Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
Dr.Sospeter Mangwella, MD
ULY CLINIC
4 Agosti 2025, 12:38:56
Matapishi ya njano
Kutapika njano au kupta matapishi ya njano au rangi ya chungwa hutokea masaa machache baada ya kupata ugonjwa ugonjwa unaosababisha kichefuchefu na kutapika. Rangi ya matapishi inaweza kuendelea kuwa njano endapo mtu atakula kitu kila anapotapika, au kubadilika na kuwa na rangi ya kijani, au njano inayoelekea kijani endapo mtu hali chochote baada ya kutapika. Rangi ya njano hutokana na majimaji ya chakula kilichomeng’enywa, hupaswi kuwa na woga unapotapika matapishi ya njano.
Visababishi vya kutapika njano
Kutapika njano huweza kusababishwa na;
Kula sumu ya chakula- dalili zinazoweza ambatani ni pamoja na maumivu ya tumbo, kuharisha na homa
Mafua ya tumbo- husababishwa na maambukizi ya virusitumboni kutokana na kula chakula au maji. Dalili zingine ni homa, maumivu ya misuli na tumbo
Mafua ya influenza- haya ni maambukizi ya virusi kwenye mfumo wa juu wa upumuaji, huleta dalili za kuchuruzika mafua na koo chungu kisha kuendelea kuwa na homa, maumivu ya misuli, uchovu maumivu ya kichwa na kutetemeka
Kipanda uso- huambatana na maumivu makali ya kichwa yanayoweza kudumu kwa masaa machache au siku kadhaa. Hisia za kutapika huweza kutokea na mtu hutapika kwa kujirudia rudia endapo maumivu ya kichwa yanaendelea
Ujauzito- huleta dalili ya kutapika wakati wa asubuhi, hutokana na mabadiliko ya homoni kipindi cha ujauzito.
Homa ya kidole tumbo (Ugonjwa wa apendisaitis)
Homa ya mwendo
Matumizi ya dawa za kuua chembe zasaratani
Maambukizi sikio la kati
Matumizi ya dawa jamii fulani au tiba ya saratani
Wakati gani wa kuwa na hofu unapotapika njano?
Endapo unatapika njano inayoambatana na dalili zifuatazo unapaswa kutilia mashaka na kutafuta msaada wa daktari;
Kizunguzungu
Kupumua kwa shinda
Kutapika nyongo kwa muda mrefu
Kutapika zaidi ya masaa 48 bila kupata nafuu
Kutapika kila kitu
Maumivu makali ya tumbo nay a ghafla
Kuwa na kisukari
Maumivu makali ya kifua
Kutapika mara kwa mara katika mwaka
Damu kwenye matapishi au matapishi kuwa meusi au rangi ya unga wa kahawa
Maumivu makali ya kichwa na homa
Kuishiwa nguvu au kupata uchovu mkali
Kupata kizunguzungu au kuzimia
Huduma ya kwanza kwa mtu anayetapika sana;
Hatua ya muhimu kuchukua endapo unatapika sana ni kufika hospitali ili kupatiwa matibabu kwa kutundikiwa dripu, hii itasaidia rejesha kiwango cha madini na maji ulichopoteza.
Kama unatapika kwa kiasi na unaweza kunywa maji, fanya iwezekanavyo kunywa maji kiasi kidogo sana lakini mara kwa mara. Ukipata maji ya Oral au wengine huita ORS na hutumika kwa watoto wanaoharisha itasaidia kuwa kama huduma ya kwanza. Kengo ni kurejesha kiwango ulichopoteza kwa kutapika na kuzuia kupata shoku kutokana na kuishiwa maji mwilini.
Zuia kutumia vitu vinavyokuletea kichefuchefu kama vinywaji nyenye mafuta, sukari na viungo kwa wingi na vingine ambavyo vinaamsha kuchefuchefu chako.
