Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
3 Aprili 2020, 18:30:55

Aspirini
Dawa hii kwa jina lingine hujulikana kama acetylsalicylic asidi.
Hutumika sana kupunguza homa na maumivu kiasi na wastani yanayotokana na maumivu ya misuli, maumivu ya jino na homa baridi. Dawa hii pia inaweza kupunguza maumivu ya athraitizi.
Sifa za dawa
Ipo kwenye kundi la dawa zijulikanazo kwa jina la NSAIDs
Hutumika kutibu homa pamoja na maumivu
Hupatikana katika mfumo wa kidonge
Mara nyingi rangi ya dawa hii ni nyeupe
Dawa hii inapaswa kutumika pamoja na chakula ili kuepusha maudhi kwenye mfumo wa chakula
Dawa zingine ambazo zipo kwenye kundi moja pamoja na acetaminophen ni:
Paracetamol
Diclofenac
Ibuprofen
Naproxen
Jinsi inavyofanya kazi mwilini?
Dawa hii hufanya kazi kwa kuzuia utengenezwaji wa kemikali ya prostaglandin mwilini. Kemikali hii hufahamika kusababisha maumivu ,homa na infamesheni.
Kazi za Aspirin Mwilini ni kama zifuatazo:
Hutumika kuondoa na kutibu maumivu
Hutumika kuondoa homa
Hutumika kupunguza sindromu ya akyuti koronari, huu ni moja ya ugonjwa wa moyo unaotokana na kuziba kwa mishipa ya damu ya koronari.
Hutumika kupunguza kasi ya kupata magonjwa ya moyo kwa wagonjwa waliopo katika kundi hatarishi kupata hasa miaka 40-70
Hutumika kwa wagonjwa wa kiharusi cha iskemia na iskemia ya mpito
Hutumika kwa wagonjwa wa osteoarthraitisi, arthraitisi ya rheumatoid haya ni magonjwa ambayo hupelekea kupata maumivu na kuvimba kwenye maungio ya mwili dawa hii hutumika kuzuia maumivu na uvimbe.
Hutumika kuzuia saratani ya kolorekto
Hutumika kutibu maumivu ya kipanda uso
Aspirini haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo:
Dichlorphenamide
Ketorolac
Captopril
Ibuprofen
Methotrexate
Fosinopril
Enalapril
Macimorelin
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao:
Vidonda vya tumbo vinavyotoa damu
Anemia ya Hemolitiki
Ugonjwa wa hemophilia
Wenye polipu (nyama) puani zilizosababishwa na pumu
Wagonjwa wenye kidole tumbo (appendisaitizi)
Pumu
Kuhara kwa muda mrefu
Dawa hii inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wafuatao:
Wenye upungufu wa damu
Wenye historia ya vidonda vya tumbo
Wagonjwa wa Ini
Wenye Figo iliyoferi kutokufanya kazi
Wenye upungufu wa vitamin K
Watumiaji wa pombe
Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha.
Kwa mama mjamzito: Endapo kuna ulazima wa kutumia dawa hii, dozi ndogo itumike ili kumuepusha mama pamoja na mtoto kwenye magonjwa ya kuvuja damu.
Kwa mama anayenyonyesha: Haipaswi kutumika kwa mama anayenyonyesha sababu ina madhara kwa mtoto. Huweza kuleta shida ya kutokwana damu pasipo kuganda kwa mtoto.
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hi ni pamoja na :
Maumivu ya tumbo
Kichefuchefu
Masikio kupunguza usikivu
Kuharibu ini
Kuharibu figo
Kutapika
Kubana kwa njia za hewa na kuleta shida katika upumuaji
Kuvimba kwa ngozi ndani bila maumivu
Matatizo ya damu kutoganda kirahisi
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Endapo ukisahau kunywa dozi yako, unaweza kunywa mara pale utakapokumbuka ,Isipokuwa endapo muda wa dozi nyingine umeshafika unatakiwa kuruka hiyo dozi uliyosahau na kuendelea na dozi yako kama muda uliopangiwa
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021, 11:49:33
Rejea za mada hii:-