Mwandishi:
Mhhariri
ULY CLINIC
Dkt. Mangwella S, MD
Alhamisi, 11 Novemba 2021
Sindromu ya kuingia hedhi
Zaidi ya asilimia 75 ya wanawake waliovunja ungo hupata dalili na ishara za kuingia hedhi kila mwezi kama vile kukasirika kirahisi, kuvimba na msongo wa mawazo. Dalili zikiwa kali na kudumu, onana na daktari kwa msaada zaidi.
Sindromu ya kuingia hedhi ni dalili na viashiria vinavyoonekana kabla ya kuingia hedhi kwa mwanamke aliye jwenye mzunguko wa hedhi ya kila mwezi. Dalili na viashiria hivyo huonekana siku 10 hadi 11 kabla ya kuingia hedhi na huisha ndani ya siku 4 baada ya kuanza kuona damu ya hedhi.
Dalili
Kwa sasa kuna jumla ya dalili 150 za kuingia hedhi ambazo huweza kutofautiana kila zinapotokea na kati ya mwanamke na mwanake.
Dalili kuu za kuingia hedhi huhusisha;
Kutaka kula chakula aina Fulani tu
Ongezeko la njaa
Kukasirika kirahisi
Hofu kuu
Kubadilikabadilika kwa hali ya moyo
Kutokwa machozi kirahisi
Sonona
Hasira
Kukanganyikiwa
Madhaifu ya kulala
Kujitenga na watu
Uchovu
Maumivu ya kichwa
Maumivu ya tumbo
Maumivu ya mgongo
Maumivu ya misuli na maungio
Kutokwa na chunusi
Kuharisha au haja ngumu
Kutostahimili kilevi
Maeneo gani ya mwili huvimba?
Maeneo ya mwili yanayoathiriwa na uvimbe ni kati ya;
Uso
Matiti
Juu ya kitovu
Kwenye kitovu
Kinena
1/3 ya katikati ya mkono
Mkono wa mbele
1/3 ya katikati ya miguu
Mapaja yote
Makundi ya sindromu ys kuingia hedhi
Sindromu ya kuingia hedhi zimegawanywa kwenye makundi manne yafuatayo;
Kundi A
Dalili na viashiria kwenye kundi A ni;
Hutawaliwa na hofu iliyopitiliza
Kukasirika kirahisi
Kutotulia
Kundi C
Dalili na viashiria kwenye kundi C ni;
Maumivu ya kichwa
Ongezeko la njaa
Hamu ya kula vitu vitamu
Uchovu mkali wa mwili
Hisia za mapigo ya moyo
Kutetemeka mwili
Kundi D
Dalili na viashiria kwenye kundi D ni;
Sonona
Kukosa usingizi
Kulia kirahisi
Kuongezeka uzito
Kundi H
Dalili na viashiria kwenye kundi H ni;
Mwili kutunza maji
Kuvimba matiti
Tumbo kujaa gesi
Kuongezeka uzito
Wakati gani wa kuonana na daktari?
Dalili na viashiria vya kuingia hedhi vinapaswa kupotea ndani ya siku 4 baada ya kuanza kuona damu ya hedhi. Onana na daktari kwa msaada zaidi endapo;
Unapata dalili kali za kuingia hedhi
Dalili haziishi hata baada ya kuingia hedhi
Unapata dalili kali kilw mwezi zinazoathiri ubora wa maisha yako
Unahisi una sonona, mabadiliko ya hisia, hasira, kuhisi za kulemewa na mambo, kushindwa tafakarina kukasirika kirahisi.
Visababishi
Mabadiliko ya homoni
Dalili na viashiria vya kuingia hedhi hubadilika kulingana na mabadiliko ya homoni yanayotokea mwilini na hupotea kwenye ujauzito na baada ya kuingia kipindi cha komahedhi.
Mabadiliko ya homoni ndani ya ubongo
Mabadiliko ya homoni ndni ya ubongo kama vile kupungua kwa homon serotonin, huchangia sana kuamsha mabadiliko ya hali ya moyo na kuamsha dalili za kineva kama vile kula sana, uchovu na matatizo ya kulala.
Sonona
Baadhi ya wanawake wenye dalili kali za kuingia hedhi huwa wana sonona ambalo halijatambuliwa bado, licha ya sonona kutosababisha dalili zote za kuingia hedhi.
