top of page
Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:

Dr.Sospeter Mangwella, MD

ULY CLINIC

4 Agosti 2025, 12:47:09

Damu au kinyama mimba ya mwezi mmoja ikiharibika (1).jpg

Bronkaitiz kali

Bronkaitiz hutokana na michomo ya kinga za mwili kwenye njia ya hewa inayoamushwa na maambukizi ya virusi, mara nyingi hujitokeza baada ya kuugua mafua. Ugonjwa huu uweza kuisha wenyewe ndani ya siku 10 bila tiba. Wagonjwa wa bronkaitizi mara nyingi hukohoa makohozi mazito yanayoweza kuwa na rangi.

8

2

Daliliza bronkaitiz


  • Kikohozi kikavu au chenye makohozi ya njano,au kijani katika siku mbili au tatu

  • Kupumua kwa shida

  • Kifua kutoa mlio wa filimbi

  • Homa

  • Maumivu wakati wa kumeza

  • Kukauka kwa koo

  • Kutetemeka

  • Kuishiwa pumzi

  • Maumivu ya mwili


Wakati gani wa kumpigia daktari?


  • Kama dalili ya kikohozi na kupiga miruzi zikiendelea kwa zaidi ya wiki mbili

  • Makohozi yanatoka na damu, kujihisi uchovu homa endelevu na kuishiwa pumzi

  • Kushindwa kulala kwa sababu ya kukohoa

  • Kupanda kwa joto la mwili


Vihatarishi


  • Kuvuta sigara- 

  • Kinga ya chini ya mwili – haswa kwa watoto, watu wazima na wanaotumia dawa za kushusha kinga ya mwili

  • Kujianika kwenye vichokoza mapafu- kemikali za viwandani

  • Kucheua tindikali 


Matibabu


Mara nyingi matibabu ya dawa kwa mtu mwenye afya nzuri si muhimu kwa sababu mwili unakinga ya kutosha kufanya ugonjwa huu kuisha wenyewe.


Endapo dawa zitahitajika zinahusisha;


  • Dawa ya kulainisha makohozi

  • Dawa ya kuzuia maumivu kama paracetamol, Diclopar na aspirin(isitumiwe na watoto)

  • Dawa za kuzuia kikohozi kama Codeine, Dextromethopan au Pholcodeine (Dawa hizi hutumika kuzuia kikohozi kikavu chenye kero kwa mgonjwa. Hivyo zisitumike kwa tiba ya kikohozi laini kwa sababu husababisha makohozi yenye vimelea vya maradhi kubakia kwenye njia ya hewa na hii ni hatari kwa wagonjwa wenye bronkiti sugu)


Matibabu ya nyumbani


  • Kunywa maji ya kutosha na epuka vitu vyenye pombe au kafeini

  • Pumzika vya kutosha ili uupatie mwili nafasi ya kujiponya

  • Ongeza unyevu kwenye hewa unayovuta au kwa kujifukiza


Madhara ya bronchaitiz kali


Mgonjwa mwenye Bronkiti kali anaweza kupata ambukizo la ziada kutokana na bakteria hivyo kupata nimonia ambapo dalili ya homa itaongezeka. Hii italazimu kutibiwa kwa kutumia dawa sahihi za kuua vimelea husika vya bakteria. Onana na daktari endapo una kikohozi pamoja na homa kwa ushauri na tiba


Kinga


  • Acha kuvuta sigara

  • Nawa mikono haswa kama kinga ya mwili iko chini

  • Pacha chanjo ya kirusi cha Influenza

  • Vaa barakoa maalumu ya kukukinga na sumu katika hew kama unafanya kazi viwandani kwenye gesi kali zinazochokoza koo


Rejea za mada hii;


  1. CDC. Acute bronchitis. https://www.cdc.gov/antibiotic-use/bronchitis.html. Imechukuliwa

  2. National Heart, Lung, and Blood Institute. What is bronchitis?. http://www.nhlbi.nih.gov/health/health-topics/topics/brnchi. Imechukuliwa 20.07.2021

  3. Goldman L, et al. Acute bronchitis and tracheitis. Goldman's Cecil Medicine. 25th ed. Philadelphia, Pa.: Saunders Elsevier; 2016. http://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 20.07.2021

  4. Stoller JK, et al. Management of infection in acute exacerbations of chronic obstructive pulmonary disease. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 20.07.2021

  5. Tintinalli's Emergency Medicine. Tintinalli JE, et al. Acute bronchitis and upper respiratory tract infections. A Comprehensive Study Guide. 8th ed. New York, N.Y.: The McGraw Hill Companies; 2016. http://accessmedicine.com. Imechukuliwa 20.07.2021

  6. Acute bronchitis. American Lung Association. http://www.lung.org/lung-health-and-diseases/lung-disease-lookup/acute-bronchitis/learn-about-acute-bronchitis.html. Imechukuliwa 20.07.2021

  7. Gautret P, et al. Travel-associated illness in older adults (>60 y). Journal of Travel Medicine. 2012;19:169.

  8. Centers for Disease Control and Prevention. Antibiotics aren't always the answer. https://www.cdc.gov/features/getsmart/. Imechukuliwa 20.07.2021

  9. Harris AM, et al. Appropriate antibiotic use for acute respiratory tract infection in adults: Advice for high-value care from the American College of Physicians and the Centers for Disease Control and Prevention. Annals of Internal Medicine. 201;164:425.

  10. Environmental Protection Agency. Use and care of home humidifiers. https://www.epa.gov/indoor-air-quality-iaq/indoor-air-facts-no-8-use-and-care-home-humidifiers. Imechukuliwa 20.07.2021

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

bottom of page