top of page
Faida za kiafya za mbegu ya boga
Faida za kiafya za mbegu ya boga

Faida za kiafya za mbegu ya boga

Kuna vitu ambavyo umekuwa ukividharau au kuona havifai kabisa unapokuwa unakula vyakula aina fulani haswa ikija kwenye ulaji wa mbegu au maganda ya matunda kama zabibu, maboga n.k. Kusoma makala hii itakusaidia kufahamu kiundani kuhusu faida za kiafya za mbegu za maboga na namna ya kutumia mbegu hizo ili kupata faida zake.

Mbegu za boga huwa na virutubisho gani ndani yake?

Mbegu za boga huwa na virutubisho vifuatavyo na muhimu sana kwa binadamu;

• Nishati
• Nyuzinyuzi
• Protini
• Mafuta ya omega 6
• Vitamin K
• Madini Phosphorous
• Madini Manganese
• Madini shaba
• Madini zinki
• Madini chuma
• Maini magnesium
• Madini potassium
• Vitamin B2
• Madini folate
• Na kemikali zingine kama lignans, tryptophan

Kila gramu 28 za mbegu za boga kwa kawaida nishati ya kalori 151

Faida kwenye afya ya tezi dume

Huimarisha afya ya tezi dume kutokana na kuwa na virutubisho muhimu

Faida za kupunguza hatari ya kupata saratani

Kwa sababu ya kuwa na vitamin kwa wingi na kemikali ya lignans ambazo hufanya kazi kama viua sumu kupunguza sumu mwilini, tafiti zinaonyesha mbegu za boga huwa na uwezo wa kutibu na kukukinga dhidi ya saratani zufuatazo endapo zitatumiwa kwa muda mrefu.

• Saratani ya titi kwa wanawake walio kwenye komahedhi

Faida za kupunguza magonjwa ya moyo

Kwa sababu mbezu za boga huwa na kiwango kizuri cha nyuzinyuzi na mafuta ya omega-6, mafuta haya huwa na tabia ya kupunguza kiwango cha rehamu (kolestro) mbaya inayoitwa kwa jina la Low density lipoprotein (LDL) na kuongeza rehamu nzuri yenye jina la High density lipoprotein (HDL). Kwa kufanya hivyo endapo utatumia mbegu hizi kwa muda mrefu utapunguza hatari ya kupata magonjwa yafuatayo yanayosababishwa na kiwango kikubwa cha kolestro kwenye damu;

• Kiharusi(stroke)
• Magonjwa ya mshituko wa moyo
• Magonjwa mengine ya moyo
• Shinikizo la damu la juu(presha)

Tafiti zinaonyesha pia matumizi ya mbegu hizi hupunguza shinikizo la damu la diastolic kwa zaidi ya asilimia 7 na kuongeza kiwango cha kolestro nzuri yaani HDL mara 12 zaidi ndani ya wiki 12 za matumizi.

Faida ya kupunguza kiwango cha sukari kwenye damu

Tafiti zinaonyesha kutumia mbegu za boga na mazao yake pia huweza kupunguza kwa kiasi kikubwa kiwango cha sukari kwenye damu haswa kwa wagonjwa wa kisukari kwa sababu ya kuwa na kiwango kikubwa cha nyuzinyuzi na madini ya magnesium. Tafiti zinahitajika kaizi kugundua ni kwanini mbegu hizi zinauwezo huo mkubwa.

Faida ya Kuimarisha mfumo wa chakula

Kwa kuwa na kiwango cha nyuzinyuzi za kutosha, mbegu za boga huimarisha mfumo wa umeng’enyaji wa chakula kwa kuupa nyuzinyuzi zinazosaidia katika shughuli za kumeng’enya na kutoa nje haraka chakula ambacho hakijafyonzwa.

Faida ya kuongeza kiwango cha shahawa

Kwa sababu huwa na madini ya zinki kwa wingi, mbegu hizi huongeza kiwango cha uzalishaji wa shahawa. Kula mbegu hizi kila siku kutakufanya uwe na uwezo wa kuwa na mbegu nyingi na kuondokana na matatizo ya uzazi.