Vipimo na utambuzi
Hakuna ishara au vipimo maalumu kwa ajili ya sindromu ya kuingia hedhi, hata hivyo endapo una dalili ambazo zinatabirika, yaani ambazo zinatokea kila mwezi karibia na au wakati wa hedhi, dalili hizo zinawezakutumika kutumiwa na daktari kutambua tatizo hili.
Ili kuweza kutambua dalili zinazotabirika za kuingia hedhi, unapaswa kuandika kwenye kalenda au kitabu cha kumbukumbu kila dalili unayopata kwa angalau miezi miwili. Dalili hizi utampatia daktari wako ili aweze kutambua kama zinahusi
ana na dalili za hedhi au la, nakupanga matibabu yako kama yatahitajika.
Kama una dalili zinazoashiria magonjwa Fulani yanayoweza fanana na sindromu ya kuingia hedhi, vipimo maalumu vitafanyika.
Magonjwa yanayoofanana na sindromu ya kuingia hedhi
Baadhi ya magonjwa yanayofanana sindromu ya kuingia hedhi ni pamoja na;
Madhaifu ya thyroid
Madhaifu ya kuingia hedhi
Sonona
Wasiwasi uliopitiliza
Matibabu
Wanawake wengi wenye sindromu ya kuingia hedhi wanapofanya mabadiliko ya maisha ya kila siku huweza kudhibiti sindromu ya kuingia hedhi au kutumia dawa kama dalili ni kali zaidi.
Matibabu ya dawa
Ufanisi wa dawa kuthibiti dalili hutegemea kati ya mtu na mtu. Baadhi ya dawa zinazotumika sana ni;
Dawa za kuondoa sonona mfano dawa kundi la selective serotonin reuptake inhibitors (SSRIs) ambazo ni fluoxetine, paroxetine, sertraline na zingine.
Dawa za maumivu jamii ya NSAIDs kama vile ibuprofen na naproxen
Dawa za kupunguza maji mwilini jamii ya diuretic kama vile Spironolactone (Aldactone)
Vichochezi wa uzazi wa mpango. Huzuia kuzalishwa kwa yai.
Mabadiliko ya maisha
Unaweza kudhibiti dalili na viashiria vya kuigia hedhi kwa kurekebisha unachokula, kufanya mazoezi na kukabiliana na mambo.
Kurekebisha unachokula
Kula kiasi kidogo cha chakula na mara kwa mara ili kupunguza gesi tumboni na hisia za tumbo kujaa
Dhibiti kiasi cha chumvi unachokula kwa siku ili kupunguza kutuwama kwa maji mwilini
Kula chakula chenye kabohydrate tata kama ile inayotoka kwenye matunda, mboa za majani na nafaka zisizokobolewa
Kula vyakula vyenye calcium kwa wingi kama maziwa, kama huwezi kunyw amaziwa unaweza kutumia vidonge vya calcium
Jiepusje kutumia kahawa na kilevi
Mazoezi
Fanya kazoezi angalau kwa muda wa dakika 30 kwa siku siku 3 au zaidi kwa wiki.
Kabiliana na msongo
Unaweza kukabiliana na msongo kwa;
Kufanya mazoezi
Kulala muda wa kutosha
Kufanya tafakuri
Kufanya yoga au masaji ili kupunguza msongo
Matibabu mbadala
Kuna matibabu mbadala ya kudhibiti sindromu ys kuingia hedhi ambayo yameonekana kufanya kazi kwenye tafiti mbalimbali, baadhi yake ni;
Matumizi ya dawa viinirishe tiba kama vile vitamin na madini mfano vitamin E, B6
Matumizi ya mitishamba kama ginko, tangawizi, chasteberry, St. John's wort n.k.
Acupuncture
Kumbuka
Kumbuka
Usitumie dawa za mitishamba bila kuwasiliana na daktari ili kufahamu kama zina mwingiliano na dawa za hospitali.
Majina mengine
Sindromu ya kuingia hedhi hufahamika kwa majina mengine ya;
Premenstrual syndrome
Sindromu ya kuingia hedhi
Sindromu ya hedhi
Dalili za kuingia hedhi
Viashiria vya kuingia hedhi
Dalili na viashiria vya kuingia hedhi