top of page

Vidokezo vya Afya

Acha kuvuta sigara

Acha kuvuta sigara

Sigara ni moja ya vyanzo vya magonjwa ya moyo. Mwaka mmoja ukiacha sigara utapunguza kwa nusu hatari ya shambulio la moyo kuliko mvutaji.

Acha mazoea ya kula chakula taka

Acha mazoea ya kula chakula taka

Chakula taka, ni aina ya chakula kisicho na thamani kubwa mwilini mwako. Sifa yake kubwa ni kuwa na nishati kwa wingi zinazotokana na mafuta au sukari, huku kikikosa au kuwa na kiwango kidogo sana cha protini, vitamin, madini, nyuzinyuzi na virutubisho vingine muhimu kwa mwili wako. Acha uteja wa kula chakula taka, kula vyakula vinavyoshauriwa kiafya.

Acha mazoea ya kutumia dawa za maumivu jamii ya NSAIDS

Acha mazoea ya kutumia dawa za maumivu jamii ya NSAIDS

Asilimia 15 ya watumiaji wa dawa za kupunguza maumivu jamii ya NSAIDS kama Ibuprofen, Indomethacin, aspirin, naproxen n.k, wana hatari ya kupata vidonda vya tumbo vinavyopelekea kutapika damu. Tumia njia mbadala au tumia dawa za maumivu inapolazimika.

Aflatoksin

Aflatoksin

Aflatoksin ni aina ya sumu inayosababisha saratani ya ini, mwili huathiriwa na sumu kwa kuvuta hewa au kula mazao yaliyoathiriwa na fangasi. Jikinge kwa kutambua na kula mazao ya shamba ambayo hayajaathiriwa.

Aina ya vipele vya UKIMWI

Aina ya vipele vya UKIMWI

Vipele vya UKIMWI husababishwa na maambukizi ya VVU, maudhi ya dawa za UKIMWI, magonjwa nyemelezi ya UKIMWI sambamba na saratani zinazoambatana na UKIMWI.

bottom of page