top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Benjamin L, MD

19 Machi 2025, 12:39:55

Image-empty-state.png

Siku za kupata mimba

Imeboreshwa:


Siku za kupata mimba ni siku ambazo mwanamke ana uwezekano mkubwa wa kushika mimba akishiriki ngono. Siku hizi zinapatikana wakati wa uovuleshaji (upevushaji wa yai), ambapo yai hutolewa kutoka kwenye ovari na kuwa tayari kurutubishwa na mbegu za kiume.


Jinsi ya Kujua siku za Kupata mimba


Mzunguko wa hedhi kwa wanawake wengi huwa kati ya siku 28 hadi 30, lakini unaweza kuwa mfupi au mrefu kwa wanawake wengine. Uovuleshaji kwa kawaida hutokea siku 14 kabla ya hedhi inayofuata.


Mfano wa mzunguko wa siku 28:

  • Siku ya 1-5: Hedhi (siku za damu kutoka).

  • Siku ya 6-10: Mwili hujiandaa kwa uovuleshaji.

  • Siku ya 11-17: Siku za hatari za kushika mimba (uovuleshaji hutokea ndani ya siku ya 12 hadi 16 ya mzunguko wa hedhi).

  • Siku ya 18-28: Kipindi cha baada ya uovuleshaji hadi siku ya kuanza hedhi inayofuata.


Siku ya uovuleshaji

Uovuleshaji ni kawaida hutokea siku 14 kabla ya hedhi inayofuata. Hii inamaanisha kuwa kwa mzunguko wa hedhi wa urefu tofauti, uovuleshaji utatokea pia katika siku tofauti kama inavyoonekana kwenye jedwali namba 1:


Jedwali namba 1: Siku za mzunguko wa hedhi, Uovuleshaji na siku za kushika mimba kwa mwanamke mwenye mzunguko wa hedhi wa siku tofauti

Siku za mzunguko wa Hedhi

Siku ya uovuleshaji

Siku za kupata mimba

28

Siku ya 14

Siku ya 10 - 16

29

Siku ya 15

Siku ya 11 - 17

30

Siku ya 16

Siku ya 12 - 18

31

Siku ya 17

Siku ya 13 - 19

32

Siku ya 18

Siku ya 14 - 20

33

Siku ya 19

Siku ya 15 - 21

34

Siku ya 20

Siku ya 16 - 22

35

Siku ya 21

Siku ya 17 - 23

36

Siku ya 22

Siku ya 18 - 24

37

Siku ya 23

Siku ya 19 - 25

38

Siku ya 24

Siku ya 20 - 26

39

Siku ya 25

Siku ya 21 - 27

40

Siku ya 26

Siku ya 22 - 28

41

Siku ya 27

Siku ya 23 - 29

42

Siku ya 28

Siku ya 24 - 30

43

Siku ya 29

Siku ya 25 - 31

44

Siku ya 30

Siku ya 26 - 32

45

Siku ya 31

Siku ya 27 - 33

Jinsi ya kujua siku za kupata mimba

Njia zifuatazo zitakusaidia kufahamu siku yako ya kushika mimba;

  • Fuatilia mzunguko wako wa hedhi ili kujua wastani wa siku zako.

  • Tumia kipimo njiti cha uovuleshaji ili kujua wakati wa ovulation kwa uhakika zaidi.

  • Angalia dalili za upvuleshaji kama ute wa uke unaovutika, ongezeko la joto la mwili, na maumivu madogo ya tumbo upande mmoja.


Dalili ya siku za kupata mimba

Zifuatazo ni dalili za siku ya kushika mimba;

  • Kuongezeka kwa ute wa uke wenye muundo wa ute wa yai.

  • Maumivu madogo ya tumbo upande mmoja.

  • Kuongezeka kwa joto la mwili kwa kiasi kidogo.

  • Kuongezeka kwa hamu ya tendo la ndoa.


Njia za kuongeza uwezekano wa kupata mimba

Njia zifuatazo zinaongeza hatari ya kushika mimba;

  • Kufanya tendo la ndoa ndani ya siku za hatari kulingana na siku za mzunguko wako wa hedhi(angalia jedwali hapo juu)

  • Kupima tarehe ya uovuleshaji kwa kutumia kipimo uovuleshaji

  • Kudumisha afya bora kwa kula lishe yenye madini ya chuma, folic acid, na vitamini.

  • Kuepuka msongo wa mawazo na kufanya mazoezi kwa kiasi.


Hitimisho

Ikiwa una mzunguko usio wa kawaida au unapata ugumu wa kushika mimba, ni vyema kushauriana na daktari kwa ushauri zaidi.

ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kufanya maamuzi yanayohusisha afya yako
Wasiliana na daktari wa  ULY Clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kutumia namba za simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeandikwa:

19 Machi 2025, 12:32:05

Rejea za dawa

  1. Wilcox AJ, et al. Timing of sexual intercourse in relation to ovulation: effects on the probability of conception, survival of the pregnancy and sex of the baby. N Engl J Med. 1995;333:517–521. doi: 10.1056/NEJM199512073332301.

  2. Wilcox AJ, et al. Post-ovulatory ageing of the human oocyte and embryo failure. Hum Reprod. 1998;13:394–397. doi: 10.1093/humrep/13.2.394.

  3. Dunson DB, et al. Day-specific probabilities of clinical pregnancy based on two studies with imperfect measures of ovulation. Hum Reprod. 1999;14:1835–1839. doi: 10.1093/humrep/14.7.1835.

  4. Wilcox AJ,  et al. Incidence of early loss of pregnancy. N Engl J Med. 1988;319:189–194. doi: 10.1056/NEJM198807283190401.

  5. Wilcox AJ, et al. Measuring early pregnancy loss: laboratory and field methods. Fertil Steril. 1985;44:366–374. 

  6. Royston JP. Basal body temperature, ovulation and the risk of conception with special reference to the lifetimes of sperm and egg. Biometrics. 1982;38:397–406.

  7. Baird DD, et al. Using the ratio of urinary estrogen and progesterone metabolites to estimate day of ovulation. Stat Med. 1991;10:255–266. doi: 10.1002/sim.4780100209.

bottom of page