top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

2 Aprili 2020 04:36:40

Kalisiamu

Kalisiamu

Kalisiamu ni madini yanayopatikana katika vyakula vingi. Hiki ni kirutubisho ambavyo viumbe hai vyote vinahitaji ikiwa pamoja na wanadamu. Madini haya huwa na nguvu na umuhimu kwa afya ya mfupa.


Mwili huhitaji kalisiamu kusaidia kudumisha mifupa yenye nguvu na kutekeleza majukumu mengi muhimu. Karibu kalsiamu yote huhifadhiwa kwenye mifupa na meno, ambapo inasaidia muundo na uimara wao. Asilimia 99 ya kalisiamu ya mwili huwa kwenye mifupa na meno.


Kwa kuongezea, kalisiamu hutumiwa kusaidia mishipa ya damu na moyo kusukuma damu kwenye mwili wote na pia kusaidia kutolewa kwa homoni na vimeng’enya zinazoathiri karibu kila kazi kwenye mwilini.


Wanadamu wanahitaji kalisiamu kujenga na kudumisha mifupa yenye nguvu na kudumisha mawasiliano mazuri kati ya ubongo na sehemu zingine za mwili.


Kalsiamu kwa asili hupatikana kwenye vyakula vingi na watengenezaji wa chakula huiongeza kwenye bidhaa malimbali na virutubisho.


Mbali na kalsiamu, watu pia wanahitaji vitamini D, kwani vitamini hii inasaidia mwili kutumia kalsiamu.

Kalsiamu katika lishe


Kalsiamu ni madini yanayopatikana kwa wingi katika mwili wa binadamu. Meno na mifupa yana kalisiamu zaidi. Seli za neva, tishu za mwil na damu yana kalsiamu iliyobaki.


Kazi za madini ya kalisiamu


Kalsiamu ni moja ya madini muhimu kwenye mwili wa binadamu. Inasaidia kuunda na kudumisha meno na mifupa yenye afya. Kiwango sahihi cha kalsiamu katika mwili kwa muda wote wa maisha kinaweza kusaidia kuzuia ugonjwa wa mifupa.Kalsiamu husaidia mwili wako katika kufanya vifuatavyo:


• Kuunda mifupa na meno yenye nguvu

• Kugandisha damu

• Kulainisha misuli

• Kutoa homoni na kemikali zingine

• Kuweka mapigo ya moyo kawaida


Ukosefu wa kalsiamu unaweza kusababisha hali inayoitwa matege kwa watoto, na ugonjwa wa mifupa katika maisha ya baadaye.


Vyanzo vya madini kalsiamu:


Vyakula vyenye kalsiamu nyingi watu wanaweza kupata kalsiamu kutoka kwa vyakula na vinywaji kadhaa ambavyo ni vyanzo vya kalsiamu ni pamoja na:


• Maziwa na vyakula vingine vya maziwa

• Mboga za majani kama vile kabichi lakini sio mchicha

• Maharagwe ya soya

• Karanga

• mkate na kitu chochote kilichotengenezwa na unga wa ngano

• samaki

• kunde na nafaka


Kalsiamu ni sababu ya vimeng’anya vgyingi. Bila kalsiamu, enzymes kadhaa muhimu haziwezi kufanya kazi vizuri.


Ni nini kinachotokea ikiwa mwili una kalsiamu nyingi?


Kuchukua kipimo kikubwa cha kalsiamu (zaidi ya 1,500mg kwa siku) kunaweza kusababisha maumivu ya tumbo na kuhara.


Utafiti pia umependekeza kwamba ulaji wa kalsiamu ya kutosha inaweza kusababisha:


• shinikizo la damu kwa vijana

• shinikizo la damu wakati wa ujauzito

• kuboresha mafuta kwenye mwili


Makundi fulani ya watu yana uwezekano mkubwa kuliko wengine kuwa na shida kupata kalsiamu ya kutosha:


Wanawake wawaliacha kuwa na hedhi, wanapata hasara kubwa ya mifupa na huwachukua pia kalisiamu. Ulaji wa kutosha wa kalsiamu kwenye chakula na virutubisho vingine huwa vinahitajika na pia unaweza kupunguza kasi ya upotezaji wa mfupa.


