top of page

Imeandikwa na ULY CLINIC

 

Maumivu sugu ya kibofu na kukojoa mara kwa mara

​

Utangulizi

​

 

Makala hii imezungumzia kuhusu maumivu sugu ya kibofu cha mkojo na viungo ndani ya nyonga yanayoambatana na kukojoa mara kwa mara na yenye kusababishwa na tatizo lenye jina la kitiba Interstitial cystitis.

​

 

Interstitial cystitis ni nini?

​

​

Ni ugonjwa sugu unaosababisha kuhisi maumivu na mgandamizo kwenye kibofu cha mkojo na wakati mwingine maumivu ndani nyonga. Maumivu huweza kuwa kwa kiasi na wakati mwingine kuwa makali sana. Ugonjwa huu huathiri wanawake kwa asilimia 90 na tatizo ni kubwa sana kwa watu weupe.

 

​

Kibofu cha mkono ni kifuko ambacho kilichotengenezwa kwa misuli laini na hufanya kazi ya kutunza na kusukuma nje mkojo. Misuli hii laini hutanuka kwa jinsi mkojo unavyoingia kujaza kibofu kutoka kwenye figo. Kibofu kinapokuwa kinatanuka, kikifikia kujaa, mishipa ya fahamu iliyo kwenye misuli hii hutoa taarifa zinazosafiri kwenda kwenye mfumo wa kati wa fahamu ili kukiambia kibofu kifunguke na kutoa mkojo nje.

​

 

Endapo una tatitzo la IS, mfumo wa utoaji wa taarifa za kukojoa huwa zimejichanganya na mtu anakuwa na hamu ya kwenda kukojoa mara kwa mara na hukojoa kiwango kidogo tu cha mkono.

​

 

Dalili za interstitial cystitis

​

​

Dalili za ugonjwa kwa mwanzoni huwa hazionekani kabisa, hata hivyo kwa jinsi kuta za kibofu zinazoendelea kuharibika, dalili za ugonjwa huonekana na ukali wake hutegemea mtu. Dalili hizo ni;

​

  • Kuhisi mgandamizo juu ya maeneo ya kibofu, sehemu ya chini katikati ya kitovu.

  • Maumivu ya kwenye nyonga kati ya uke na njia ya haja kubwa kwa wanawake

  • Maumivu kati yakorodani na njia ya haja kubwa kwa wanaume

  • Maumivu sugu ndani ya nyonga

  • Kutoisha kwa hamu ya kwenda kukojoa

  • Kukojoa mara kwa mara na kukojoa kiasi kidogo sana cha mkojo inaweza kuwa zaidi ya mara 50 kwa siku kwa baadhi ya siku

  • Maumivu wakati kibofu kimejaa mkojo yanayopoa wakati umemaliza kukojoa

  • Maumivu wakati wa kujamiana

  • Maumivu kuongezeka wakati wa kuwa na msongo wa mawazo

  • Baadhi ya watu hupata maumivu makali sana wakati wa ovuleshen, hedhi au kwenye msimu wa aleji

 

Kumbuka: Dalili za ugonjwa huu huweza kufanana na dalili za ugonjwa wa UTI sugu, hata hivyo mgonjwa wa IS huwa hana maambukizi endapo atafanya kipimo. Endapo maambukizi ya UTI yatatokea kwa mgonjwa wa IS, dalili huwa kali Zaidi.

 

 

Wakati gani wa kumwona daktari kwa matibabu;

​

 

Mwone daktari kwa uchunguzi na tiba endapo

 

  • Unapata maumivu wakati wa kukojoa

  • Unakojoa mara kwa mara

  • Unamaumivu sugu ya kibofu

​

​

Visababishi

​

 

Kisababishi halisi cha ugonjwa huu hakifahamiki, hata hivyo sababu halisi ya kipathologia ni kwamba, ukuta wa juu ndani ya kibofu unaoitwa urothelial huwa umeharibiwa na hivyo kupelekea kupenya na kuingia kwa madini ya potassium na sumu zingine kwenye misuli ya kibofu. Kupenya kwa madini na kemikali zingine huamsha mishipa ya fahamu na kusababisha uharibifu kwenye misuli ya kuta za kibofu.

