Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
Dr.Sospeter Mangwella, MD
ULY CLINIC
4 Agosti 2025, 12:28:35
Ni nini husababisha maumivu ya jicho?
Maumivu ya jicho ni hali inayotokea pale ambapo kuna tatizo katika kuta za nje au ndani ya jicho. Maumivu haya yanaweza kueleweka kama hisia za jicho kuwaka, kuungua, au kuchoma choma. Hali hii mara nyingi hutokana na mchakato wa kuwaka kwa kemikali mwilini kutokana na kuwepo kwa kitu kigeni au majeraha kwenye jicho.
Sababu Zinaweza Kusababisha Maumivu ya Jicho
Aleji au mzio kwa vitu kama vumbi, vipodozi, au kemikali
Michomo kwenye kope au sehemu za jicho zinazozunguka
Kuziba kwa mrija wa machozi, hali inayosababisha macho kuwa makavu
Kuota kwa kifuko cha maji (chalazion) kwenye kope
Maumivu yanayotokana na kichwa, hasa migraines au matatizo ya sinus
Matumizi ya lensi za kupambazesha (contact lenses) bila usafi au kwa muda mrefu
Mikwaruzo kwenye kuta za konea (conjunctiva)
Macho kuwa makavu kutokana na upungufu wa machozi
Kuingia kwa vitu vya kigeni kwenye jicho kama vumbi, mchanga, au kemikali
Tatizo la glaucoma, ambalo ni ugonjwa unaosababisha shinikizo la juu ndani ya jicho
Majeraha kama kuumia au kujigonga jicho
Michomo au uvimbe kwenye sehemu nyeupe ya jicho (sclera) au kwenye konea (conjunctiva)
Michomo ya mshipa wa fahamu wa optic, ambayo inaweza kusababisha maumivu makali
Uvimbe mwekundu wenye maumivu karibu na kingo za kope
Kugeuza kope kwa njia isiyo ya kawaida (entropion au ectropion)
Ni Muhimu kufanya Nini?
Kama unapata maumivu ya jicho, ni muhimu usiache hali hiyo ipite peke yake. Tafuta msaada wa daktari kwa uchunguzi na matibabu sahihi.
Rejea za mada hii
American Academy of Ophthalmology. Red Eye. In: Basic and Clinical Science Course. San Francisco, CA: American Academy of Ophthalmology; 2023.
Kanski JJ, Bowling B. Clinical Ophthalmology: A Systematic Approach. 9th ed. Elsevier; 2019.
Azari AA, Barney NP. Conjunctivitis: A Systematic Review of Diagnosis and Treatment. JAMA. 2013;310(16):1721-1729. doi:10.1001/jama.2013.280318.
Wilhelmus KR. Ocular infections. In: Merck Manual Professional Version [Internet]. 2022 [cited 2025 Jun 18]. Available from: https://www.merckmanuals.com/professional/eye-disorders/infections-of-the-eye/ocular-infections
McGhee CNJ, Dean S. Glaucoma. In: Clinical Ophthalmology. BMJ Publishing Group; 2014.
Tabbara KF. Contact Lens Related Eye Infections. Saudi J Ophthalmol. 2014;28(1):30-36. doi:10.1016/j.sjopt.2013.07.004.
Dart JK, Stapleton F, Minassian D. Contact lenses and other risk factors in microbial keratitis. Lancet. 1991;338(8768):650-653.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
