Afya ya uzazi na uzazi
​
Ni Mambo mengi ambayo mwanamke na mama mjamzito anapaswa kuyafahamu akiwa mjamzito au akiwa anataka kuwa mjamzito ili kuchukua hatua za msingi kuhakikisha anakuwa na ujauzito bora na kupata mtoto mwenye afya njema. Katika sehemu hii utakutana na mambo kama hatua za kuchukua kabla ya kuwa mjamzito, mambo ya kuzingatia ukiwa mjamzito, vyakula vya kula ukiwa mjamzito na dalili aina na hatua za uchungu
Uzazi wa mpango ni hali ya kupanga ni wakati gani, idani gani na kwa miaka mingapi watoto wako watofautiane umri. Zipo njia kadha za uzazi wa mpango ambazo hutumika ikitegemea uchaguzi wa mtu ama ujuzi ama uzoefu wa awali wa matumizi ya dawa njia hizi.
Wakati wa ujauzito, afya ya mtoto wako ni ya kwanza kuzingatia ndio maana matatizo ya ujauzito yanaweza kuwa ya kuogopesha kwa sababu usipokuwa makini unaweza kupoteza ujauzito ama kujifungua mtoto mwenye matatizo, Afya ya mama pia ni muhimu kuzingatiwa ili mtoto aweze kukua vizuri tumboni
Kipindi baada ya ujauzito kuna baadhi ya mambo mama anatakiwa kuyafanya ili kuhakikisha kuwa anaendelea kuwa na afya njema yeye na mtoto wake
Sehemu hii inazungumzia elimu kwa ujumla kwa wasichana na kinamama ambao hawana au wana watoto.