 

  • Udhaifu katika ukuta wa ndani ya kibofu zinazosababisha mkojo kuingia kwenye kuta za chini na kuleta maumivu

 

Visababishi vingine ambavyo havijathibitishwa bado ni;

  • Magonjwa ya autoimmune

  • Magonjwa ya kurithi

  • Maambukizi kwenye kibofu

  • Mzio (aleji kwenye kibofu)

 

​

Vihatarishi

 

​

Vihatarishi vifuatavyo vinaweza kupelekea kupata tatizo la IS ambavyo ni;

  • Kuwa na jinsia ya kike ni kihatarishi cha kupata tatizo hili kuliko kuwa mwanaume. Dalili za tatizo hili kwa wanaume zinaweza kuwa zimesababishwa na ugonjwa wa Prostatitis

  • Kuwa na rangi nyekundu ya nwele

  • Kuwa na umri wa miaka 30 au Zaidi

  • Kuwa na maumivu mengine sugu kama ya ugonjwa wa maumivu ya misuli n.k

 

​

Uchunguzi

​

​

Uchunguzi wa tatizo hili hufanyika kwa kuanza na kuulizwa maswali mbalimbali kuhusu historia ya tatizo na kisha kufanyiwa uchunguzi wa awali wa kuangalia na kushika mwili wako ikihusisha mwili mzima bila kusahau eneo ambalo lenye shida. Baada ya kuulizwa taarifa na kuona dalili au ishara Fulani, daktari anaweza kushauri ufanyiwe vipimo kati ya vifuatavyo;

 

  • Kipimo cha biopsy- kipimo hiki hutumia sampuli iliyochukuliwa wakati unafanyiwa cystoscopy. Kinyama hupimwa kuangalia endapo kunamabadiliko yoyote kwenye asili ya kuta za kibofu cha mkojo yanayopelekea wewe kupata dalili hizo.

  • Kipimo cha kuangalia ndani ya kibofu cha mkojo chenye jina la cystoscopy. Kamera ndogo itapitishwa kwenye mrija wa mkojo ili kuangalia ni hali ya kuta za kibofu na kuchukua sampuli kutoka kwenye kuta hizo.

  • Kipimo cha mkojo- utachukuliwa mkojo kwa ajili ya kwenda kuangalia kama una maambukizi ya UTI

  • Kipimo cha mwitikio wa kibofu kwenye potassium

  • Kipimo cha urine cytology- mkojo utachukuliwa ili kuangalia chembe zilizopo kwenye mkojo, kinaweza kutofautisha endapao una saratani au la.

 

​

Matibabu

 

​

Matibabu ya tatizo hili si rahisi, Hakuna dawa inayofahamika kitaalamu ambayo inaweza kupelekea kuondoa tatizo hili na matibabu pia hutofautiana mtu na mtu. Unatakiwa kujaribu aina tofauti za matibabu ili kuona ni matibabu yapi ni msaada sana kwako.

 

Matibau ya kifiziko

 

​

​

Shirikiana na mtaalamu wa mazoezi ili kuweza kupata msaada, matibabu ya kifiziko huweza kuondoa maumivu ya misuli, kulainisha tishu zilizokauka na madhaifu ya ndnai ya nyonga na hivyo kupunguza maumivu.

 

​

​

Matumizi ya dawa za kunywa

 

  • Dawa za kutuliza m aumivu jamii ya NSAIDs kama vile ibuprofen au naproxen sodium

  • Dawa za kulainisha misuli ya kibofu jamii ya Tricyclic antidepressants kama amitriptyline au imipramine

  • Dawa za kupunguza hamu ya kukojoa mara kwa jamii ya antihistamine kama vile loratadine

  • Dawa za kurejesha asili ya ukuta wa ndani ya kibofu kama vile Pentosan polysulfate sodium (Elmiron)

 

​

Tiba ya kuamsha mishipa ya fahamu

 

Huweza kusaidia kufanya misuli ya kibofu iamke na kuongeza mzunguko wa damu. Hii hupelekea kupunguza maumivu. Tiba hii hutumia umeme kuamsha misuli ya kibofu au mfumo wa fahamu kwenye ngonga

 

​

Tiba ya kutanua kibofu

 

Wakati unafanyiwa kipimo cha cystoscopy maji maalumu huwekwa kwenye kibofu ili kukitanua kwa kukijaza. Baadhi ya watu baada ya kipimo hiki hupata unafuu, endapo unafuu unadumu kwa muda mrefu, inaweza kuhitajika ukafanyiwa tiba hii kwa wakati kadhaa.

 

​

Tiba ya kuweka dawa ndani ya kibofu

 

Dawa maalumu yenye kifupi cha DMSO huwekwa kwenye kibofu kupitia mirija wa urethra na kuachwa ikae kwamuda wa dakika 15 kabla ya kuambiwa uikojoe.  Dawa hii huchanganywa na ganzi ili kusaidia kuondoa maumivu. Utatumia dawa hii kwa muda wa wiki kadhaa mpaka nane na baada ya hapo utakuwa na unapata dozi ya nyongeza kila wiki kwa mwaka mzima. Lengo la matibabu haya ni kuondoa maumivu ya kibofu.

