top of page

Imeandikwa na daktari wa ULY clinic

​

Kuwahi kufika kileleni/ kuwahi kumwaga shahawa

 

 

Kuwahi kufika kileleni (kumwaga shahawa mapema) hutokea pale mwanaume anapomwaga shahawa mapema tofauti na matarajio yake au mpenzi wake.

Kama unafika kileleni mapema mara kwa mara, itakubi utafute msaada wa kiafya, lakini endapo ni mara chache basi huna haja ya kuhofia maana hutokea kwa wanaume wengi.

​

Ili usemekane kuwa unawahi kufika kileleni, utakuwa unawahi kumwaga manii ndani ya dakika moja unapoingiza mboo kwenye uke, unashindwa kuzuia shahawa kutoka wakati wa tendo mara nyingi au karibia mara zote na unajihisi haupo sawa katika tendo na wakati mwingine unaogopa kushiriki kujamiiana kwa sababu ya woga wa kuwahi kumwaga shahawa.

 

Mambo ya kisaikolojia na kifiziolojia huchangia mtu kuwahi kumwaga shahawa wakati wa tendo. Hata hivyo matibabu yapo,  hivyo usiwe na hofu.

 

Kuwahi kufika kileleni kunaweza kugawanywa katika makundi mawili, kundi la kwanza ni tatizo la maisha ikiwa inamaanisha toka uanze kushiriki kujamiana umekuwa unamwaga upesi. Kundi la pili ni tatizo linalopatikana baadae ikiwa inamanisha ulikuwa na uwezo wa kuchelewa kumwaga lakini sasa unamwaga shahawa mapema zaidi ya matarajio yako.

 

Visababishi

​

Kuna visababishi vya kisaikolojia, kibayolojia na visababishi vingine

 

Visababishi vya kisaikolojia

​

  • Kuwahi kuanza kufanya ngono

  • Kufanyiwa ukatili wa kingono

  • Mwonekano dhaifu wa mwili

  • Msongo wa mawazo

  • Hofu ya kuwahi kumaliza

  • Kujihisi umekosea na ukaenda kushiriki tendo

​

Unahitajika kuwa na barua pepe ili kuendelea kusoma zaidi makala hii. Bonyez ahapa kuendelea kusoma kuhusu 

​

Visababishi vya kibayolojia, Visababishi vingine, Vihatarishi, â€‹Madhara​, Matibabu

​

​

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako endapo unashida yoyote ya kiafya kabla ya kuchukua uamuzi unaozuru afya yako.

 

Wasiliana na daktari wa ULY clinic kwa kubonyeza ‘Pata Tiba’ au kupiga namba za simu chini ya tovuti hii.

​

  1. Ferri FF. Ejaculation and orgasm disorders. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 8.5.2020

  2. Wein AJ, et al., eds. Disorders of male orgasm and ejaculation. http://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 8.5.2020

  3. Siegel AL. Pelvic floor muscle training in males: Practical applications. National Institute of Diabetes and Digestive and Kidney Diseases. https://www.niddk.nih.gov/health-information/health-topics/urologic-disease/urinary-incontinence-women/Pages/insertC.aspx. Imechukuliwa 8.5.2020

  4. Harvard health publishing. Premature Ejaculation.https://www.health.harvard.edu/a_to_z/premature-ejaculation-a-to-z. Imechukuliwa 8.5.2020

  5. NHS. Ejaculation problem. https://www.nhs.uk/conditions/ejaculation-problems/. Imechukuliwa 8.05.2020

bottom of page