Mwandishi:
Dkt. Mangwella S, MD
Mhariri:
Dkt. Peter C, MD
22 Novemba 2021, 19:37:50

Wiki ya 10 ya ujauzito
Nini kinatokea mwilini mwako?
Kijusi hukua kutoka kwenye ukubwa wa mbegu ya mbaazi hadi ukubwa wa zabibu.

Mazoezi ni muhimu wakati huu kwa kuwa yatasaidia kuuandaa mwili wako na msongo, kubeba uzito wa ziada pamoja na uchungu. Hata hivyo pia yatasaidia kupunguza maumivu ya mgongo wakati wa ujauzito na kufanya mwili wako urejee kwenye hali ya kawaida baada ya kujifungua.
Unaweza kufanya mazoezi ya kutembea au mengine unayoweza kwa miezi tisa yote. Unapaswa kuwasiliana na daktari kuhusu mazoezi gani yanakufaa wiki kwa wiki katika ujauzito.
Nini kinatokea kwa mtoto?
Wiki hii hutia alama ya kuanza kipindi cha ukuaji wa mtoto na wakati huu viungo mbalimbali vya mtoto hukua haraka.
Kipindi hiki mapigo ya moyo ya mtoto yanaweza kutambuliwa kwa kifaa maalumu kinachowekwa kwenye ukuta wa tumbo kinachoitwa Doppler stethoscope. Mtaalamu wa afya anaweza kukusikilizisha mapigo ya mwanao utakapotembelea kliniki
Mtoto hupata uwezo wa kunywa maji yaliyo ndani ya chupa ya uzazi na pia huweza kujikunja na kunyoosha miguu yake.
Viungo mbalimbali vya mtoto huanza kufanya kazi vema na kwa kujitegemea.
Mwonekano wa nje wa uti wamgongo huonekana na pia mishipa ya fahamu ya uti wa mgongo hukua kutoka kwenye uti wa mgongo.
Majina mengine
Majina mengine yanayoendana na mada hii ni:
Ujauzito wa wiki 10
Mimba ya wiki 10
Wiki 10 za mimba
Kijusi cha wiki 10
Mwonekano wa ujauzito wa wiki 10
ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kufanya maamuzi yanayohusisha afya yako
Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kutumia namba za simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
12 Julai 2022, 10:19:46
Rejea za dawa
American Society for Reproductive Medicine; American College of Obstetricians and Gynecologists' Committee on Gynecologic Practice. Prepregnancy counseling: Committee Opinion No. 762. Fertil Steril. 2019 Jan;111(1):32-42. [PubMed]
Berglund A, et al. Preconception health and care (PHC)-a strategy for improved maternal and child health. Ups J Med Sci. 2016 Nov;121(4):216-221. [PMC free article] [PubMed]
Annadurai K, et al. Preconception care: A pragmatic approach for planned pregnancy. J Res Med Sci. 2017;22:26. [PMC free article] [PubMed]
McClatchey T, et al. Missed opportunities: unidentified genetic risk factors in prenatal care. Prenat Diagn. 2018 Jan;38(1):75-79. [PubMed]
Ko SC, et al. Estimated Annual Perinatal Hepatitis B Virus Infections in the United States, 2000-2009. J Pediatric Infect Dis Soc. 2016 Jun;5(2):114-21. [PubMed]
Tohme RA, et al. Hepatitis B virus infection among pregnant women in Haiti: A cross-sectional serosurvey. J Clin Virol. 2016 Mar;76:66-71. [PMC free article] [PubMed]
Kagan KO, et al. Principles of first trimester screening in the age of non-invasive prenatal diagnosis: screening for chromosomal abnormalities. Arch Gynecol Obstet. 2017 Oct;296(4):645-651. [PubMed]
Bhavadharini B, et al. Screening and diagnosis of gestational diabetes mellitus - relevance to low and middle income countries. Clin Diabetes Endocrinol. 2016;2:13. [PMC free article] [PubMed]
ACOG Practice Bulletin No. 190 Summary: Gestational Diabetes Mellitus. Obstet Gynecol. 2018 Feb;131(2):406-408. [PubMed]
Rule T, et al. Introducing a new collaborative prenatal clinic model. Int J Gynaecol Obstet. 2019 Mar;144(3):248-251. [PubMed]