Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
26 Oktoba 2020 07:16:11
Dawa ya Acrisorcin
Acrisorcin ni dawa mojawapo ya kutibu magonjwa ya fangasi iliyopo katika kundi la dawa linaloitwa antifangasi. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Akrinol
Fomu ya dawa Acrisorcin
Acrisorcin hupatikana katika fomu ya mafuta kwa ajili ya kupaka
Namna Acrisorcin inavyofanya kazi
Dawa ya Acrisorcin ni aina ya dawa ambayo hufanya kazi kwa kufungamana na steroli (ergosteroli) kwenye ukuta wa seli ya fangasi. Kwa kufanya hivi hutengeneza matundu na kufanya ukuta wa seli kuwa na uzaifu ambapo hupelekea kuruhusu kuvuja kwa sehemu za ndani na kufa kwa fangasi. Ergosteroli ni aina ya steroli ambayo ni kiungo kikuu katika ukuta wa seli ya fangasi na ni sehemu ambayo dawa hii hufanya kazi yake na dawa nyingine ya Azole.
Dawa zingine kundi moja na Acrisorcin
Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo: ⦁ Amphotericin B ⦁ Butoconazole ⦁ Capsofungin ⦁ Econazole ⦁ Flucytosine ⦁ Griseofulvin ⦁ Itraconazole ⦁ Miconazole ⦁ Naftifine hydrochloride ⦁ Oxiconazole nitrate ⦁ Sulconazole nitrate ⦁ Terbinifine ⦁ Terconazole ⦁ Tioconazole ⦁ Tolnaftate
Kazi ya dawa Acrisorcin
Hutumika kwenye matibabu ya Pityriasis versicolor
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Acrisorcin
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi
Tahadhari kwa watumiaji wa Acrisorcin
⦁ Dawa hii huweza kupelekea shida kwenye ini ⦁ Huweza kusababisha kubana kwa mirija ya mfumo wa upumuaji
Matumizi ya Acrisorcin kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
⦁ Dawa hii bado haijapewa kundi la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito ⦁ Dawa hii inaweza kutumika endapo itahitajika sana kwa mama mjamzito bila kuwepo kwa dawa nyingine mbadala
Matumizi ya Acrisorcin kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Hakuna takwimu zinazoonyesha kuwa dawa hii hutolewa kwenye maziwa ,Inaweza kutolewa kwa tahadhari
Maudhi ya kutumia Acrisorcin
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni pamoja na : • Kuharisha • Haipokalemia • Kichefuchefu • Ngozi kuwasha
Endapo utasahau dozi yako ya Acrisorcin ufanyaje ?
Endapo ukisahau kutumia dozi yako, tumia mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine, acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako inayofuata kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:54:56
Rejea za mada hii:-