Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Mangwella S, MD
15 Novemba 2021, 19:06:28
Mabadiliko ya mwili baada ya kujifungua
Mara baada ya kujifungua mama hupata mabadiliko ya kawaida katika mwili wake kwenye majimaji yanayotoka ukeni, mji wa mimba, matiti, saikolojia na kibofu cha mkojo na kisaikolojia. Ni muhimu kwa mama na ndugu anayemhudumia mama aliyejifungua kufahamu kuhusu mabadiliko haya .
Mji wa Mimba
mambo yafuatayo ni kawaida kutokea baada ya kujifungua;
Kunywea kwa mji wa mimba
Kuhisi maumivu makali baada ya kujifungua wakati mji wa mimba unaposinyaa
Majimaji ya ukeni
Baada ya kujifungua sifa za majimaji ukeni hubadilika jinsi siku zninavyoenda kisha kuwa kawaida. Ni muhimu ukaahamu kuwa majimaji ya ukeni baada ya kijifungua kwa kawaida huwa hayana harufu mbaya. Ikitokea kuwa na harufu mbaya hii humaanisha kuwa na tatizo hivyo uwasiliane na daktari.
Baada ya kujifungua, mabadiliko ya majimaji ukeni huwa kama ifuatavyo;
Siku nne za mwanzo:- Huwa na rangi nyekundu
Siku ya nne hadi tisa:- Majimaji hupungua na huwa na rangi ya pinki
Siku ya tisa hadi kumi na tano:- Rangi njano mpuko
Siku ya kumi na tano na kuendelea:- hakupaswi kuwa na majimaji ya ukeni baada ya kujifungua
Mabadiliko ya Matiti:
Tangu kujifungua mpaka siku ya tatu, matiti hutoa maziwa yenye rangi ya manjano (dang’a),
Maziwa yenye rangi ya manjano (dang’a) ni lishe tosha kwa mtoto mchanga kwa siku kadhaa za mwanzo,
Maziwa yenye rangi ya manjano (dang’a) humkinga mtoto mchanga dhidi ya maambukizi,
Matiti hujaa yanapoanza kutengeneza maziwa yenye rangi nyeupe.
Kibofu cha mkojo
Kiasi cha mkojo huongezeka mara baada ya kujifungua, hali hii hutokana na mabadiliko yanayotokea wakati wa ujauzito,
Baadhi ya kinamama hushindwa kukojoa mhimize mama akojoe mara kwa mara.
Mabadiliko Kisaikolojia:
Kwa kawaida kupata mtoto ni tukio lenye msisimko mkubwa kwa mama na familia. Hata
hivyo, wakati mwingine mama huonyesha hali zisizo za kawaida kutegemeana na mwitikio wake wa kisaikolojia.
Mabadiliko ya kisaikolojia yanayoweza kutokea baada ya kujifungua kama;
Mabadiliko ya kihisia kama vile kuridhika, furaha na msisimko na pia uchovu, hisia za unyonge, kutoridhika na kukata tamaa.
Ahueni – “Nashukuru, nimetua mzigo.” Haya hutamkwa na wanawake wengi mara baada ua kujifungua.
Wengine wanaweza kujisikia kuwa karibu zaidi na mwenzi au kichanga chake.
Baadhi wanaweza kuonyesha kutokumpenda mtoto, woga wa mambo asiyoyajua au uchovu
ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kufanya maamuzi yanayohusisha afya yako
Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kutumia namba za simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
16 Novemba 2021, 07:04:09
Rejea za dawa
Romano M, Cacciatore A, Giordano R, La Rosa B. Postpartum period: three distinct but continuous phases. J Prenat Med. 2010 Apr;4(2):22-5.
Brown JS, Posner SF, Stewart AL. Urge incontinence: new health-related quality of life measures. J Am Geriatr Soc. 1999 Aug;47(8):980-8.
Bystrova K, Matthiesen AS, Vorontsov I, Widström AM, Ransjö-Arvidson AB, Uvnäs-Moberg K. Maternal axillar and breast temperature after giving birth: effects of delivery ward practices and relation to infant temperature. Birth. 2007 Dec;34(4):291-300.
Nathan HL, El Ayadi A, Hezelgrave NL, Seed P, Butrick E, Miller S, Briley A, Bewley S, Shennan AH. Shock index: an effective predictor of outcome in postpartum haemorrhage? BJOG. 2015 Jan;122(2):268-75.
Matthys LA, Coppage KH, Lambers DS, Barton JR, Sibai BM. Delayed postpartum preeclampsia: an experience of 151 cases. Am J Obstet Gynecol. 2004 May;190(5):1464-6.
Benson MD, Haney E, Dinsmoor M, Beaumont JL. Shaking rigors in parturients. J Reprod Med. 2008 Sep;53(9):685-90.
Alekseev NP, Vladimir II, Nadezhda TE. Pathological postpartum breast engorgement: prediction, prevention, and resolution. Breastfeed Med. 2015 May;10(4):203-8
Woodd SL, Montoya A, Barreix M, Pi L, Calvert C, Rehman AM, Chou D, Campbell OMR. Incidence of maternal peripartum infection: A systematic review and meta-analysis. PLoS Med. 2019 Dec;16(12):e1002984