Wanawake wa umri wa kuzaa watoto ambao wakati wa hedhi hawapati (amenorrhea) kwa sababu ya mazoezi sana hula kidogo. Wanahitaji kalsiamu ya kutosha ili kukabiliana na kalsiamu iliyopungua, kuongezeka kwa upungufu wa kalisiamu katika mkojo na kusababisha udhaifu katika mfupa.


Vegans (watu ambao hawali nyama au bidhaa za nyama) kwa sababu huepuka bidhaa za nyama ambazo ni chanzo kikuu cha kalsiamu katika chakula.


Hali inayoonyesha uhitaji wa kalisiamu ya kutosha?


Ulaji usio wa usawa wa kalsiamu haitoi dalili dhahiri kwa muda mfupi kwa sababu mwili huweka viwango vya kalsiamu katika damu kwa kuichukua kutoka kwa mfupa. Kwa muda mrefu ulaji wa kalsiamu wa chini husababisha ugonjwa wa mifupa na kuongeza kwa hatari mfupa kuvunjika.


Dalili za upungufu mkubwa wa kalsiamu ni pamoja na:


• Mwili kufa ganzi

• Kutetemeka kwa vidole,

• Mwili kututumka,

• Mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida ambayo yanaweza kusababisha kifo ikiwa haitarekebishwa


Je! Ni athari gani za kalsiamu kwenye afya?


Wanasayansi wanaendelea kufanya utafiti wa kalsiamu kuelewa jinsi inavyoathiri afya. Hapa kuna mifano kadhaa ya kile utafiti huu umeonyesha:


  • Afya ya mfupa na ugonjwa wa mifupa: Mifupa inahitaji kalsiamu na vitamini D wakati wote wa utotoni na ujana kufikia ukubwani na maudhui ya kalsiamu hutokea kwenye umri takriban wa miaka 30. Baada ya hapo mifupa hupoteza kalsiamu kidogo, lakini watu wanaweza kusaidia kupunguza hasara hizi kwa kupata kiwango kilichopendekezwa cha kalsiamu kwa watu wazima na na kuwa na maisha mazuri ya kuishi ambayo ni pamoja na shughuli za mwilikupunguza uzito (kama vile kutembea na kukimbia).

  • Osteoporosisi ni ugonjwa wa mifupa kwa watu wazima wakubwa (haswa wanawake) ambao mifupa inakuwa dhaifu na inayoweza kuvunjika. Ulaji wa kutosha wa kalsiamu na vitamini D pamoja na mazoezi ya mara kwa mara ni muhimu kuweka mifupa yenye afya wakati wote wa maisha. Kuchukua virutubisho vya kalsiamu na vitamini D hupunguza hatari ya kuvunjika kwa mfupa na hatari ya kuanguka kwa udhaifu, wazee ambao huwa mara nyingi huwa na shida hii. Lakini haijulikani wazi virutubisho gani huwa vinasaidia kuzuia kuharibika kwa mfupa na kuanguka kwa wazee ambao huishi nyumbani.

  • Saratani: Uchunguzi umeonyesha kuwa virutubisho vya kalsiamu au lishe nyingi kwenye kalsiamu zinaweza kupunguza hatari ya kupata saratani ya utumbo mkubwa

  • Ugonjwa wa moyo na mishipa: Tafiti zingine zinaonyesha kuwa kupata kalisiamu ya kutosha kunaweza kupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo na kiharusi. Uchunguzi mwingine hugundua kuwa kiwango kikubwa cha kalisiamu haswa kwenye virutubisho vinaweza kuongeza hatari ya ugonjwa wa moyo.

