top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Mangwella S, MD

15 Novemba 2021 19:14:59

Image-empty-state.png

Umuhimu wa mjamzito kuhudhuria kliniki

Kuhudhuria kliniki mapema kabisa kabla au baada ya kupata ujauzito huwa na faida zifuatazo kwa mama na mtoto;


Kuboresha afya ya mama mjamzito


Afya ya mjamzito itaboreka kwa;

 • Kupata elimu kuhusu masuala ya afya

 • Kupata unasihi kuhusu lishe bora

 • Kupata unasihi na kupima VVU

 • Kufahamishwa umuhimu wa kujikinga dhidi ya magonjwa kama vile malaria, minyoo, magonjwa ya ngono na VVU

 • Kupata ushauri kuhusu njia za uzazi wa mpango baada ya kujifungua


Mjamzito kupatiwa dawa na chanjo muhimu


Dawa zinazotolewa wakati wa ujauzito zinazotumika kukinga na kuponya maradhi mbalimbali ni;


Vidonge vya kuongeza damu ili kujikinga dhidi ya upungufu wa damu

Chanjo ya pepopunda kama ni muda muafaka

Vidonge vya folic acid

Vidonge za kujikinga na malaria kwa wamama wanaoishi kwenye maeneo yenye malaria


Kujifungua salama


Mama atakapohudhuria klinini ataongeza uwezekano w akujifungua salama kwa;

 • Kufundwa kutengeneza mpango binafsi wa maandalizi ya kujifungua na kuhimizwa kuhusu kujifungua katika kituo cha kutolea huduma za afya

 • Kugundua mapema viashiria vya hatari kama vile kisukari, shinikizo la juula damu na kifua kikuu

 • Kufahamu umuhimu wa kutoa taarifa mapema ya magonjwa, kwa kuwa magonjwa haya yanaweza kuathiri ujauzito

 • Kutambua dalili za hatari na kupata huduma za afya mapema

 • Kutambua umuhimu wa kuwashirikisha akinababa katika huduma ya mama, mtoto mchanga na mtoto chini ya miaka mitano


Nani afanye maamuzi ya mjamzito kuhudhuria kliniki?


Mwenzi wa kiume na mama mjamzito wanapaswa kufanya maamuzi kwa kushirikiana kuhusu wapi na lini mama mjamzito atakwenda kupata huduma.


Mjamzito anapaswa kuhusika kufanya maamuzi mapema kuhusu wapi anapenda akapate huduma za afya mara tu anapoona inahitajika ili kupunguza madhara ya ujauzito kwake na mtoto.

ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kufanya maamuzi yanayohusisha afya yako
Wasiliana na daktari wa  ULY Clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kutumia namba za simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

15 Novemba 2021 19:26:08

Rejea za dawa


 1. World Health Organization (2010) IMPAC Integrated Management of Pregnancy and Childbirth WHO Recommended Interventions for Improving Maternal and Newborn Health. Geneva: World Health Organization.

 2. Campbell OMR, et al. Strategies for reducing maternal mortality: getting on with what works. The Lancet 368: 1284–1299.

 3. Carroli G, et al. (2001) WHO systematic review of randomised controlled trials of routine antenatal care. The Lancet 357: 1565–1570.

 4. World Health Organization (2011) WHO statement on antenatal care. Geneva: World Health Organization.

bottom of page