Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD
Mhariri:
Dkt. Peter A, MD
19 Desemba 2021, 11:34:39

Mabadiliko ya mwili kwenye ujauzito
Unapogundua kwamba una ujauzito, unaweza ukaanza kupanga kuhusu afya ya ujauzito wako wiki moja baada ya nyingine. Kila siku unaweza kuwa unajiuliza maswali jinsi ya kuwa na afya njema ya ujauzito uliobeba na mabadiliko ya mwili yanayotokea.
Nini au vipimo gani nifanye?
Kama umebeba mapacha unaweza kuanza kupanga kuhusu ujauzito huo kila wiki kwamba uzito gani natakiwa kua nao? Nini nifanye nisipate uchungu kabla ya wakati wake? Au unahitaji kupumzika?
Kwa Kila jambo unaloweza kujiuliza, kifupi ni kwamba ni muhimu kujua kuhusu ujauzito wako wiki moja baada ya nyingine kwa sababu kutakupa kufanya uamuzi sahihi kipindi chote cha ujauzito. Jifunze kuhusu vyakula vinavyotakiwa na ambavyo havitakiwi na upate elimu ya msingi kuhusu mambo flani yanayotokea kipindi cha ujauzito kuanzia mazoezi maumivu ya mgongo kujamiana. Kufahamu kuhusu ujauzito wako kunakuweka tayari kujiandaa wakati wowote kukabili mambo yanayoweza kutokea mbeleni wakati wa ujauzito
Kipindi cha kwanza cha ujauzito
Miezi mitatu ya kwanza (Kipindi cha kwanza cha ujauzito) huambatana na mabadiliko ya haraka ya mwili wako na kijusi aliyepo tumboni.
Mabadiliko kwa mama
Mabadiliko ya kimwili kwa mjamzito ni;
Maumivu ya matiti
Uchovu
Kichefuchefu
Hulka yako inaweza kuwa ya furaha au huzuni sana.
Mabadiliko kwa kijusi
Wakati huu kijusi huwa anakuwa haraka na kubadilika. Ubongo wa mtoto, uti wa mgongo na viungo au organi mbalimbali huanza kutengenezwa na moyo wa mtoto huanza kufanya kazi pia na vidole vya mkono na miguu huanza kuwa na umbo halisi.
Kama upo katika kipindi hiki cha miezi mitatu ya kwanza basi fanya mawasiliano na mtaalamu wa afya unaze kliniki kwa ajili ya wajawazito unaweza kujifunza kuhusu nini utarajie katika kipindi hiki na utakachojifunza kinaweza kukusaidia kuchukua hatua ili uwe na afya njema na mtoto wako
Kipindi cha pili
Kipindi chapili cha ujauzito, kuanzia miezi minne hadi sita unaweza kujisikia vyema kuliko ilivyokuwa miezi mitatu ya kwanza na wakati huu ni wa kufurahia ujauzito ulionao. Kipindi hiki mtoto anaanza kuonekana kuwa kama binadamu.
Mabadiliko kwa mama mjamzito
Dalili kwa mama zinaweza kuwa;
Maziwa kubwa makubwa
Tumbo kuongezeka
Mabadiliko ya ngozi yako.
Mabadiliko kwa mtoto tumboni
Mtoto hupata uwezo wa kucheza na kusikia pia. Unapofikisha wiki ishirini za ujauzito unakuwa katikati ya kipindi chote cha ujauzito.
Kutembelea kliniki kila mwezi au wiki kutokana na taratibu ulizowekewa na dakitari hutakiwa kufanyika kama kawaida, mwambie mhudumu wa afya kuhusu nini unataka kujua nini hata kama ni cha ujinga au hakina umuhimu eleza hisia zako
Kipindi cha tatu cha ujauzito
Miezi mitatu ya mwisho au trimester ya tatu inaweza kuwa kuwa na mabadiliko ya kimwili na kihisia laini mama anaweza kupata dalili za maumivu nyuma ya mgongo, kuvimba miguu na kupata huzuni inayoongezeka
Wakati huu, mtoto atafungua macho na kuongezeka uzito pia. Ukuaji au uongezekaji wa haraka wa uzito unaweza kuambatana na mtoto kuongeza kucheza tumboni na unapoanza wiki ya 39 za ujauzito , mtoto huwa ameshakuwa katika kiwango cha mwisho
Kipindi cha tatu cha ujauzito utatakiwa kukutana na wataalamu wa afya au kliniki kama ilivyo ratiba uliyopewa na tarehe za matarajio za kujifungua zinapokaribia jaribu kuuliza maswali mengi kwa mtaalamu wa afya. Mtaalamu wa afya utaweza kupimwa shingo ya kizazi na mlalo wa mtoto.
Kujua kuhusu kipindi hiki cha miezi mitatu ya mwisho kunaweza kukusaidia wakati wa mwisho wa kujifungua.
Bofya kusoma makala zingine zaidi kuhusu;
Huduma za kliniki wakati wa ujauzito
Namna ya Kujua tarehe ya kujifungua
ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kufanya maamuzi yanayohusisha afya yako
Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kutumia namba za simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
19 Desemba 2021, 11:34:39
Rejea za dawa