 

Tumia tiba mbadala

 

​

Tumia tiba mbadala ambazo zinafanya kazi zipo na unaweza kuzitumia. Baadhi ya tiba huwa ni acupuncture au tiba ya dawa za kurejesha asili ya kuta za ndani ya kibofu pamoja na kuondoa uvimbe wa kibofu kutokana na shambulio la kinga za mwili.

 

​

Upasuaji

​

​

Hufanyika kuondoa vidonda au kuongeza uwezo wa kibofu kutunza mkojo mwingi, matibabu ya upasuaji hufanyika baada ya njia zote kushindwa.

 

​

Matibabu ya nyumbani

 

Matibabu haya huhusisha

 

  • Kujikinga na vyakula vinavyopelekea tatizo lako kuwa kali Zaidi kama vile

  • Vinywaji vilivyo na carbon kama soda, kahawa, chocolate, matunda yenye chachu na vyakula vyenye vitamin C kwa wingi.

  • Vyakula na vinywaji kama vile nyanya, pombe na vyakula vilivyotiwa chachu kama piko na viungo vingi vinatakiwa kuepukwa pia.

  • Vyakula vingine ambavyo unadhani ukila na unapata dalili kali ni vema ukaviepuka pia.

​

 

Kufundisha kibofu

​

  • Huhusisha kukojoa kwa wakati uliopanga badala ya kusubiri hamu ya kukojoa itokee.  Anza kwa kujiwekea muda kwamba, kila baad aya nusu saa unatakiwa kukojoa, baad aya hapo, endapo umefanikiwa kwa muda huo, ongeza nusu saa tena iwe kila baada ya saa moja. Jifunze pia namna ya kulegeza kibofu chako kwa kupumua taratibu na kwa kina, huku ukiwa unafikiria kuhusu upumuaji wako. Usilete kitu cha nje kikuchukue akili yako.

  • Vaa nguo zisizobana tumbo lako

  • Punguz amsongo wa mawazo

  • Acha kuvuta sigara maana huweza kufanya tatizo likawa na dalili kaliz aidi

  • Fanya mazoezi ya kunyoosha misuli ya mwili kusaidia kupunguza maumivu ya kibofu.

 

Madhara

​

  • Kupungua uwezo wa kibofu kutunza mkojo- hii ni kwa sababu kibofu hukakamaa na kusababisha kuta zake kushindwa kutanuka ili kutunza mkojo

  • Kupungua kwa ubora wa maisha- hii ni kutokana na hali ya kwenda

  • Kuharibika kwa mahusiano ya kingono

  • Msongo wa mawazo

​

ULY CLINIC inkushauri siku zote ufuate ushauri wa daktari wako kabla ya kuchukua hatua baada ya kusoma makala hii.

​

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kupitia namba za simu au kubonyeza pata tiba chini ya tovuti hii kwa ushauri na tiba.

​

Imeboreshwa 20.01.2021

​

Rejea za Makala hii;

​

  1. American Urological Association. Diagnosis and treatment of interstitial cystitis/bladder pain syndrome. Linthicum, Md. http://www.auanet.org/education/guidelines/ic-bladder-pain-syndrome.cfm. Accessed July 1, 2016.

  2. Clemens JQ. Pathogenesis, clinical features, and diagnosis of interstitial cystitis/bladder pain syndrome. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 20.01.2020

  3. Interstitial cystitis/painful bladder syndrome. National Institute of Diabetes and Digestive and Kidney Diseases. http://kidney.niddk.nih.gov/kudiseases/pubs/interstitialcystitis/. Imechukuliwa 20.01.2020

  4. Longo DL, et al., eds. Dysuria, bladder pain, and the interstitial cystitis/bladder pain syndrome. Harrison's Principles of Internal Medicine. 19th ed. http://www.accessmedicine.com. Imechukuliwa 20.01.2020

  5. Merck Manual Professional Version. Interstitial cystitis. http://www.merckmanuals.com/professional/genitourinary_disorders/voiding_disorders/interstitial_cystitis.html. Imechukuliwa 20.01.2020

  6. National Institute of Diabetes and Digestive and Kidney Diseases. The urinary tract and how it works. https://www.niddk.nih.gov/health-information/health-topics/Anatomy/urinary-tract-how-it-works/Pages/anatomy.aspx. Imechukuliwa 20.01.2020

  7. Up-to-date. Clemens JQ. Management of interstitial cystitis/bladder pain syndrome. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 20.01.2020

  8. Wein AJ, et al., eds. Bladder pain syndrome (interstitial cystitis) and related isorders. In: Campbell-Walsh Urology. 11th ed. Philadelphia, Pa.: Elsevier; 2016. http://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 20.01.2020

bottom of page