Ingawa kikohozi kikavu ni dalili mojawapo ya maambukizi ya HIV, hutakiwi kuhofu sana endapo una dalili hii.
Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha kikohozi kikavu kama vile;
kucheua tindikali, ugonjwa wa sinazi, maambukizi ya chlamydia au mwitikio wa mwili kwenye hewa ya baridi na sababu zingine.
Jambo la msingi utatakiwa kufanya ni kuonana na daktari wako endapo kikohozi kitaendelea kwa muda mrefu kwa uchunguzi.
Ndio! Maambukizi ya VVU au UKIMWI unaweza kusababisha kikohozi kikavu. Hii ni kwa sababu VVU hupunguza uwezo wa mwili kupambana na maambukizi na magonjwa mengine ambayo huathiri mfumo wa hewa na kuleta dalili ya kikohozi kikavu.
Kusoma zaidi kuhusu dalili za ukimwi bofya linki inayofuata
https://www.ulyclinic.com/foramu/majadiliano-na-wataalamu/dalili-za-ukimwi-ni-zipi
au
https://www.ulyclinic.com/ukimwi
Dalili za ukimwi zinaweza kutofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine, vivyo hivi kutokea na kupotea kwa kikohozi kikavu hutegemea kinga ya mwili ya mtu dhidi ya maradi, hivyo huweza kudumu kwa muda wa wiki chache hadi miezi kadhaa na kwa baadhi ya watu kikohozi huwa hakiishi haswa endapo mgonjwa yupo kwenye hatua za mwisho za maambukizi ya VVU/UKIMWI.
Ndio!
Endapo kinga ya mwili ni dhaifu kutokana na maambukizi ya VVU, na kutotumia dawa, mwili hushambuliwa na magonjwa mbalimbali ya mfumo wa upumuaji. Anayeishi na maambukizi ya VVU anaweza kupata magonjwa ya mfumo wa hewa kama Nimonia n.k ambayo hupelekea dalili za kikohozi kibichi n.k
Soma majibu zaidi kwenye makala ya dalili za ukimwi kwenye mfumo wa hewa.
Kama itashindikana kutoshiriki ngono wakati unatumia PEP, unashauriwa kutumia kondomu ili kumkinga mwenza wako dhidi ya maambukizi ya VVU.
Mambo mengine unayoshauriwa kuepuka ni kushiriki vifaa au sindano ya kudunga dawa za kulevya.
Maelezo zaidi unaweza kupata kwa mtaalamu wa afya katika kituo cha afya karibu nawe au kuwasiliana na daktari wa ULY CLINIC kupitia mawasiliano chini ya tovuti.
Virusi vya UKIMWI huathiri kinywa na ulimi hivyo kuleta dalili mbalimbali ambazo kwa baadhi ya watu huwa ni dalili ya awali.
Dalili za UKIMWI kwenye ulimi ni pamoja na;
Utando mweupe kwenye ulimi mithiri ya uji au pamba au kama maziwa mazito- hii ni kutokana na kuzaliana kwa kasi kwa fangasi wanaoishi ndani ya kinywa. utando huweza kuonekana pia kwenye kwenye kona, sakafu na paa la kinywa na huleta hisia za kuwa na pamba kinywani na kupotea kwa ladha. Endapo utando utakwanguliwa huwa unatoka.
Mabaka meupe kwenye mikunjo na kingo za ulimi. Mabaka hayo yanaweza kujitenga mithiri ya nywele nyeupe, hata hivyo huweza tokea eneo lolote lile la ulimi. Kutokea kwake hakuambatani na dalili ya maumivu na huwa hayatoki hata yakikwanguliwa. Kisababishi huwa ni kuamka kwa maambukizi ya kisuri cha Epistein Bar (EBV).
Vidonda homa mdomoni kutokana na maambukizi ya virusi vya Hepes simplexx 1 na 2. Ingawa vidonda hipi huonekana sana kwenye midomo, pia huweza kutokea kwenye ulimi na ndani ya kuta za kinywa kwa wagonjwa wa UKIMWI.
Mabaka meusi kwenye ulimi. Mabaka haya hufanyika sana kwa watu wenye asili ya afrika, ingawa hutokea sana kwenye kuta za kinywa, mabaka haya pia huweza kuonekana kwenye ulimi. Ulimi huonekana kuwa na mabaka ya kahawia kuelekea nyeusi au meusi, inaweza kuwa baka moja au mengi. Hii inaweza kusababishwa na Virusi vya UKIMWI au dawa zinazotumika kupambana na maambukizi ya VVU
Kuota kwa Chunjua, hii husababishwa na maambukizi ya human papillomavirus (HPV) ambacho huambukizwa kwa njia ya kujamiana au kubusiana. Chunjua huweza kuwa na mwonekano wa rangi nyeupe au pinki isiyokolea au kijivu na huweza kuwa na mwonekano pia kama wa ua lililochanua
Virusi vya UKIMWI vinaweza kuishi muda wa saa 1 hadi siku 42 ikitegemea mambo yafuatayo wingi wa virusi, wingi wa damu, joto, unyevu kwenye hewa na mwanga wa jua.
Muda wa virusi vya UKIMWI kuishi kwenye sindano ya tundu
Virusi vinaweza kuishi muda mrefu zaidi kwenye sindano ya kuchomea dawa endapo joto na hali ya hewa havibadiliki badiliko. Mfano endapo sindano imewekwa kwenye jokofu, virusi vilivyo kwenye sindano vinaweza kuishi hadi siku 42
Endapo sindano hii ipo kwenye joto la mazingira, virusi vya UKIMWI vinaweza kuishi muda wa siku 7.
