top of page

Huduma ya kwanza majeruhi wa ajali za vyombo vya moto

​

Janga ambalo unaweza kukutana nalo sana katika maisha yako ni ajali ya vyombo vya moto ikiwa pamoja na pikipiki na gari. Ingawa dhumuni lako la awali litakuwa kumsaidia majeruhi, ni vema ukachukua tahadhari wa usalama wako na wale wanaokusaidia kwanza kabla ya kuingia kwenye tukio.

 

Endapo umeshuhudia ajali imetokea na upo kwenye gari yako kama mpitanjia, hakikisha unapaki gari lako sehemu salama na usifunge njia kwa ajili ya watalamu wa huduma za dharura kuweka kufika na kumbeba majeruhi. Washa taa ya hazardi na kuweka triangle kwenye barabara kuonyesha tahadhari kwa magari yanayokuja pande zote kisha endapo una nguo za kuakisi mwanga kama zile za polisi au watengeneza barabara, zifae ili uonekane kirahisi kwa mbali.

 

  • Endapo majeruhi amenaswa ndani ya gari, mtoe kwenye sehemu hiyo haraka endapo ni salama kabla moto haujalipuka,

  • Chukua tahadhari ili kutoleta majeraha Zaidi kwenye shingo na mgongoni kwa sababu unaweza kusababisha mgonjwa kupoteza mawasiliano ya mfumo wa fahamu au kifo cha ghafla.

  • Mweke majeruhi katika pozi lililotulia kichwa na mgondo usitikisike ili kuzuia majeraha ya shingo na uti wa mgongo

  • Wakati wa kumnasua majeruhi hakikisha mazingira ni salama kwamba hutelezi au kukatwa kwa kushikwe vioo vilivyovunjika kwenye eneo la tukio wakati wa kumtoa majeruhi aliyenaswa.

 

Endapo airbag haijapasuka bado wakati wa ajali, hakikisha hukai usawa wa sehemu inapotoka ili kuzuia kupata majeraha kutokana na kupasuka kwake.

bottom of page