Kichefuchefu na kutapika
Imeandaliwa na madaktari wa ULY-Clinic
​
Kichefuchefu na kutapika ni dalili inayoweza kusababishwa na mambo mengi sana. Kichefuchefu na kutapika mara nyingi husababishwa na maambukizi ya virusi katika mfumo wa chakula, mara nyingi imekosewa kwa kusemwa mafua ya tumbo au homa ya asubuh ya mwanzoni mwa ujauzito.
Madawa mengi pia yanaweza kusababisha kichefuchefu na kutapika, pamoja na madawa ya kaputi yanayotumika wakati wa upasuaji. Kwa mara chache sana dalili hizi zinamaanisha kuna tatizo kubwa ndani ya mwili linalotishia maisha.
​
Nini huweza husababisha kichefuchefu na kutapika?
Kichefuchefu na kutapika huweza kutokea kila kimoja kwa kujitegemea au kwa pamoja, mambo yanayosababisha kwa kiasi kikubwa ni kama;
-
Matumizi ya Madawa ya saratani
-
Kupooza kwa tumbo utumbo
-
Madawa ya kaputi
-
Kuziba kwa utumbo
-
Homa ya kutembea
-
Homa ya asubuhi
-
Kipanda uso
-
Maambukizi ya rotavirus
-
Maambukizi ya virusi kwenye tumbo
-
Matatizo katika mfumo wa fahamu wa sikio
Sababu zingine zinazoweza kuchangia ni kama vile;
-
Matatizo ya kunywa pombe
-
Tatizo la kujinyima chakula
-
Aleji/Mzio
-
Ugonjwa wa kidole tumbo(apendeksi)
-
Tatizo la kula kupita kiasi
-
Ugonjwa wa crohns
-
Kizunguzungu
-
Msongo wa mawazo
-
Maambukizi kwenye sikio
-
Kula chakula Chenye sumu
-
Kushikwa kwa moyo
-
Kufeli kwa moyo
-
Homa
-
Kiwango cha juu cha homoni ya tezi shingo
-
Kuvilia damu ndani ya kichwa
-
Maambukizi uti wa mgongo
-
Mzio wa maziwa kwa watoto
-
Homa ya kongosho
-
Homa ya pancrease
-
Vidonda vya tumbo
-
Kuziba kwa mrija wa kutolea chakula nje ya kifuko cha chakula
-
Matibabu ya mionzi
-
Maumivu makali
-
Jeraha katika kichwa
-
Saratani ya pancrease
​
Soma zaidi kuhusu kutapika sana wakati wa ujauzito kwa kubonyeza hapa
​
ULY CLINIC inakukumbusha uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua zozote zile za kiafya
​
​
Imeboreshwa mara ya mwisho 01.6.2020