Maswali yaliyoulizwa sana na majibu yake
Kwa nini matapishi yangu yamekuwa ya rangi ya njano?
Matapishi ya njano hutokea kwa sababu yanakuwa yamechanganyika na majimaji ya nyongo yanayotoka kwenye ini na kuhifadhiwa kwenye kibofu cha nyongo. Nyongo hii kawaida husaidia kumeng’enya mafuta kwenye utumbo.
Wakati mtu anatapika sana hadi tumbo linabaki tupu (hakuna chakula ndani), majimaji ya nyongo yanaweza kuanza kutoka tumboni na kusababisha rangi ya manjano kwenye matapishi. Hili ni jambo la kawaida, hasa:
Mtu anapotapika mara nyingi mfululizo
Asipokula kwa muda mrefu
Wakati wa kichefuchefu kinachosababishwa na ujauzito au maambukizi ya tumbo
Ikiwa hali hii inaendelea kwa muda mrefu au inahusisha maumivu makali ya tumbo, homa, au kizunguzungu, ni vizuri kumuona daktari.
Je, matapishi ya njano ni hatari?
Kwa ujumla sio, inaweza kutokea kwa sababu ya mlo au kichefuchefu; lakini inapotokea mara kwa mara au ikiwa inaambatana na dalili nyingine, ni muhimu kushauriana na daktari.
Ni sababu gani kuu zinazosababisha matapishi ya njano?
Sumu ya chakula
Mafua ya tumbo
Influenza
Ujauzito
Homa ya kidole tumbo (Apendisaitis)
Matumizi ya kemikali za saratani
Maambukizi ya sikio la kati
Dawa fulani
Lini ni wakati wa kuwa na wasiwasi na kutafuta huduma ya dharura?
Kutapika nyongo kwa muda mrefu
Kutapika zaidi ya masaa 48 bila nafuu
Maumivu makali ya tumbo ghafla
Damu kwenye matapishi au matapishi meusi/“kama unga wa kahawa”
Kupata kizunguzungu, uchovu mkali, au kuzimia
Ninachoweza kufanya kama ninatapika sana na kwa muda mrefu?
Tembelea hospitali kwa ajili ya dripu ya maji
Kunywa maji kidogo lakini mara kwa mara
Tumia maji ya orol (ORS) kwa ajili ya regeni ya madini na maji mwilini
Je, kuna vinywaji au vyakula ninavyopaswa kuepuka wakati wa kutapika?
Ni vinywaji vyenye mafuta mengi, sukari na viungo vingi ambavyo vinaweza kuongeza kichefuchefu.
Matapishi ya kijani ni tofauti na matapishi ya njano?
Ndiyo, kuna tofauti.Matapishi ya rangi ya kijani mara nyingi huonyesha uwepo wa nyongo iliyochanganyika na chakula au maji yaliyopo tumboni. Hali hii hutokea pindi mtu anapotapika mara kwa mara, au tumboni hakuna chakula kingine isipokuwa majimaji kutoka kwenye ini.
Kwa upande mwingine, matapishi ya njano mara nyingi huwa na kiasi kidogo cha nyongo na yanaweza kuonekana mwanzoni mwa kichefuchefu au kutapika kwa kawaida.
Ingawa mara nyingi matapishi ya kijani si hatari, yanaweza kuwa dalili ya shida kubwa ikiwa yanatokea mara kwa mara, yanaambatana na maumivu makali, au damu. Katika hali kama hizo, ni muhimu kumuona daktari.
Je, kwa nini matapishi yanakuwa ya kijani badala ya njano?
Matapishi ya rangi ya kijani hutokana na kuchanganyika kwa nyongo (bile) na chakula kilichotapika, hasa wakati mtu anakuwa amekula au kunywa kitu kinachosababisha mwitikio wa haraka tumboni kama vile sumu ya chakula, maambukizi, au kichefuchefu cha ghafla. Nyongo inaweza kutoka kwenye kibofu cha nyongo na kufika mapema tumboni kabla chakula hakijameng’enywa vizuri, na kutoa matapishi ya kijani.
