top of page

Imeandikwa na  ULY-Clinic

 

 

 

Kupata mshindo bila kutoa manii/shahawa- Azoospermia

​

Hutokea endapo mwanaume amefika kileleni bila mbegu kutoka kwenye uume, au kutoa mbegu-manii kidogo sana. Manii ni mchanganyiko wa majimaji na mbegu za kiume.

 

Hali hii mara nyingi huwa sio hatari, lakini inaweza kusababisha tatizo la kisaikolojia kwa mwanaume, pia huweza sababisha kukosa mtoto.

 

Huweza kutokea kama matokea baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuondoa tezi dume, na mitoki inayozunguka maeneo ya tezi na upasuaji wa kuondoa kibofu cha mkojo. Miongoni mwa upasuaji uliotajwa hapo juu huweza kusababisha kutopata mbegu wakati wa mshindo.

 

Kwa baadhi ya nyakati mbegu huzalishwa na kuingia katika kibofu cha mkojo badala ya kutoka nje ya mwili wakati wa kufika kwenye mshindo. Mara nyingi huletwa na upasuaji wa kuondoa tezi dume ama matumizi ya baadhi ya madawa na magonjwa fulani.

​

Baadhi ya visababishi huwa ni kutozalishwa kwa manii ya kutosha ili zitoke wakati wa kufika kileleni au kufika kileleni mara nyingi zaidi. Hata hivyo hali hii huisha baada ya wiki chache.

 

Visababishi

​

​

Imeboreshwa, 2.12.2020

Anchor 1
bottom of page