivi utaepusha moyo kwenda mbio na kukakamaa kwa misuli.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

7 Oktoba 2021 04:59:14

Rejea za mada hii:

1. Versey. NG, et al. Water immersion recovery for athletes: Effect on exercise performance and practical recommendation. DOI:. Https://doi.org/10.1007/s40279-013-0063-8. Imechukuliwa 26.07.2021

2. Tan. PMS, et al. Evaluation of various cooling systems after exercise-induced hyperthermia. DOI: https://doi.org/10.4085/1062-6050-52.1.11. Imechukuliwa 26.07.2021

3. Roberts. LA, et al. Post-exercise cold water immersion attenuates acute anabolic signaling and long-term adaptations in muscle to strength training. DOI: https://dx.doi.org/10.1113/JP270570. Imechukuliwa 26.07.2021

4. Mayo Clinic. Aerobic exercise: How to warm up and cool down. Mayoclinic.org/healthy-lifestyle/fitness/in-depth/exercise/art-20045517. Imechukuliwa 26.07.2021

5. Butts. CL, et al. Physiologic and perceptual responses to cold-shower cooling after exercise-induced hyperthermia. DOI:. Https://dx.doi.org/10.4085/1062-6050-51.4.01. Imechukuliwa 26.07.2021

6. Buijze. GA, et al. The effect of cold showering on health and work: A randomized controlled trial. DOI:. Https://dx.doi.org/10.1371/journal.pone.0161749. Imechukuliwa 26.07.2021

7. Allan. R, et al. Is the ice bath finally melting? Cold water immersion is no greater than active recovery upon local and systemic inflammatory cellular stress in humans. DOI:. Https://dx.doi.org/10.1113/JP273796. Imechukuliwa 26.07.2021

8. Ajjimaporn. A, et al. Effect of cold shower on recovery from high-intensity cycling in the heat.
Pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/31343603/. Imechukuliwa 26.07.2021

bottom of page