top of page

Imeandikwa na daktari wa ULY-Clinic 

 

Sifa za sindromu ya kichanga pombe(fetal alcohol syndrome)

Kichanga pombe ni neno ambalo limetumika kumaanisha mtoto anayedhaliwa na dalili na viashiria vinavyotokana na mama kutumia pombe wakati waujauzito wake

Sifa za kichanga pombe zinajumuisha

  1. Kushindwa kuongezeka kwa urefu, uzito na kichwa kunakoanzia uchangani.

  2. Maumbile mabaya ya sura

  3. Madhaifu ya moyo- matundu kwenye moyo

  4. Madhaifu madogo ya maungio na miguu- kama kushindwa kujongea  kwa miguu n.k

  5. Kudumaa kiakili na kiukuaji wa mtoto huweza kuwa wastani au dalili kali sana

Imechapishwa 3/3/2015

Imeboreshwa 29/11/2020

bottom of page