top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

9 Julai 2020 08:20:00

Dawa ya Terconazole

Dawa ya Terconazole

Terconazole ni dawa mojawapo ya kutibu magonjwa ya fangasi iliyoko katika kundi la dawa linaloitwa antifangasi aina ya Triazole. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Terazol


Terconazole hupatikana katika mfumo wa krimu wenye ujazo wa asilimia mbalimbali kama

• 0.4

• 0.8


Terconazole hupatikana katika mfumo wa kidonge kwa ajili ya kuweka ukeni chenye uzito wa miligramu 80


Namna dawa inavyofanya kazi ili kutibu fangasi


Dawa hii hufanya mambo yafuatayo ili kutibu fangasi;


• Dawa hii ya Terconazole hufanya kazi zake kwa kuharibu ukuta wa seli ya fangasi. Terconazole na aina nyingine za dawa ya fangasi hufanya kazi kwa kuzuia utengenezaji wa homoni ergosteroli,homoni hii ni muhimu sana kwani huhusika katika utengenezaji wa vijenzi muhimu vya ukita wa seli ya fangasi.


Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo;


• Albaconazole

• Efinaconazole

• Epoxiconazole

• Fluconazole

• Isavuconazole

• Itraconazole

• Posaconazole

• Propiconazole

• Ravuconazole

• Voriconazole


Kazi za hii dawa ni kama ifuatavyo:


• Hutumika kwenye matibabu ya fangasi aina ya Kandidiasisi.


Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao;


• Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi


Kundi la dawa kipinid cha ujauzito


• Dawa hii ipo kwenye kundi B la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito


Matumizi kwa mama mjamzito


• Dawa hii hushauriwa kutumika wakati wa kipindi cha ujauzito


Matumizi kwa mama anayenyonyesha


• Takwimu hazijaonyesha kuwa kuna uwezekano wa hii dawa kuingia kwenye maziwa ya mtoto ila itumike kwa wamama wajawazito kwa uangalifu.


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa ni;


• Mwili kupata Homa

• Maumivu ya kichwa

• Kuwashwa kwenye uke

• Kukojoa sana

• Maumivu wakati wa hedhi


Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?


Endapo ukisahau tumia dozi yako, tumia mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi inayofuata kama ulivyopangiwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023 16:55:27

Rejea za mada hii:-

1. Modern pharmacology with Clinical applications written by Charles R. Craig and Robert E. Stitizel ISBN 978-0316159340 ukurasa wa 601

2. Drugs.Terconazole.https://www.drugs.com/mtm/terconazole-vaginal.html. Imechukuliwa 07.07.2020

3.Medscape.Terconazole.https://reference.medscape.com/drug/terazol-3-terconazole-vaginal-342596. Imechukuliwa 07.07.2020

4.WebMd.Terconazole.https://www.webmd.com/drugs/2/drug-78031/terconazole-vaginal/details. Imechukuliwa 07.07.2020

5.MedicinePlus.Terconazole.https://medlineplus.gov/druginfo/meds/a688022.html. Imechukuliwa 07.07.2020

6.Drugbank.Terconazole.https://www.drugbank.ca/drugs/DB00251. Imechukuliwa 07.07.2020
bottom of page