Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Sospeter B, MD
15 Novemba 2021 19:20:20
Dalili za hatari kwa mjamzito
Dalili za hatari wakati wa ujauzito ni dalili zinapaswa kufahamika sana kwa mjamzito pamoja na ndugu wanaomzunguka ili mara zitakapotokea hatua zichukuliwe haraka kulinda afya ya mama na mtoto tumboni. Zifuatazo ni dalili za hatari kwa mjamzito;
Dalili za upungufu wa damu
Dalili zinazomaanisha upungufu wa damu kwa mjamzito ni pamoja na;
Kulegea
Kupoteza fahamu
Uchovu
Kuishiwa pumzi
Kuhisi mapigo ya moyo
Dalili za ujauzito kutishia kutoka
Kutokwa na damu ukeni wakati wa ujauzito
Kupata maumivu ya tumbo mithiri ya uchungu
Dalili za kifafa cha mimba
Dalili zifuatazo kwa mjamzito, huweza ashiria kuwa na shinikizo la juu la damu linaloelekea kifafa cha mimba
Maumivu makali ya kichwa
Kiza cha macho
Maumivu kwenye chemba yamoyo
Kupoteza fahamu
Degedege
Kujaa maji mwilini kwa wingi (Kuvimba mikono au uso)
Dalili za maambukizi kwenye chupa ya uzazi
Baadhi yadalili zinazoashiria maambukizi kwenye chupa ya uzazi kwamjamzito ni;
Maumivu makali ya tumbo
Kupasuka chupa ya uzazi
Kuvuja ukeni kwa maji ya mji wa mimba
Kutokwa na maji yenye harufu mbaya ukeni
Dalili za kupasuka kwa chupa ya uzazi
Kuvuja kwa maji ya chupa ya uzazi ukeni (maji huweza fika mapajani au kwenye miguu)
Maumivu ya tumbo
Dalili za malaria
Dalili za malaria kwa mjamzito ni;
Homa
Kutetemeka
Kutapika
Dalili za mtoto kuumwa au kufia tumboni
Dalili za mtoto kuumwa au kufia tumboni mwa mjamzito ni;
Kuacha kuhisi hisia za mtoto kucheza tumboni
Kuisha kwa dalili za ujauzito
Tumbo la ujauzito kutokuwa
Maumivu ya tumbo mithiri ya uchungu
Wakati gani wa kuwasiliana na daktari?
Ni muhimu kwa mama, ndugu na mwenza kufahamu kuhusu viashiria vya hatari wakati wa ujauzito na kutafutamsaada kwa mtaalamu wa afya kwa msaada mara dalili hizo zitakapoonekana. Kuhudhuria kliniki kwa wakati huzuia madhara yanayoweza kutokea kwa mama na mtoto tumboni.
ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kufanya maamuzi yanayohusisha afya yako
Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kutumia namba za simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
16 Novemba 2021 07:03:38
Rejea za dawa
Mwilike, B, et al. Knowledge of danger signs during pregnancy and subsequent healthcare seeking actions among women in Urban Tanzania: a cross-sectional study. BMC Pregnancy Childbirth 18, 4 (2018). https://doi.org/10.1186/s12884-017-1628-6
NCBI. Danger signs in pregnancyhttps://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK304178/. Imechukuliwa 15.11.2021