Mwandishi;
Dkt. Mercy M, CO
Mhariri;
Dkt. Sospeter B, MD
5 Oktoba 2021 17:19:59
Human parvovirus B19
Kirusi Human parvovirus ni kirusi kinachosababisha ugonjwawa fifth unaoonekana kwa homa na kubadilika kwa ngozi mithiri ya mtu aliyepigwa kofi kwenye shavu.
Kirusi ugonjwa gani?
Kirusi hiki husababisha ugonjwa wa ngozi hasa kwa watoto unaojulikana kama erythema infectiosum.
Kirusi kiliguduliwa mwaka gani?
Kirusi human parvovirus B19 uligundulika kwa mara ya kwanza mwaka 1975.
Kirusi Human parvovirus B19 kipo katika Familia gani?
Kirusi Human parvovirus B19 ni kimoja wapo kwenye genus ya Erythrovirus na familia ya Parvoviridae. Virusi katika familia hii hufahamika kwa kuwa na strendi moja ya DNA pia husababisha ugonjwa wa ngozi.
Sifa za kirusi
Human parvovirus B19 ni kirusi chenye strendi moja ya DNA katika familia ya virusi vya Parvoviridae na huwa na sifa zifuatazo;
Strendi moja ya DNA
Kipenyo cha 23-28nm
Wana umbile lenye pande ishirini
Ukuta wa seli yake umefugwa
Kirusi hutunzwa na nani?
Kirusi Human parvovirus B19 hutunzwa na binadamu.
Kirusi Human parvovirus B19 kinaenezwa kwa njia gani?
Kirusi Human parvovirus B19 kinaenezwa kwa njia zifuatazo;
Ugonjwa huu unaweza kusambaa kutoka mtu mmoja kwenda mtu mwingine kupitia kugusana na matone ya mtu mwenye maambukizi anapopiga chafya, anapokohoa au anapopumua.
Wakati mwingine watu huambukizwa wanapogusa vitu au sehemu yenye virusi na kujigusa puani au mdomoni.
Kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Vihatarishi vya kupata maambukizi ya kirusi Human parvovirus B19
Watoto wadogo
Wajawazito
Mtu yeyote anayekaa karibu na mtu mwenye maambukizi
Dalili za maambukizi ya kirusi Human parvovirus B19
Muda wa kuatema huwa ndani ya siku 4 hadi 14. Mtu mwenye maambukizi ya kirusi human parvovirus B19 huweza kumuambukiza mwingine hata kabla dalili hazijaonekana. Dalili za maambukizi ya kirusi human parvovirus B19 ni;
Vipele
Homa
Maumivu ya kichwa
Maumivu ya viungo
Mafua
Mwili kudhoofika
Kichefuchefu
Viashiria
Kupanda kwa joto la mwili
Vipele mithiri ya mabaka au vilivyoinuka kiasi
Wekundu kwenye ngozi mithiri ya mtu aliyepigwa kofi la mkono
Kupanda kwa vimeng’enya vya ini
Vipimo vya kirusi Human parvovirus B19;
Picha nzima ya damu
Kuotesha kirusi
C-reactive protini
Polymerase chain reaction
Serolojia ya parvovirus
Serum protein electrophoresis
Magonjwa yanayoweza kufanana dalili na kirusi Human parvovirus B19 ni pamoja na;
Pediatric Rubella
Matibabu ya maambukizi ya kirusi Human parvovirus B19
Mgonjwa atapatiwa dawa kwa ajiri ya homa na maumivu
Mgonjwa dawa aina ya antihistamine kwaajiri ya kuzuia aleji
Mgonjwa atapatiwa sindano ya immunoglobulin
Hakuna dawa maalum kwaajiri ya kirusi human parvovirus B19
Je kuna chanjo ya kirusi Human parvovirus B19?
Mpaka sasa hakuna chanjo ya kirusi human parvovirus B19.
Fanya yafuatayo ili uweze kuwakinga wengine endapo umepata maambukizi
Ukiwa umeugua, usitoke nyumbani, isipokuwa pale unapohitaji huduma ya matibabu
Funika mdomo na pua kwa kitambaa wakati unapokohoa au kupiga chafya au fanya hivyo ndani ya kiwiko chako na ukioshe baadaye
Tupa kifaa kilichotumika kwenye takataka
Nawa mikono yako mara kwa mara kwa maji safi na sabuni
Usiguse macho yako, pua na mdomo
Usikae karibu na mtu mwenye maambukizi
Imeboreshwa;
5 Oktoba 2021 17:19:59