Muda wa virusi vya UKIMWI kuishi Kwenye manii/shahawa
Mara baada ya mbegu za kiume kutoka nje ya mwili, huanza kufa mara moja kutokana na kupigwa na hewa pamoja na joto la mazingira. Hivyo inachukua saa1 hadi 2 kuwa havina uwezo wa kuambukiza endapo mbegu hizo zimekauka kabisa.
Muda wa virusi vya UKIMWI kuishi Kwenye damu iliyokwenye mazingira
Asilimia 90 hadi 99 ya virusi hufa ndani ya masaa kadhaa baada ya damu au majimaji kupigwa na hewa, mwanga wa jua na kukauka katika joto la mazingira.
Muda wa virusi vya UKIMWI kuishi Kwenye maji
Virusi vya UKIMWI endapo vitawekwa kwenye maji huchukua muda wa masaa nane kupoteza uwezo wake wa kuambukiza (hufa). Hata hivyo ndani ya masaa 2 kwenye maji, ni asilimia 10 tu ya virusi vinawez akuishi na muda unavyoongezeka, idadi a virusi huwa 0 baada ya masaa 8.
Kipimo cha
kwenye vituo vya kutolea huduma za afya za serikali ni bure, hata katika baadhi ya hospitali binafsi zinazopokea masaada wa vipimo.
Kwenye hospitali za kulipia huduma, bei ya kipimo hiki inaweza kuwa kati ya shilingi elfu 1 hadi 10.
Kwa sasa hakuna tekinolojia yenye uwezo wa kupima UKIMWI kwa kutumia simu. Vipimo vya UKIMWI ni vya kutumia damu, mate pamoja na kitambuzi cha UKIMWI kama SD bioline, Unigold n.k
Hata hivyo unaweza kutumia huduma za ULY CLINIC au zingine kupata majibu ya KIPIMO kwenye simu endapo utakuwa umeacha sampuli ( umechukuliwa sampuli) na huna muda wa kuubiria majibu.
Jinsi ya kupima UKIMWI kwa kutumia mate;
Chukua kichukua sampuli ya mate kisha pitisha kwenye fizi za juu na chini mara moja ili kukusanya sampuli kisha
Weka sampuli yako kwenye kipimo, sehemu ya kuweka sampuli
Endapo sampuli ni ya kutosha, haina haja ya kuweka bafa ( endapo sampuli ni kidogo weka matone 2 ya bafa
Subiri sampuli itembee kwenye kipimo
Soma majibu ya kipimo ndani ya dakika 15
Tafiti zinaonyesha, matumizi ya mate inaweza kuwa njia mbadala ya kutumia damu. Majibu ya kipimo cha UKIMWI kwenye mate inaweza kugundua kwa asilimia 99.
Endapo una kipimo maalumu cha kutumia mate, pitisha kichukua sampuli mara moja kweney fizi za juu, kisha fizi za chini na kisha kiunganishe kwenye kipimo chako na soma majibu ndani ya dakika 20.
Kumbuka: Kupima UKIMWI Kwa kutumia mate inahitaji uwe na kipimo ambacho kimetengenezwa kupima uwepo antibodies za VVU kwenye mate, endapo utatumia kipimo kisicho sahihi unatoa uwezekano wa kupata majibu yasiyo sahihi.
Mistari mitatu kwenye kipimo cha UKIMWI humaanisha kuwa una maambukizi ya kirusi cha UKIMWI namba 1 na 2
Kuna aina mbili za Virusi vya UKIMWI,
Kirusi cha UKIMWI 1
Hupatikana duniani kote
Huongoza maambukizi kwa binadamu
Maambukizi huelekea ugonjwa wa UKIMWI haraka zaidi
Kirusi cha UKIMWI 2
Ni nadra sana kuambukizwa kwa binadamu
Maambukizi huchelewa kuelekea kwenye ugonjwa wa UKIMWI
Hupatikana sana afrika magh'aribi.
Hivyo endapo mistari mitatu itaonekana kwenye kipimo cha SD bioline, hii inamaanisha una maambukizi ya Virusi vyote viwili.
Vipimo vya UKIMWI vinapatikana kwenye vituo vyote vya kutolea huduma ya afya na Kituo cha ushauri nasaha (CTC), hata hivyo unaweza kupata vipimo hivi kwa kununua kwenye baadhi ya maduka ya dawa moto (pharmacy).
Endapo unahitaji kupima maambukizi ya VVU, fika kituo cha ushauri nasaha au kituo cha afya karibu nawe kwa kupima bure.
Kuna aina mbili za Virusi vya UKIMWI, Kirusi cha UKIMWI 1 na Kirusi cha UKIMWI 2
Kirusi cha UKIMWI 1
Hupatikana duniani kote
Huongoza maambukizi kwa binadamu
Maambukizi huelekea ugonjwa wa UKIMWI haraka zaidi
Kirusi cha UKIMWI 2
Ni nadra sana kuambukizwa kwa binadamu
Maambukizi huchelewa kuelekea kwenye ugonjwa wa UKIMWI
Hupatikana sana afrika magh'aribi.
Soma zaidi kuhusu virusi vya UKIMWI kwa kubofya hapa