Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD
Mhariri:
Dkt. Sospeter B, MD
16 Novemba 2021 17:51:37
Mambo muhimu kufahamu kuhusi kichanga
Ni muhimu kwa mzazi na ndugu wanaomhudumia mzazi kufahamu mambo muhimu kuhusu kichanga. Mambo haya yatasaidia kuimarisha afya ya mama na mtoto na kuzuia madhara yanayiweza kutokea kwa mtoto.
Mambo muhimu kufahamu kuhusu kichanga aliyezaliwa mpaka anapofikisha miezi sita ni;
Anapaswa kufunikwa vizuri ili asipatwe na baridi
Anapaswa kunyonyeshwa mara tu baada ya kuzaliwa
Anapaswa kunnyonya maziwa ya mama tu mfululizo kwa muda wa miezi sita ya baada ya kuzaliwa
Mlezi au mzazi anapaswa kutambua viashiria vya hatari kwa vichanga
Mzazi au mlezi anapaswa kuzingatia usafi na kinga dhidi ya maradhi (maradhi ya kuambukiza)
Anapaswa kupata chanjo kwa mujibu wa Mwongozo ya Taifa
Mtoto njiti na waliozaliwa na uzito kidogo wanapaswa kupatiwa matunzo maalumu ikiwemo ya kangaruu
Watoto waliozaliwa na mama mwenye maambuziki ya VVU anapaswa kupata matunzo maalumu
Kumbuka
Makala hii pia imejibu maswali ya
Matunzo maalumu anayopaswa kupata kichanga
Matunzo maalumu anayopaswa kupata mtoto chini ya miezi sita
ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kufanya maamuzi yanayohusisha afya yako
Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kutumia namba za simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
16 Novemba 2021 17:51:37
Rejea za dawa
Postnatal care of the mother and newborn katika kitabu cha Counselling for Maternal and Newborn Health Care: A Handbook for Building Skills. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK304190/pdf/Bookshelf_NBK304190.pdf. Imechukuliwa 16.11.2021