top of page
Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:

Dkt. Glory, MD

ULY CLINIC

8 Juni 2025, 06:58:16

Damu au kinyama mimba ya mwezi mmoja ikiharibika (1).jpg

Siku za ovulation ni ngapi?

Ovulation ni kitendo cha yai kutoka kwenye ovari na kuwa tayari kwa safari ya kuelekea kwenye mji wa mimba kupitia mrija wa uzazi wa falopia. Wakati huu endapo kuna mbegu ya kiume ilizoingia au itaingia ndani ya via vya uzazi, yai litarutubishwa na kuanza safari ya ujauzito. Kwa kawaida, ovulation hutokea siku 14 kabla ya hedhi inayofuata kwa mzunguko wa hedhi wa siku 28.


ree

Siku gani ovulation hutokea?

Siku ya kutokea kwa ovulation hutegemea idadi ya siku za mzunguko wako wa hedhi, mfano wa siku ya ovulesheni kwa mzunguko wa hedhi ni;

  • Mzunguko wa siku 21: Ovulation ni siku ya 7

  • Mzunguko wa siku 22: Ovulation ni siku ya 8

  • Mzunguko wa siku 23: Ovulation ni siku ya 9

  • Mzunguko wa siku 24: Ovulation ni siku ya 10

  • Mzunguko wa siku 25: Ovulation ni siku ya 11

  • Mzunguko wa siku 26: Ovulation ni siku ya 12

  • Mzunguko wa siku 27: Ovulation ni siku ya 13

  • Mzunguko wa siku 28: Ovulation ni siku ya 14

  • Mzunguko wa siku 29: Ovulation ni siku ya 15

  • Mzunguko wa siku 30: Ovulation ni siku ya 16

  • Mzunguko wa siku 31: Ovulation ni siku ya 17

  • Mzunguko wa siku 32: Ovulation ni siku ya 18

  • Mzunguko wa siku 33: Ovulation ni siku ya 19

  • Mzunguko wa siku 34: Ovulation ni siku ya 20

  • Mzunguko wa siku 35: Ovulation ni siku ya 21


Ovulation huchukua siku ngapi?

Ovulation yenyewe huchukua masaa 12-24


Yai huishi siku ngapi baada ya ovulation?

Baada ya ovulation yai lililotolewa linaweza kuishi hadi siku moja yaani masaa 24 tu baada ya kutolewa. Kama mbegu za kiume zitaingia katika masaa haya uchavushaji utatokea. Hata hivyo ikiwa mbegu zimeingia kwenye kizazi hata siku tano kabla, zikikutana na ovulesheni mimba inaweza kutungwa siku hiyo kwa kuwa huweza kuishi kwa wastani wa siku 5 ndani ya kizazi.


Jinsi ya kutambua siku ya ovulation

Ili kufahamu siku yako ya ovulation, unapaswa kufanya mambo yafuatayo;

  • Hesabu siku za mzunguko wako wa hedhi ili kufahamu una wastani wa siku ngapi

  • Chunguza mabadiliko ya ute wako ukeni ambao hubadilika kuwa wa maji ya yai na kuvutika wakati huu

  • Chunguza joto la mwili, endapo linaongezeka zaidi ni dalili mojawapo ya kuwa kwenye siku hiyo.

  • Chunguza uwepo wa maumivu kidogo ya tumbo upande mmoja wa nyonga, inaweza kumaanisha yai linatolewa kwenye ovari ya upande huo katika siku hii.


Hitimisho

Endapo unataka kushika mimba, unapaswa kuzingatia siku ya ovulation na kama unapata mzunguko usio wa kawaida tumia kipimo cha ovulation ili kutambua siku hiyo kwa uhakika.


Rejea za mada hii

  1. Richards JS, et al. Molecular mechanisms of ovulation and luteinization. Mol Cell Endocrinol. 1998 Oct 25;145(1-2):47-54.

  2. Kara E, et al. Modulation of Gonadotropins Activity by Antibodies. Front Endocrinol (Lausanne). 2019;10:15.

  3. Laven JSE. Follicle Stimulating Hormone Receptor (FSHR) Polymorphisms and Polycystic Ovary Syndrome (PCOS). Front Endocrinol (Lausanne). 2019;10:23.

  4. Gilbert RO. Symposium review: Mechanisms of disruption of fertility by infectious diseases of the reproductive tract. J Dairy Sci. 2019 Apr;102(4):3754-3765.

  5. Tsutsumi R, Webster NJ. GnRH pulsatility, the pituitary response and reproductive dysfunction. Endocr J. 2009;56(6):729-37.

  6. Kumar P, Sait SF. Luteinizing hormone and its dilemma in ovulation induction. J Hum Reprod Sci. 2011 Jan;4(1):2-7.

  7. Toosy S, et al. Lean polycystic ovary syndrome (PCOS): an evidence-based practical approach. J Diabetes Metab Disord. 2018 Dec;17(2):277-285.

  8. Richards JS, Pangas SA. The ovary: basic biology and clinical implications. J Clin Invest. 2010 Apr;120(4):963-72.

  9. Fujisawa M, et al. Ovarian stromal cells as a source of cancer-associated fibroblasts in human epithelial ovarian cancer: A histopathological study. PLoS One. 2018;13(10):e0205494.

  10. Reed BG, Carr BR. The Normal Menstrual Cycle and the Control of Ovulation. In: Feingold KR, et al, editors. Endotext [Internet]. MDText.com, Inc.; South Dartmouth (MA): Aug 5, 2018.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

bottom of page