top of page
Bei ya Ceftriaxone

Bei ya Ceftriaxone

Ceftriaxone ni antibiotiki ya kundi la cephalosporins (kizazi cha tatu) inayotumika kutibu maambukizi makali ya bakteria kama ya mapafu (nimonia kali), homa ya uti wa mgongo (meningitis), kusamba kwa sumu ya bakteria kwenye damu (sepsis), njia ya mkojo, tumbo, na magonjwa ya zinaa kama kisonono (gono). Hutumika zaidi hospitalini kwa wagonjwa waliolazwa.


Fomu za kawaida za Ceftriaxone


Ceftriaxone ya sindano (Injection 250mg, 500mg, 1g)

Hutumika kwa watu wazima na watoto. Dozi ya kawaida: mara 1 kwa siku (au kulingana na ugonjwa)


Bei:

  • MSD / Bohari ya Dawa: TZS 800–1,500 kwa dozi

  • Hospitali / famasi binafsi: TZS 2,000–5,000 kwa dozi (bila gharama ya huduma)


Kumbuka Muhimu

  • Ceftriaxone si dawa ya fangasi, ni ya bakteria pekee

  • Hutolewa kwa sindano tu (IM au IV) chini ya uangalizi wa mtaalamu

  • Tumia kwa uangalifu kwa wagonjwa wenye aleji ya cephalosporins au penicillin

  • Haitakiwi kuchanganywa na calcium IV kwa watoto wachanga

  • Haitakiwi kutumiwa bila ushauri wa mtaalamu wa afya

  • Matumizi mabaya ya antibiotiki huchangia usugu wa dawa

Imehuishwa:

11 Januari 2026, 06:15:33

bottom of page