top of page
Imeandikwa na Daktari wa ULY Clinic

Haipothairoidizimu

Haipothairoidizimu
Upungufu wa homoni ya thairoidi (haipothairoidizimu)

Haipothairoidizimu ni hali ya kutozalishwa kwa kiwango cha kutosha cha homoni ya thairoid. Homoni ya thaitoid hufanya kazi muhimu mwilini. Upungufu wa uzalishaji wa homoni hii huambatana na dalili mbalimbali mapema Zaidi wakati upungufu unatokea kama tatizo la obeziti, maumivu ya maungio ya mwili, ugumba na magonjwa ya moyo.

Vipimo vya kupima kiwango cha homoni pamoja na ufanyaji kazi wa tezi ya thairoid vinapatikana, matiabu pia ya kutumia homoni zilizozalishwa nje ya mwili pia yapo ili kupambana na tatizo hili.

Visababishi

Kisababishi kikuu cha upungufu wa homoni ya thairoidi ni ugonjwa wa autoimmune thairoidaitizi kwa jina jingine hashmoto’s thairoidaitizi). Tatizo hili hutokana na chembe za ulizi za mwili kushambulia tezi ya thairoidi.

Visababishi vingine vinaweza kuwa

Matibabu- kama vile upasuaji wa kuondoa sehemu au tezi ya yote ya thairoidi kama kwa wagonjwa wenye saratani, matibabu ya kutumia radioactive iodine- haya huharibu sana seli za thairoidi na kufanya uzalishaji upungue, uzalishaji hafifu wa homoni ya TSH kutokana na matatizo ya tezi ya pituitari.

Viashiria

Dalili na viashiria vya haipothairoidizimu hutegemea hatua za tatizo, viashiria huanza taratibu na kuongezeka jinsi muda miaka inavyokwenda.

Kwenye hatua za awali, unaweza usitambue dalili hizi kuwa zinahusiana na tatizo la haipothairoidizimu ambazo ni uchovu, na kuongezeka uzito, wakati mwingine unaweza kuzani kuwa zinatokana na kukua.

Kwa jinsi metabolizimu mwilini inavyopungua, dalili halizi huanza kutokea na kuonekana. Dalili hizi huwa ni;
• Uchovu
• Kuhisi baridi sana
• Konstipesheni
• Kukauka kwa Ngozi
• Kuvimba uso
• Kutoa sauti ya farasi
• Misuli kuwa dhaifu
• Kuongezeka kwa kiwango cha rehamu kwenye damu(kolesto)
• Maumivu ya misuli, kubana kwa misuli na maumivu endapo misuli inashikwa
• Maumivu kukakamaa na kuvimba kwa maungio ya mwili
• Kupata hedhi kali(kutokwana damu nyingi wakati wa hedhi kuliko kawaida)
• Nywele kuwa laini
• Kuwa mkorofi
• Kupoteza kumbukumbu
• Kupata hedhi isiyoeleweka
• Kupungua kwa hamu ya tendo (libido)
• Kupungua kwa mapigo ya moyo
• Dipresheni
• Matatizo ya kumbukumbu
• Kuvimba kwa tezi ya thairoidi endapo tatizo litadumu kwa muda mrefu

Dalili kwa Watoto wadogo na vichanga

Watoto wanaozaliwa na madhaifu ya uzalishwaji wa homoni ya thairoidi, kwa mara ya kwanza huwa wana dalili kiasi tu. Endapo mtoto hata pata tiba anaweza kupata matatizo makubwa ya ukuaji na mtindio wa ubongo. Dalili zinazotokea kwa vichanga huwa pamoja na;

• Manjano
• Ulimi kuwa mkubwa na uliotoka nje
• Kushindwa kupumua vema
• Kulia sauti ya falasi
• Henia kwenye kitovu
• Mtoto kushindwa kukua kwa kuwa wafupi
• Kuchelewa kuota meno ya kudumu
• Kuchelewa kubarehe
• Konstipesheni
• Misuli dhaifu
• Kulala sana
• Matatizo ya kiakili

Vipimo

Daktari mara baada ya kuchukua historia ya tatizo lako atakuandikiwa vipimo vya kupima upungufu huu wa homoni

Utaandikiwa kipimo cha kupima utendaji kazi wa tezi ya Thairoidi na uzalishaji wa kichochezi cha thairoidi (thairoid stimulating homoni)

Baadhi ya dawa huweza kupunguza ufanisi wa kipimo cha homoni kwa huathiri kiwango cha homoni ya thairoidi kwenye damu. Dawa hizi ni dawa za kuyeyusha damu(heparini) na Vitamini (Biotin), ni vema ukamfahamisha daktari wako mapema kama unatumia dawa hizi.

Matibabu

Matibabu yapo ya kurejesha kiwango cha homoni kwenye damu kwa kutumia vidonge vya homoni kama vile levothyroxine na zinginezo. Dawa hizi husaidia kuondoa dalili zilizojitokeza.

Dalili huanza kupotea mara matibabu yanapoanza, dawa hizi hupunguza kiwango cha kolestro kwenye damu na hivyo husababisha uzito pia kupungua. Utatumia dawa hizi Maisha mazima lakini dozi inaweza kubadilika. Daktari ataagiza kupima kipimo cha TSH baada ya wiki sita mpaka nane baada ya kuanza matibabu, kisha kipimo kitafanyika miezi sita baadaye. Mara baada ya kiwango kuwa saw ana kujulikana kwa dozi daktarin atakuwa akikupima kila mwaka kiwango cha homoni ya TSH.

Maudhi ya dawa ya levothyroxine

Dawa hii endapo dozi itakuwa kubwa kuliko kawaida huweza kuleta maudhi ya
• Kuongezeka wka hamu ya kula
• Kukosa usingizi
• Kuhisi mapigo ya moyo
• Kutetemeka
ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile dhidi ya afya yako
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba, piga namba za simu au bonyeza sehemu imeandikwa "pata Tiba" chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa mara ya mwisho
25 Machi 2020 16:15:29

Rejea za mada

1.Chaker L, et al. Hypothyroidism. The Lancet. 2017;390:1550.

2.Hypothyroidism. American Thyroid Association. https://www.thyroid.org/hypothyroidism/. Imechukuliwa 25.03.2020

3. Hypothyroidism. National Institute of Diabetes and Digestive and Kidney Diseases. https://www.niddk.nih.gov/health-information/endocrine-diseases/hypothyroidism. Imechukuliwa 25.03.2020

4.Jameson JL, et al., eds. Hypothyroidism. In: Harrison's Principles of Internal Medicine. 20th ed. New York, N.Y.: The McGraw-Hill Companies; 2018. https://accessmedicine.mhmedical.com. Imechukuliwa 25.03.2020

5.Ferri FF. Hypothyroidism. In: Ferri's Clinical Advisor 2019. Philadelphia, Pa.: Elsevier; 2019. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 25.03.2020

6.Hyperthyroidism. Merck Manual Professional Version. https://www.merckmanuals.com/professional/pediatrics/endocrine-disorders-in-children/hypothyroidism-in-infants-and-children. Imechukuliwa. 25.03.2020

7.ATA Hypothyroidism Web Booklet. American Thyroid Association Web site. Available at: http://thyroid.org/patients/brochures/Hypothyroidism%20_web_booklet.pdf. Imechukuliwa 24.05.2020

8.Skugor, M. The Underactive Thyroid: Hypothyroidism. In: The Cleveland Clinic Gide to Thyroid Disorders. New York: Kaplan Publishing; 2009:11-28.
bottom of page