Mwandishi:
Mhhariri
ULY CLINIC
Dkt. Benjamin L, MD
Jumatatu, 8 Novemba 2021

Kirusi cha corona
Virusi vya corona ni familia kubwa ya virusi inayosababisha binadamu kuugua, mtu anaweza kupata dalili kali na kutokwa mafua au kuwa na dalili kali na za ghafla zaidi kwenye mfumo wa upumuaji.
Kwanini kirusi huyu anaitwa corona
Jina la kirusi cha corona limetokana na neno la la kilatini "corona" ikimaanisha "taji" na kirusi huyu aliitwa hivyo kutokana na muonekano wa sura yake kuwa kama taji ya mfalme.
Aina
Aina ya virusi vya corona kwa binadamu.
Virusi vya corona vipo duniani kote, kuna aina saba (7) ya virusi ambavyo wanasayansi wanavifahamu kuwa vina athiri binadamu na kuwafanya waugue.
Baadhi ya virusi hawa waligunduliwa zamani sana na wengine wamegunduliwa hivi karibuni. Virusi vya corona wanaweza sababisha homa kiasi au homa kali sana.
Wapo Virusi wawili waliojulikana hivi karibuni kusababisha binadamu kuugua mara kwa mara ambaao ni kirusi aina ya SARS-CoV na kirusi cha MERS-CoV
Virusi aina nyingine ni pamoja na;
229E(alpha)
NL63(alpha)
OC43(beta)
HKU1(beta)
2019 nCoV
Aina gani inadhuru sana binadamu?
Watu wengi duniani wanaathiriwa na kirusi cha 229E(alpha), NL63(alpha), OC43(beta) na HKU1(beta)
Kirusi cha corona anaweza kubadilika asili yake mara anapoingia kwa binadamu na kuwa kirusi mpya mfano wa virusi wapya ni virusi aina tatu vilivyogunduliwa hivi karibuni ni SARS-CoV, MERS-CoV na 2019 nCoV.
Kirusi cha corona pia huweza safari kati ya binadamu na Wanyama mfano popo, paka, ngamia n.k. Jamii fulani ya virusi hawa wanaonekana kuambukizwa kutoka kwa Wanyama mfano kirusi cha SARS-CoV kimeonekana kuambukizwa kati ya paka na binadamu na cha MERS-CoV kati ya ngamia na binadamu.
Dalili
Dalili za ugonjwa huu ni;
Homa
Kikohozi kibichi
Kuishiwa pumzi
Kupata shida ya kupumua(Uhemaji wa tabu)
Mwili kuuma
Homa kali ya mapafu
Mtindio wa ubongo
Dalili zingine zinaweza kuwa;
Kuhara
Kutapika
Kichwa kuuma
Kukohoa damu
Maumivu ya kifua
Wakati gani unaweza kupata dalili baada ya maambukizi?
Kirusi cha korona kwenye mwili wa binadamu huchukua siku 2 mpaka 14 (wastani siku 5) kuanza kuonesha dalili baada ya kuambukizwa na virusi vya korona
Maambukizi hutokeaje?
Kirusi cha corona huambukizwa kwa njia ya matone yatokanayo na kukohoa au kugusana moja kwa moja na mgonjwa au vitu vilivyoguswa na mgonjwa.
Dalili kali huwa pamoja na dalili za nimonia, dalili za figo kufeli kufanya kazi, mkusanyiko wa dalili za kuathirika kwa mfumo wa upumuaji
Mambo ya kufanya yaliyoshauriwa na CDC pamoja na shirika la Afya Duniani WHO ili kuzuia maambukizi ni pamoja na
Kutoenda maeneo ambayo yana mlipuko wa ugonjwa huo mpaka usalama uwepo au kupata ushauri wa CDC na WHO
Nawa mikono mara kwa mara kwa kutumia sabuni na maji, au kutumia sanitiza
Funika midomo na pua kwa kutumia kiwiko cha mkono unapopiga chafya au kukohoa
Kuacha kugusa macho, pua na mdomo endapo mikono yako si safi
Acha kutumia vyombo, miwani, kitanda vifaa vingine pamoja na mtu anayeumwa kirusi huyu au kama wewe ni mgonjwa
Kutokaa karibu na mtu ambaye ana dalili za kuumwa kifua kama vile kukohoa na kupiga chafya
Kusafisha maeneo unayoshika mara kwa mara kwa kutumia dawa za kuua na kuondoa vimelea vya maradhi.
Kukaa nyumbani ukitoka kazini, acha kukaa kwenye mazingira ya watu wengi endapo wewe ni mgonjwa ili kuzuia maambukizi kwao
Kupika vema mayai na nyama
Mambo ya kufahamu pia
Jinsi unavyoshika vitu mbalimbali unakusanya vimelea vya kutosha kwenye mikono yako na unaweza kujiambukiza na vimelea hivyo endapo utashika pua, macho au mdomo.
Kutumia sabuni kunawa mikono na maji kwa sekunde 20 au kutumia sanitiza huondoa vimelea kwenye mikono yako.
Video fupi yanamna ya kunawa mikono