top of page

Sera ya Matangazo na udhamin

 

Kuwezesha kazi zetu za kuelimisha jamii kwa elimu bora na inayotakiwa, tunakubali matangazo na udhamini kwa vigezo vikali tulivyoweka.

 

Tunakataa matangazo yote tunayoamini kwamba yanaleta udanganyifu ama hayaendani na yale tunayooamini ni sahihi kwenye afya ya mtu na jamii kwa ujumla. Kuwepo kwa tangazo katika website yetu au katika moja ya barua pepe haimaanishi tumetoa rehani kuhusu usalama wa tangazo hilo na kampuni.

 

Kampuni linalotangaza na wadhamini hawatakiwi kuwahakikishia watumiaji kuwa  ULY-Clinic imethibitisha tangazo hilo ama bidhaa wanazotangaza, kwa kufanya hivyo unapingana na sera zetu.

 

Tangazo linaweza kuwekwa kwenye ujumbe unaoendana na mada inayozungumzwa kwenye website yetu. ULY-Clinic imetenga matangazo na habari muhimu za elimu kwa kuonyesha kama ni tangazo ama ni wadhamini ili watazamaji wasome na kuelewa, matangazo na wadhamini wamewekwa kwenye sehemu maalumu mbali na mada ili kuondoa upotovu kwamba matangazo hayo ni sehemu ya bidhaa za ULY-Clinic.

                                           

bottom of page