  • Shinikizo la damu: Tafiti zingine zimegundua kuwa ulaji wa kalsiamu uliyopendekezwa kunaweza kupunguza hatari ya kupata shinikizo la damu.

  • Kifafa cha mimba ni hali mbaya ya kiafya ambayo mwanamke mjamzito huwa na shinikizo la damu na shida kwenye figo ambayo husababisha protini kuwa ndani ya mkojo. Ni sababu inayoongoza ya magonjwa na kifo kwa wanawake wajawazito na watoto wao wachanga.

  • Mawe kwenye figo, Mawe mengi ya figo huwa sana katika oxalate ya kalsiamu. Uchunguzi mwingine umegundua kuwa ulaji wa kiwango cha juu cha kalsiamu kutoka kwa virutubisho vya lishe unahusishwa na hatari kubwa ya mawe kutengeneza kwenye figo haswa kwa watu wazee .

  • Kupunguza uzito, Ingawa tafiti kadhaa zimeonyesha kuwa kupata kalsiamu zaidi husaidia kupunguza uzito wa mwili au kupunguza uzani kwa wakati, tafiti nyingi zimegundua kuwa kalsiamu - kutoka kwa vyakula au virutubisho vya lishe- haina athari yoyote kwenye uzito wa mwili na kiwango cha mafuta ya mwili


Daktari anaweza kupendekeza kalsiamu ya ziada kwa watu ambao:


• Watu ambao hawanywi maziwa ya ng'ombe

• Kwa watu ambao hawali nyama (vegan)

• Kwa watu wenye upungufu wa kalsiamu


Hali zifuatazo au tabia ya maisha inaweza kusababisha kiwango cha chini cha kalsiamu, pia hujulikana kama hypokalemia:


• Shida za kula (Anorexia).

• Kutokana na madini ya zebaki na magnesiamu

• Matumizi ya muda mrefu yakulainisha misuli(laxatives).

• Matumizi ya muda mrefu ya dawa kadhaa, kama vile kemotherapi.

• Ukosefu wa homoni ya parathyroid

• Saratani kadhaa

• matumizi makubwa ya kafeini, soda, au pombe

• hali zingine, kama ugonjwa wa tumbo, ugonjwa wa Crohnna magonjwa mengine ya kumengenya

• kushindwa kwa figo

• upungufu wa vitamini D

• upungufu wa phosphati


Mwili huondoa kalisi fulani cha madini ya kalisiamu katika jasho, mkojo, na kinyesi. Chakula na shughuli zinazohimiza kazi hizi zinaweza kupunguza kiwango cha kalsiamu mwilini.


Je! Kalisiamu inaweza kuwa na madhara?


Vidonge vya lishe ya kalsiamu vinaweza kuingilianana dawa fulani unazotumia, na dawa zingine zinaweza kupunguza au kuinua kiwango cha kalsiamu mwilini. Hapa kuna mifano kadhaa:


• Bisphosphonates (kutibu osteoporosis)

• Antibiotiki ya fluoroquinolone na familia ya tetracycline

• Levothyroxine (kutibu tezi)

• Phenytoin (anticonvulsant)

• Tiludronate disodium (kutibu ugonjwa wa Paget).

• Diuretics hutofautiana katika athari zao.

• Glucocorticoids (kama vile prednisone) inaweza kusababisha kupungua kwa kalsiamu na mwishowe

kupata ugonjwa wa mifupa.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

28 Januari 2022 19:34:33

Rejea za mada hii:-

1. Medicine plus on rile of calcium in the body. https://medlineplus.gov/ency/article/002412.htm

2. Benefits and sources of calcium. Medically reviewed by Kathy Warwick, RD, LD on January 28, 2020 — Written by Tim Newman. https://www.medicalnewstoday.com/articles/248958#side-effects-of-calcium-supplements

3. National health institute,Office of dietary supplements.https://ods.od.nih.gov/factsheets/Calcium-Consumer/
bottom of page