Dawa ambazo ni hatari kipindi cha ujauzito ni zipi?
Dawa zisizoruhusiwa kutumika kipindi cha ujauzito ni zipi?
Dawa zinazoleta ulemavu kwa kichanga ni zipi?
Dawa zinazoleta ulemavu kwa kijusi tumboni ni zipi?
Dawa hatari kwa mjamzito?
Dawa hatari kwa mama mjamzito ni zipi?
Dawa usizopaswa kutumia wakati wa ujauzito ni zipi?
top of page
To see this working, head to your live site.
Edited: Jun 23, 2021
Dawa sumu kwa kichanga
Dawa sumu kwa kichanga
1 answer0 replies
Like
Maoni (1)
bottom of page
Haya ni maswali mama yoyote ambaye anajali ujauzito wake anapaswa kujiuliza. Majibu yake yatakuwa marefu zaidi lakini mwisoni utapata linki ya kuendelea kusoma mambo mbalimbali kuhusu.
Makala hii itajibu kuhusu dawa ambazo ni sumu yaani ambazo hazitakiwi kutumika kabisa kwa mama mjamzito kwa jina jingine dawa teratojenia.
Ni nini mama mjamzito unatakiwa fahamu kuhusu dawa?
Dawa zinaweza kuleta madhara hasi kwa kijusi au mtoto kwenye kipindi chochote kabla au baada ya kupata ujauzito na baada ya mtoto kuzaliwa. Ni muhimu kuweka akilini kuwa kutumia dawa kwenye umri wa uzazi kwa mwanaume au mwanamke inaweza kuambatana na madhara kwa mtoto.
Wakati wa kipindi cha kwanza cha ujauzito
Katika kipindi cha kwanza cha ujauzito kipindi cha wiki kumi na mbili za mwanzoni mwa ujauzito, ni kipindi ambacho uumbaji wa viungo mbalimbali vya mtoto unatokea. Dawa zinaweza kusababisha madhaifu ya kiuumbaji, mfano kukosewa kwa uumbaji wa ubongo, moyo, mishipa ya damu, mifupa n.k huweza tokea ikitegemea aina na dozi ya dawa uliyotumia.
Maelezo zaidi kuhusu kipindi cha tatu na mengine ingia kwenye linki hii
Sasa turudi kwenye swali letu
Dawa sumu kwenye ujauzito ni zipi?
Baadhi ya dawa ambazo ni sumu kwa kijusi na mama mjamzito
Dawa zifuatazo ni sumu kwa mama na kichanga na hazipaswi kutumika wakati wa ujauzito;
Aminopterin
Androgens
Carbamazepine
Carbimazole
Chloramphenicol
Coumarins kama warfarin
Danazol
Dawa jamii ya ACE
Dawa jamii ya Fluoroquinolones
Dethylstilbestrol
Dozi kubwa ya vitamin A
Etretine
Fluconazole
Iodine
Isotretinoin
Lithium
Methimazole
Methimazole (MMI)
Methotrexate
Phenobarbital
Phenytoin
Phenytoin
Pombe
Propylthiouracil (PTU)
Tetracycline
Tetracyclines
Trimethadione
Valproate
Dawa sumu kwenye ujauzito inamanisha nini?
Dawa sumu kwenye ujauzito zinatumika kumaanisha dawa ambazo ni teratojenia yaani dawa zenye uwezo wa kuleta madhaifu katika uumbaji wa kichanga na hivyo kumletea madhaifu ya kimaumbile na pia kumsababishia saratani au matatizo mengine ya kiuumbaji wakati anazaliwa au wakati anaendelea kukua. Dawa hizi zimethibitishwa na tafiti nyingi kuwa ni teratojenia
Kusoma kuhusu dawa zingine ingia kwenye makala kupitia linki zifuatazo;
Rejea za mada hii
Eleni S. Tsamantioti, et al. Teratogenic Medications. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK553086/. Imechukuliwa 23.06.2021
Drugs in pregnancy. www.uktis.org. Imechukuliwa 23.06.2021
BNF 2018-2019, prescribing drugs in pregnancy
@ulyclinic. Madhara ya dawa kipindi cha ujauzito. https://www.ulyclinic.com/madhara-ya-dawa-kwa-mjamzito-na-mto. Imechukuliwa 23.06.2021
@ulyclinic. Dawa salama kipindi cha ujauzito. https://www.ulyclinic.com/dawa-salama-kipindi-cha-ujauzito. Imechukuliwa 23.06.2021
Better Health Channel. Drugs, medication and birth defects. https://www.betterhealth.vic.gov.au/health/ConditionsAndTreatments/drugs-medication-and-birth-defects. Imechukuliwa 23.06.2021
Thalidomide Teratogenic Effects Linked to Degradation of SALL4: After 60 years, researchers have now shed light on the mechanism underlying thalidomide's devastating teratogenic effects. Am J Med Genet A. 2018 Dec;176(12):2538-2539.
Kennedy MLH. Medication management of bipolar disorder during the reproductive years. Ment Health Clin. 2017 Nov;7(6):255-261.
Ornoy A. Neuroteratogens in man: an overview with special emphasis on the teratogenicity of antiepileptic drugs in pregnancy. Reprod Toxicol. 2006 Aug;22(2):214-26.
Mantovani A, et al. Delayed developmental effects following prenatal exposure to drugs. Curr Pharm Des. 2001 Jun;7(9):859-80.
Kennedy D, et al. Valproic acid use in psychiatry: issues in treating women of reproductive age. J Psychiatry Neurosci. 1998 Sep;23(4):223-8.
Ornoy A. Valproic acid in pregnancy: how much are we endangering the embryo and fetus? Reprod Toxicol. 2009 Jul;28(1):1-10.
Nie Q, Su B, et al. Neurological teratogenic effects of antiepileptic drugs during pregnancy. Exp Ther Med. 2016 Oct;12(4):2400-2404.
Katarina Dathe, et al. The Use of Medication in Pregnancy. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC6935972/. Imechukuliwa 23.06.2021