top of page

Kikokotoo- Kipimo cha mimba

Jinsi kinavyofanya kazi

Kikokotoo cha Kupima Mimba hukusaidia kujua ni lini kipimo cha mimba kinaweza kutoa majibu sahihi, kulingana na tarehe ya uovuleshaji au tarehe ya kwanza ya hedhi yako ya mwisho.

Hatua za kutumia

  1. Chagua tarehe ya uovuleshaji au siku ya kwanza ya hedhi ya mwisho (LMP) kwa kutumia kalenda ya kikokotoo.

  2. Weka urefu wa mzunguko wako wa hedhi (mfano: 28 kwa mzunguko wa kawaida).

  3. Bonyeza kitufe cha "Kokotoa".

 

Kikokotoo kitaonyesha

  • Tarehe ya kukadiriwa kushika mimba

  • Tarehe ya kipimo cha mkojo kinachoweza kuonyesha matokeo sahihi

  • Tarehe ya kipimo cha damu (huweza kutoa majibu mapema zaidi)

  • Umri wa mimba kwa siku na wiki (ikiwa mimba imefanikiwa)

Maelezo muhimu

  • Kipimo cha damu kwa kawaida huweza kuonyesha ujauzito kuanzia siku 7–10 baada ya uovuleshaji.

  • Kipimo cha mkojo (kwa kutumia strip) huwa sahihi zaidi kuanzia siku 14 baada ya uovuleshaji.

  • Tarehe hizi ni za kukadiria – ili kuthibitisha mimba, vipimo vya kitaalamu au ushauri wa daktari ni muhimu.

  • Kikokotoo hiki kinafaa kwa wanawake wenye mzunguko wa hedhi kati ya siku 20 hadi 45.

bottom of page