Dalili za mgonjwa wa TB
Imeandikwa na madaktari wa uly clinic
Dalili za mgonjwa wa TB hutegemea mambo mbalimbali ikiwemo umri na hali ya mtu kuwa na magonjwa mengine ama ugonjwa huu umesambaa au umeathiri maeneo gani mengine ya mwili mbali na Mapafu
Dalili kwa ujumla kwa mtu yeyote huweza kuwa kama zifuatazo
-
Kukohoa mfululizo kusikopungua wiki mbili
-
Kupata homa kwa mda wa mwezi mzima
-
Kupata jasho jingi (kiasi cha kulowanisha mashuka) wakati wa usiku
-
Kupungua uzito kusikoelezeka na sababu yeyote
-
Kukohoa damu
-
kupoteza hamu ya kula
-
Maumivu ya kifua ama kushindwa kupumua vizuri
-
Mwili kuchoka
Dalili ambazo zinatokea kwa watu walioathirika na maambukizi ya HIV ama watu wenye kinga za mwili za chini sana huwa ni
-
Kupungua kwa uzito
-
Homa am homa inaweza kuwa hamna
-
Wakati mwingine hata kipimo cha makohozi kikichukuliwa huweza kusomeka kwamna mtu hana TB na hali anayo, hivyo kipimo cha Gene expert na Xnray hufanyika
Wazee na watoto hawawezi kuonyesha dalili tambulifu za TB kwa sababu ya kinga ya mwili inayopambana na maradhi hayo kuwa chini hivyo huwa na dalili za pneumonia isiyopona
Dalili za ugonjwa wa TB kusambaa huweza kuwa
TB ya moyo- maumivu ya kifua ama kushindwa kupumua vema na kulala chali wakati wa usiku ama kuamka wakati wa usiku kwa kukosa hewa safi
TB ya ubongo- mtu anakwa na maumivu makali ya kichwa kwa mda wa wiki mbili ama tatu kabla hajjapoteza fahamu ama kuchanganyikiwa
TB ya uti wa mgongo- Mgonjwa anapata ugonjwa unaoitwa pott disease, mifupa ya uti wa mgongo hulika na kupinda. Dalili zinaweza kuwa kama vile , maumivu makali nyuma ya mgongo, kukakamaa kwa uti wa mgongo, na kupata gaanzi ama kupalalizi miguuni.
TB ya Mfumo wa uzazi na mkojo
Mgonjwa anapata maumivu ya nyonga na chini ya mbavu, kushindwa kukojoa, kukojoa mara kwa mara, ama mkojo kutoka kwa maumivu. kwa wanaume wanaweza kuvimba korodani ama mapumbu na kuwa na maumivu makali sana. Kwa wanawake wanaweza kupata.
TB ya mfumo wa chakula
-
Kupata vidonda mdomoni visivyopona
-
Ugumu katika kumeza
-
Maumivu ya tumbo kama vile ya vidonda vya tumbo
-
Maumivu, kuhara, kuhara damu,
TB ya Mitoki
Kuvimba mitoke sehemu zote za mwili ama maeneo ya
Shingo makwapani na kwenye nyonga
Toleo la 2
Imeboreshwa 6/1/2019