top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

24 Aprili 2020 09:04:33

Atenolol

Atenolol

Atenolol ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyo katika kundi la dawa linaloitwa beta bloka. Dawa hii iliyo maarufu pia kwa jina la Tenormin huwa na rangi nyeupe au maziwa, hata hivyo rangi ya dawa hutegemea aina ya kiwanda kinachotenegeneza


Fomula ikemia ya dawa ni


C14H22N2O3


Ufyonzwaji wa dawa


Mara baada ya kunywa dawa, asilimia 50 hufyonzwa kwa haraka na utumbo ili kuingia kwenye damu, kiasi kinachobaki hutolewa kwenye kinyesi.


Dawa hufikia kilele kwenye damu kati ya masaa 2 hadi 4 baada ya kuingia tumboni. Tofauti na dawa zingine kwenye kundi lake yaani nadolol, atenolol hufanyiwa metabolizimu kidogo kwenye ini au kupita bila kufanyiwa metabolizimu. Mabaki ya dawa hutolewa nje ya mwili kwa njia ya mkojo(asilimia 85) ndani ya masaa 24 kwa dozi ya mishipa na asilimia 50 tu kwa dozi ya kidonge.


Atenolol hupatikana katika mfumo wa kidonge chenye uzito wa miligramu;


 • 25mg

 • 50mg na

 • 100mg


Namna dawa inavyofanya kazi kupunguza shinikizo la damu;

Dawa jamii ya beta bloka ikiwa pamoja na Atenolol hufanya kazi zifuatvyo ili kupunguza shinikizo la damu;


Huzuia ufanyaji kazi wa homoni epinefrini na kuchochewa kwa seli za beta adrenejik zilizo kwenye mishipa ya damu.


Kwa kufanya hivi hupunguza mapigo ya moyo kwenda kasi na shinikizo la damu la juu hivyo kuruhusu mzunguko wa damu kuwa wa kawaida.


Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo:

 • Acebutolol (Sectral)

 • Betaxolol (Kerlone)

 • Bisoprolol (Zebeta, Ziac)

 • Carteolol (Cartrol)

 • Carvedilol (Coreg)

 • Labetalol (Normodyne, Trandate)

 • Metoprolol (Lopressor, Toprol-XL)

 • Nadolol (Corgard)

 • Nebivolol (Bystolic)

 • Penbutolol (Levatol)

 • Pindolol (Visken)

 • Propanolol (Inderal)

 • Sotalol (Betapace)

 • Timolol (Blocadren)


Kazi za dawa ni;


 • Kutibu shinikizo la juu la damu

 • Kutibu Anjina pektorisi

 • Kutibu mayokadio infaksheni


Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo:


 • Verapamil

 • Timolol

 • Sotalol

 • Saquinavir

 • Rivastigmine

 • Propranolol

 • Pindolol

 • Penbutolol

 • Nebivolol

 • Nadolol

 • Metoprolol

 • Lofexidine

 • Labetalol

 • Esmolol

 • Diltiazem

 • Digoxin

 • Clonidine

 • Celiprolol

 • Carvedilol

 • Bisoprolol

 • Betaxolol

 • Acebutolol

Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao:

 • Wagonjwa wenye mzio na dawa hii au jamii ya dawa za Beta bloka

 • Wagonjwa wenye bradikadia ya sainazi

 • Wagonjwa walio na upinzani kwenye umeme wa moyo

 • Wagonjwa wenye shoku ya kadiojeniki

 • Wagonjwa walioferi moyo na kuwa na dalili za kuchoka na kushindwa kupumua vema


Dawa hii inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wafuatao;


 • Wagonjwa wenye kisukari

 • Wagonjwa wenye haipathairodizim

 • Wagonjwa wenye shida ya figo

 • Wagonjwa wenye shida ya Ini

 • Wagonjwa wenye shida ya Moyo kuferi

 • Wagonjwa wenye umri mkubwa


Matumizi wakati wa ujauzito

Dawa hii itumike wakati wa tahadhari ambapo hamna dawa nyingine ya mbadala ya kumpa mama mjamzito. Takwimu zinaonyesha kuwa kuna madhara ya kutumia hii dawa


Matumizi ya dawa wakati wa kunyonyesha

Dawa hii huingia kwenye maziwa ya mama anayenyonyesha, watoto wanaozaliwa na mama anayetumia dawa hii wana hatari ya kupata haipoglaisemia na hupelekea mapigo ya moyo kuwa chini. Hivyo itumike kwa uangalifu


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa ni;


 • Kizunguzungu

 • Maumivu ya miguu na misuli

 • Haipotesheni

 • Msongo wa mawazo

 • Kuharisha

 • Kuota njozi usiku

 • Kutokwa na vipele

 • Miguu kuwa baridi

 • Mwili kuchoka


Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?


Endapo ukisahau kunywa dozi yako, kunywa mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

3 Novemba 2021 11:49:46

Rejea za mada hii:-

1.Modern pharmacology with Clinical applications written by Charles R. Craig and Robert E. Stitizel ISBN 978-0316159340 ukurasa wa 170,196 na 201-2013

2.FDA.Atenolo. https://www.accessdata.fda.gov/drugsatfda_docs/label/2012/018240s032lbl.pdf. Imechukuliwa 23/4/2020

3.Drugs.Atenolol.https://www.drugs.com/atenolol.html. Imechukuliwa 23/4/2020

4.Medscape.Atenolol.https://reference.medscape.com/drug/tenormin-atenolol-342356. Imechukuliwa 23/4/2020

5.WebMd.Atenolol.https://www.webmd.com/drugs/2/drug-11035/atenolol-oral/details. Imechukuliwa 23/4/2020

6.MedicinePlus.Atenolol.https://medlineplus.gov/druginfo/meds/a684031.html. Imechukuliwa 23/4/2020
bottom of page