Tafiti zinaonyesha pia zinki hupunguza uharibiifu wa shahawa kutokana na dawa za chemotherapy na magonjwa ya autoimmune mwilini

Kwa kuwa na kiwango kizuri pia cha viuasumu husaidia kufanya kiwango cha homoni testosterone kuwa kizuri kwenye damu na hivyo kuchangia afya njema kwa mwanaume

Faida ya kukufanya upate usingizi

Kwa kuwa na kiwango kizuri cha amino acid iitwayo tryptophan, kula gramu 200 za mbegu za boga husaidi kuleta usingizi kwa watu ambao wana matatizo ya usingizi.

Hata hivyo madini zinki yaliyo kwenye mbegu ya boga huwez akuchochea uzalishaji wa homoni ya serotonin inayokusababisha utulie na upate usingizi mnono pia.

Kiwango cha magnesium kilicho kwenye mbegu hizi pia husaidia kuleta usingizi kwa watu wenye kiwango kidogo cha madini haya.

Faida zingine

Mbegu hizi zina faida zingine zaidi kama kuongeza kinga za mwili, kuongeza nguvu mwilini na zingine zaidi ambazo zitaendelea kuorodheshwa katika makala hii.

Namna ya kutumia mbegu hizi za boga ili kupata faida zake

• Unaweza kuandaa chakula kwa kutumia mafuta ya mbegu hizi mfano unapotumia mrenda mkavu twanga kwa kutumia mbegu hizi mpaka ulainike kasha pika na furahia mlo wako
• Kanga mbegu hizi na kuzila kama karanga, unaweza kula gramu 50 hadi 200 kwa siku
• Kamua mbegu kutengeneza mafuta kasha kupikia kwenye chakula n.k
• Tumia mbegu za maboga huku umechanganya na maziwa mgando kula kama kifungua kinywa asubuhi, naam unaweza utumia pia kama chakula chako cha mchana

ULY CLNIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa elimu na ushauri kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala hii

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu zilizo chini ya tovuti hii au bonyeza pata tiba.

Imeboreshwa,

29 Novemba 2020 11:36:52

Rejea za mada hii,

1. 11 Reasons Why You Should Eat Pumpkin Seeds. https://www.ecowatch.com/11-reasons-why-you-should-eat-pumpkin-seeds-1891177236.html. Imechukuliwa 25.11.2020
2. Aida Karina Zaineddin etal. The association between dietary lignans, phytoestrogen-rich foods, and fiber intake and postmenopausal breast cancer risk: a German case-control study. http://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/22591208. Imechuuliwa 25.11.2020
3. Dagmar Richter etal. Effects of phytoestrogen extracts isolated from pumpkin seeds on estradiol production and ER/PR expression in breast cancer and trophoblast tumor cells. http://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/23859042. Imechuuliwa 25.11.2020
4. M Gossell-Williams etal. Improvement in HDL cholesterol in postmenopausal women supplemented with pumpkin seed oil: pilot study. http://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/21545273. Imechuuliwa 25.11.2020
5. Ecowatch. 11 Reasons Why You Should Eat Pumpkin Seeds. http://ecowatch.com/2016/06/18/health-benefits-pumpkin-seeds/. Imechuuliwa 25.11.2020
6. Fu Caili etal. A review on pharmacological activit. http://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/16758316. Imechuuliwa 25.11.2020
7. Author links open overlay panelS.A.Elfiky etal. Protective effect of pumpkin seed oil against genotoxicity induced by azathioprine. http://www.sciencedirect.com/science/article/pii/S2090989612000422. Imechuuliwa 25.11.2020
8. Shona L. Halson. Sleep in Elite Athletes and Nutritional Interventions to Enhance Sleep. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC4008810/. Imechuuliwa 25.11.2020
9. Oral Mg(2+) supplementation reverses age-related neuroendocrine and sleep EEG changes in humanshttp://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/12163983. Imechuuliwa 25.11.2020

bottom of page