top of page
Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Mangwella S, MD
16 Novemba 2021, 18:28:42
Kumkinga kichanga na baridi
Namna ya kumkinga kichanga kupatwa na baridi.
Ili kumkinga kichanga kupatwa na baridi unapaswa kufanya mamabo yafuatayo;
Mfute mtoto mara azaliwapo na mfunike kwa nguo kavu ili apate joto
Mpakate mtoto huku ukihakikisha kwamba ngozi yake na yako zinagusana
Mnyonyeshe mara tu baada ya kuzaliwa yaani ndani ya saa moja
Usimuogeshe mtoto mpaka baada ya masaa 24 kupita tangu kuzaliwa
Mpatie matunzo ya kangaruu kwa watoto waliozaliwa kabla ya muda (njiti) na watoto wanaozaliwa na uzito kidogo
ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kufanya maamuzi yanayohusisha afya yako
Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kutumia namba za simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
16 Novemba 2021, 18:28:42
Rejea za dawa
WHO. Kangaroo mother care a practical guide. http://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/42587/9241590351.pdf. Imechukuliwa 16.11.2021
bottom of page