top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter B, MD

Mhariri:

Dkt. Samweli M, MD

19 Desemba 2021 11:49:42

Image-empty-state.png

Dalili hatari kwenye ujauzito

Kuna dalili mbalimbali ambazo mjamzito au ndugu waishio na mjamzito wanapaswa kuzifahamu ili zitakapotokea waweze kumsisitiza na kumfikisha mjamzito katika kituo cha afya cha karibu aweze kupatiwa husuma. Hii itaepusha hatari ya madhara kwa mama na mtoto. Dalili za hatari kwa mjamzito ni pamoja na;

​

Kutokwa damu kusiko kawaida

​

Wakati wa ujauzito kutokwa na majimaji ya rangi nyeupe, kahawia, au pink ni kitu cha kawaida. Kutokwa na majimaji yenye damu au yenye mabonge ya damu huwa si kitu cha kawaida katika ujauzito, unahitaji kuonana na daktari ili kujua tatizo ni nini

​

Maumivu makali ya tumbo

​

Maumivu wastani ya tumbo wakati wa ujauzito yanaweza yakawa ni kwa sababu ya mgandamizo wa mtoto kwenye mishipa au tumbo la mama, maumivu makali ya tumbo huweza kumaanisha vitu mbalimbali pamoja na shinikizo la damu linaloelekea kifafa cha mimba au mimba kutungwa nje ya mfuko wa kizazi

Baada ya kujifungua maumivu ya tumbo huweza kumaanisha maambukizi katika via vya uzazi

​

Kutokwa kwa maji mengi ukeni

​

Maji ya chupa ya uzazi huwa na rangi kama ya mkojo, na huweza kuhisiwa ni mkojo mpaka mtu atofautishe kwa kunusa harufu ya maji hayo. Maji yakitoka mengi ukeni humaanisha kupasuka kwa chupa ya uzazi na pia hupelekea mtoto kushindwa kukua tumboni au mimba kutoka. Sababu zinazoweza kusababisha maji kutoka ukeni ni pamoja na majeraha kwenye tumbo la mama, maambukizi ndani ya mfuko wa kizazi wakati wa ujauzito n.k. Mambo yanayoweza kuambatana na kupungua kwa maji kwenye chupa ya uzazi huwa pamoja na mimba kutoka

​

Mtoto Kupunguza kucheza tumboni

​

Kupungua kucheza kwa mtoto tumboni humaanisha mtoto anaumwa, mtoto kuacha kucheza kabisa kunaweza maanisha mtoto amefia tumboni au yupo kwenye hali mbaya. Mtoto huanza kucheza tumboni kuanzia wiki ya 16 hadi ya 20 katika ujauzito. Wakati wamama wenye ujauzito wa kwanza huchelewa kusikia mtoto anacheza, wale walio na ujuzito wa pili na kuendelea huwahi kusikia mtoto anacheza tumboni.

​

Kubana kwa tumbo

​

Maumivu yenye sifa ya kubana na kuachia kwenye tumbo la chini yanayotokea kila baada ya mda Fulani kupita kwa utaratibu maalumu kabla ya kukamilisha wiki 37 za ujauzito humaanisha dalili mbaya ya mimba kutoka kabla yam da kutimia. Maumivu haya huweza kusababisha mimba kutoka na humaanisha kuna shida katika ujauzito wa mama.

​

Kuongezeka kwa shinikizo la damu mwilini(presha)

​

Kuongezeka kwa shinikizo la damu wakati wa ujauzito humaanisha mwili unapambana na sumu Fulani ndnai ya mwili, mtoto akiwa tumboni mwili humtambua kuwa ni kitu kigeni na hujaribu kupambana ili kukiondoa. Kwa sababu kinga za mwili hushuka wakati wa ujauzito, basi mimba huweza kuendelea kukua mpaka kukamilisha miezi 9 ya ujauzito. Kwa baadhi ya watu huweza kupata madhara kama kuongezeka kwa shinikizo la damu linalopelekea kifafa au kupata kifafa cha mimba. Endapo mama ameongezeka shinikizo la damu basi ni vema kuhudhuria kliniki mara kwa mara na kupata ushauri wa daktari.

​

Kuvimba mwili

​

Kuvimba kwa miguu na mikono au kuvimba mwili mzima humaanisha

​

Kutokwa uchafu unaonuka ukeni


Kutokwa na uchafu mzito baada ya kujifungua, unaonuka kama samaki huweza kumaanisha maambukizi katika kizazi. Dalili zingine zinazoweza kuambatana ni maumivu ya tumbo la chini na homa.

​

Homa

​

Homa inaweza kumaanisha kuna maambukizi yanaoendelea ndani ya mwili

​

Kupoteza fahamu

​

Mama anaweza kupoteza fahamu kwa sababu ya kuishiwa damu au kuziba kwa mishipa ya damu katika mapafu kutokana na kuingia maji ya chupa ya uzazi katika mishipa ya damu. Hali hii huitwa embolism

​

Kutoona vema, kuona ukungu

​

Hali ya kutoona vema au kuona ukungu inaweza kumaanisha shinikizo la damu linaloelekea kuwa kifafa cha mimba au kwa jina jingine preeclampsia.

ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kufanya maamuzi yanayohusisha afya yako
Wasiliana na daktari wa  ULY Clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kutumia namba za simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

19 Desemba 2021 11:49:42

Rejea za dawa

  1. Mwilike, B, et al. Knowledge of danger signs during pregnancy and subsequent healthcare seeking actions among women in Urban Tanzania: a cross-sectional study. BMC Pregnancy Childbirth 18, 4 (2018). https://doi.org/10.1186/s12884-017-1628-6

  2. NCBI. Danger signs in pregnancyhttps://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK304178/. Imechukuliwa 15.11.2021

bottom of page