Je, ujauzito unaweza kusababisha matapishi ya njano?
Ndiyo— “morning sickness” mara nyingi huambatana na kutapika na matapishi ya rangi ya njano
Je, ujauzito unaweza kusababisha matapishi ya njano?
Ndiyo— “morning sickness” mara nyingi huambatana na kutapika na matapishi ya rangi ya njano
Je, matapishi ya njano yanahitaji dawa maalum?
Si lazima – ni muhimu kwanza kurejeshwa maji na madini; lakini ikiwa matatizo yanaendelea au kuna dalili mbaya, tafuta msaada wa daktari kwa uchunguzi zaidi.
Rejea za mada hii
Vomiting in adults. https://www.nhsinform.scot/illnesses-and-conditions/stomach-liver-and-gastrointestinal-tract/vomiting-in-adults. Imechukuliwa 28.06.2021
Catiele Antunes, et al. Upper Gastrointestinal Bleeding. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK470300/#: Imechukuliwa 28.06.2021
I.Dodd Wilson. Chapter 85Hematemesis, Melena, and Hematochezia. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK411/. Imechukuliwa 28.06.2021
Amyloidosis. my.clevelandclinic.org/health/diseases/15718-amyloidosis. Imechukuliwa 28.06.2021
Cyclic vomiting syndrome. niddk.nih.gov/health-information/digestive-diseases/cyclic-vomiting-syndrome. Imechukuliwa 28.06.2021
Lamps LW, et al.Fungal infections of the gastrointestinal tract in the immunocompromised host: An update. DOI: 10.1097/PAP.0000000000000016. Imechukuliwa 28.06.2021
Mayo Clinic Staff. Acute liver failure. mayoclinic.org/diseases-conditions/acute-liver-failure/symptoms-causes/syc-20352863. Imechukuliwa 28.06.2021
Mayo Clinic Staff. Viral gastroenteritis (stomach flu). https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/viral-gastroenteritis/symptoms-causes/syc-20378847. Imechukuliwa 28.06.2021
Mayo Clinic Staff.Food poisoning. mayoclinic.org/diseases-conditions/food-poisoning/symptoms-causes/syc-20356230. Imechukuliwa 28.06.2021
Mayo Clinic Staff.Gastritis.mayoclinic.org/diseases-conditions/gastritis/symptoms-causes/syc-20355807. Imechukuliwa 28.06.2021
Mayo Clinic Staff.Gastroesophageal reflux disease (GERD). mayoclinic.org/diseases-conditions/gerd/symptoms-causes/syc-20361940. Imechukuliwa 28.06.2021
Mayo Clinic Staff.Intestinal obstruction. mayoclinic.org/diseases-conditions/intestinal-obstruction/symptoms-causes/syc-20351460. Imechukuliwa 28.06.2021
Mayo Clinic Staff.Nausea and vomiting. mayoclinic.org/symptoms/nausea/basics/definition/sym-20050736. Imechukuliwa 28.06.2021
Mayo Clinic Staff.Vomiting blood. mayoclinic.org/symptoms/vomiting-blood/basics/definition/sym-20050732
Nausea and vomiting in adults. nhs.uk/conditions/nausea-and-vomiting-in-adults/. Imechukuliwa 28.06.2021
Nausea and vomiting. my.clevelandclinic.org/health/symptoms/8106-nausea--vomiting. Imechukuliwa 28.06.2021
Vomit looks like coffee grounds after drinking alcohol. goaskalice.columbia.edu/answered-questions/vomit-looks-coffee-grounds-after-drinking-alcohol. Imechukuliwa 28.06.2021
Vomiting in adults. (2018). nhsinform.scot/illnesses-and-conditions/stomach-liver-and-gastrointestinal-tract/vomiting-in-adults. Imechukuliwa 28.06.2021
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
